Ajali : basi la best line na MWANZA COACH

Ajali : basi la best line na MWANZA COACH

Kiba

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2012
Posts
459
Reaction score
62
Kumetokea ajali mbaya ktk eneo la STOP OVER barabara ya Mwanza Musoma iliyokutanisha basi la Mwanza coach lililokuwa likielekea Mwanza na Best line lilikua likielekea Musoma . Mabasi haya yalipishana kwa ukaribu kitendo kilichosababisha bodi kugongana .
Watu saba wamepoteza maisha hapo hapo akiwemo dereva wa Best line.
 
daa juzi mombasa raha imesababisha watu saba kupoteza maisha huko bariad leo tena best line na mwanza coach, asubuhi nilisoma humu kuna ajali ya mabasi mawili kutokea dar..Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi ameni..
 
Ni kweli ajali mbaya sana imetokea nilifikapo jana ndg zetu saba wamepoteza maisha na walio mahututi ni 14 hali zao sio nzuri
 
Hiyo ajali ni mbaya sana kwani nimepata kuiona kupitia ITV katika taarifa ya habari jioni hii ila hakika ni ajili mbaya sana ndugu zanguni.............ni MUNGU pekee akasimame na hizi vyombo vya moto tunazosafiri nazo..............marehemu wote MUNGU awape pumziko njema shambani mwake Bwana na hata majeruhi MUNGU wetu usiwapite wape nguvu wapone mapema warudi katika afya njema!!!!
 
Back
Top Bottom