Ajali: Basi la Kampuni ya BM Coach lapinduka wakati likikwepa Kichwa cha Treni (kiberenge) maeneo Chekelei

Basi la Kampuni ya BM Coach limepata ajali ya kupinduka leo majira ya Alasiri Machi 4, 2019 wakati likijaribu kukwepa Kichwa cha Treni (Kiberenge) maeneo ya Chekelei wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa dereva wa Basi la BM Coach, akitoka Arusha kuelekea Morogogo alishindwa kusimama katika kivuko cha Treni eneo la Chekelei Mombo, barabara kuu ya Segera/Same.

Ameongeza kuwa; wakati kichwa cha Treni kikikaribia eneo hilo na ndipo basi hilo likagongwa na kulala ubavu huku kichwa hicho cha Garimoshi kikiendelea na safari bila kusimama.

Hakuna taarifa ya vifo kwa sasa isipokuwa abiria kadhaa wamejeruhiwa akiwemo dereva wa BM Coach ambaye ameumia sana. Amesema kamanda wa polisi mkoa wa Tanga.View attachment 1037885View attachment 1037887View attachment 1037888
Miaka ya sitini hapo iligongwa basi wakati wa usiku na kuua idadi mkubwa ya manesi wanafunzi.
 
21st century. I have seen in many countries such intersections controlled by machine and no need of constant attendance of personnel. Yes, its money. But accidents, injuries and time lost costs more.
 
BM Ina mabasi mapya na mazuri ila uongozi wake wasipokuwa makini izo bus zitaogopwa.Kama Route ya Arusha Dar kupitia chalinze,kuna DEREVA wa V.I.P konda wake ni mwanaume,hua ana mbio bila hesabu,kuanzia anavyotoka SHEKILANGO abiria ni Roho mkononi.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Makutano ya njia za gar na tren huwa pameandikwa stop.

Kwahiyo ukifika hapo kama una gar yakupasa usitop then utazame pande zote kama hakuna kiberenge bas unaweza endelea na safari zako

Ni hayo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo alama haitoshi, utaratibu wa kusimamisha magari ndio suluhu tosha.

Madereva wengine akili zao wanazijua wenyewe, atahisi kusimama kwa hiari anapoteza muda ukizingatia treni ndefu hadi ipite yote. Ndio maana wanaamua kupita ili waiwahi treni/kiberenge hatimaye wanagongwa
 
Poleni wote mliofikwa na Adha hiyo.

Kwenye hayo mapishano ya Reli, hakuna watu wanaocontrol magari(kusimamisha magari) pindi treni inapopita?

Au huo mtindo wa kufunga barabara kwa muda ili Treni ipite upo mijini tu?
Inatakiwa kutumia taaluma yako ya udereva ulivyofundishwa chuoni simama ukifika kwenye railway cross na kuangalia pande zote mbili Kama kuko salama vuka.

Mtagongwa wengi tu kwa kuvuka kienyeji
 
Ajali hutokea mahali popote siku yoyote lakini mimi nilishajiapiza kwamba sitakuja kupanda bus la BM ni bora nikodi bodaboda...

Hili basi liliwahi kunipindua pale daraja la mto Ruvu natokea Moro naenda Dar alaf kwa makosa ya kizembe sana...

Ukifuatilia ajali nyingi za BM ni kwa sababu ya uzembe wa madereva and they don't care... Yani sijui hata kama wanachukuliwa hatua, I gues wanawachukua madereva wasio na viwango pengine kukwepa gharama za kuwalipa wenye weledi...

Poor BM
 
Inatakiwa kutumia taaluma yako ya udereva ulivyofundishwa chuoni simama ukifika kwenye railway cross na kuangalia pande zote mbili Kama kuko salama vuka.

Mtagongwa wengi tu kwa kuvuka kienyeji
Sasa kama taaluma haitumiwi, nini kifanyike?

Mimi nimependekeza pawepo na utaratibu wa kuzuia/kusimamisha magari pindi treni inapopita kama ilivyo sehemu za mijini.
 
Back
Top Bottom