Ajabu Mbunge Kenya hulipwa 14m kwa mwezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajabu Mbunge Kenya hulipwa 14m kwa mwezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzalendoHalisi, Feb 14, 2009.

 1. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Ni ajabu ila kweli kuwa mshahara Mbunge Kenya ni 14m Tshs kwa mwezi!

  Hii iko hata juu ya malipo ya wabunge Uingereza!

  Je mnasemaje JF wakati wandugu kibao Kenya wanakufa njaa kwa kukosa chakula?

  Mwalimu Primary Kenya hupata tu laki 2 (200,000 Tshs).

  Jamani Jf mnasemaj tofauti hii kubwa hivi kwa wanasiasa?

  Nini mchango wa wabunge ktk jamii?? Kupiga domo?

  Kumbuka uchaguzi ndo ulileteleza mauaji wa 1500 citizens!

  Je tunawahitaji wabunge ili iweje????
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Unaweza kutupatia source ya hii finding?
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  This is a fact not an opininion!

  Je huamini?

  Uliza mtu mtu yoyote toka Kenya!

  Mbunge hulipwa 800,0000 Kshs wakati huu wa Kibaki!

  Sasa unataka ushaidi gani zaidi???

  Source: Treasury Kenya!
   
  Last edited: Feb 14, 2009
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Halafu walimu Kenya wakigoma wanaonekana wanafanya uhaini... Potelea mbali!
   
 5. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni ajabu kwa nini??

  Uingereza ni gold standard ya nchi zingine au?!

  Hii inawasaidia kupunguza ufisadi. Ndio maana wanazidi kuendelea.
   
 6. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwenye nchi za wenzetu zilizoendelea siasa kwa kiasi kubwa ni kutumikia watu ......kwa maana kuwa kwa walio wengi hukiingia kwenye siasa mapato yanapungua ila kwetu Afrika siasa ndio njia ya kutokea....iwe kwa mtu binafsi, familia yake au ndugu na jamaa wote jicho litakuwa kwako mwanasiasa.

  Ndio maana tunashuhudia watu wanauana, wanachafuana na kufanyiana kila namna ya visa kwa ajili siasa.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mukulu, unaweza tu kuwa humble na kusema kiungwana 'sina source', huna haja ya kuwa hysterical.


  Asante.
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...wabunge wa Tanzania nakumbuka mpaka miaka mitatu iliyopita walikuwa wanapokea;

  30,000,000/= kila wakimaliza miaka yao mitano.
  1,000,000/= Constituency Allowance kila mwezi
  600,000/= monthly Allowance
  95,000/= sitting Allowance

  na bado kuna wengine waliokuwa wanaona ubahili kuwalipa hata madereva wao...

   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Maneno mazito haya mzee.

  Mimi binafsi siamini ktk siasa maana ishu nzima tunayoiita 'demokrasia' is based on a fallacy. Na hii sio hapa Tz tu, bali ulimwenguni kote. Kutegemea mchezo wa kuigiza unaoitwa siasa ili kuleta maendeleo is not realistic to me.

  Mimi naamini ktk utaalamu na si siasa, hususan za nchi zetu zilizo masikini wa kutupa. Tunahitaji jopo la wataalamu, wa fani na nyanja mbalimbali wenye uchungu na nchi na wanaojua majukumu yao, washike hatamu kutuongoza. Ili nchi isonge mbele katu haihitaji wanasiasa ambao ktk nchi zetu wamegeuka walafi, wahunzi wa machafuko na hata kuwaibia wananchi masikini wazi wazi bila aibu.
   
  Last edited by a moderator: Feb 14, 2009
Loading...