AJABU: Chenge aitetea DOWANS ilipwe!

Hongera chenge, Bravo Fisadi masterminder,
Waonyeshe njia, watanabaishe kuwa hii nchni haina dola wala kiongozi yoyote anayeweza kuwazuia nyie kufanya lolote mnalotaka.

Wadhiirishie kuwa kelele za chura (Nape) hazimzui mgombe kunywa maji (Fisadi hatetereki).
Waambie kwa vitendo kuwa hakuna aliye juu yenu hapa katika ardhi ya Tanzania, waambie hao wasiokujueni kuwa hata raia hawawezi ni mwenzenu.

Kazi nzuri sana chenge Bravo! Kwani ulipowaambi wewe unavijinti kwani si walibisha! Mbona walipojua ya EPA, Meremeta na Dowans walikubali kuwa zako kweli vijisenti!
 
Kwa maelezo yako ni kama unataka kutuambia kwamba Chenge anajua sheria sana siyo?Inawezekana anaijua sheria lakini kujua kwake sheria hakujaisaidia hii nchi.Serikali iliingia kwenye mikataba mibovu ya madini Chenge akiwa mwanasheria mkuu je wwakati huo alikua haijui hiyo sheria?au aliijua ila alikua ana masilahi binafsi?na kama niko sahihi basi hata sasa inawezekana ana masilahi binafsi kwenye hili suala la Dowans.Hoja si kujua sheria tu,na hiyo sheria unaiyumia vipi kwa masilahi ya Taifa!
 
Hawa jamaa hawana huruma kwakweli.

Moja ya sababu ya umaskini wa watanzania ni kuwa wanawaonea huruma mafisadi wanaosababisha uchumi wao uzorote wakati wenyewe hawaionei huruma nchi. Ili nchi yetu iendelee ni lazima viongozi wetu waache kuchekacheka na kuwaadhibu wahalifu kwa mujibu wa sheria zetu hata ikibidi zibadishwe. Nchi ya China kwa mfano imepata maendeleo yake kwa kasi kwasababu hawawaonei huruma mafisadi na ndio maana wakipatikana hupewa hukumu ya kifo; hata hapa karibu kwetu Africa, nchi ya Ghana ilipokombolewa na Lt. Rawlings kitu cha kwanza alichofanya ni kuwanyonga mafisadi wakina Achempong na genge lake na ndio maana tunaona hali ya uchumi ya Ghana imekua kwa kasi kubwa!!! Tusipochukua hatua madhubuti dhidi ya ufisadi kila siku tutakuwa watu wakulalamika kuwa hatujui chanzo cha umaskini wa nchi yetu.
 

mkuu nakuunga mkono asilimia 100.. wote tukifuata ushauri wako tutalikomboa taifa letu
 
Reactions: EMT
Uamuzi aliouchukua Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Mzee wa vijisenti/'Mr. Clean) wa kuongeza nguvu Dowans kwa kutoa ushauri wa kisheria ili ilipwe bilioni 94 na Tanesco=Tanzania, unadhihirisha jinsi alivyoumizwa na uamuzi wa chama chake CCM wa kuvuliwa gamba na sasa ameamua kuwasaidia Dowans ili Tanzania ilipe mabilioni ya fedha. Ikumbukwe huyu jamaa alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na amesaini mikataba mingi na huenda alishirikishwa kwa kuomba ushauri katika suala la Dowans lakini leo ameamua kuvuaa miwani ya mbao na kuitetea.
 

ENYI WANA WA TAMAA! Wekeni mbali vazi la majivuno na mjivue vazi la ufedhuli.ewe asili halisi ya shauku! Weka mbali tama na tafuteni kuridhika kwa maana mwenye tamaa daima amenyimwa, na mwenye kuridhika daima amependwa na kusifiwa na mngu
 
U wapi uzalendo wa viongozi kwa Taifa lao.,bila hata aibu unaisaidia kampuni 'inayoidai' serikali unayoitumikia ili iweje?.Nilitegemea angesaidia serikali na nchi yake isiingie au jinsi ya kujitoa katika katika migogoro ya kisheria...

Nani kakwambia kuwa nchi hii ina viongozi wazalendo?Huoni jinsi mambo yanavyokwenda, wachimbaji wadogo wakijigundulia madini na kuanza kujitafutia riziki kesho yake viongozi wako hao unaowaita wazalendo wanawaita wawekezeji uchwara na kuwatimua wananchi.
 

Mkuu umenena vyema. Chenge kama mwanasheria ana haki ya kufanya hivyo. Tatizo ni hao walioingia mkataba huo ambao pamoja na wanasheria wao. Pia kuna wanasheria walioshauri mkataba uvunjwe na kisha wanasema ni haki tozo ilipwe. Tuasiangalie tulioangukia, tuangalie tulipojikwaa.
 


malalamiko menngi ya nini? ukilalamika unapata faida gani??

Kwani si yote haya kila mtu anayaona listen my friend everybody for himself but God for us all
 
Awali nilidhani upo humu kutetea CCM na mafisadi kumbe I was wrong. Wewe upo si kwa ajili ya CCM ila kwa ajili ya JK na udini.
Hilo nimelinusa. Hata hivyo wenye fikra pevu wanakudharau.
Mkuu kumbe ulikuwa haulijui hilo? wenzio tulishamshitukia kitaaaambo
huyo ni mdini sana alafu ni mchawi
 
Chenge anaweza kuwa ni mjuvi wa sheria anayoitumia kwa maslahi yake binafsi na ndiyo maana 'mtaalamu mzanzibar' J Shamhuna alimtolea uvivu pale alipojidai kupindisha vifungu ilhali akijua kabisa kuwa wazenji wanatambua kuwa znz ni nchi.
 


so unataka tufanyeje embu sometimes tuwe tunaongea vitu vya msingi vinavyo tupleka kwenye solution ya hilo jambo sio malalamiko tuuuuu
 
Mwizi mkubwa huyu na alipokuwa AG alitumia elimu kuibia watanzania kwa kusaini mikataka ya kifisadi na sasa anaendeleza ufisadi
 

Tatizo ni kwamba Sehemu ambayo akili inapaswa kuingilia Umeifunika. Nenda kavue huo ujinga kwanza ndipo ubongo wako ufunguke na kuchangia points zenye akili. Nyau we!!
 


Kuna jopo la wanasheria wa CCM waliojitolea kuitetea Serikali ndidi ya mzigo huu wakiongozwa na Mh. Nimrodi Mkono; ina maana Mh. Chenge hakuwa mmoja wa hilo jopo?
 
ENYI WANA WA TAMAA! Wekeni mbali vazi la majivuno na mjivue vazi la ufedhuli.ewe asili halisi ya shauku! Weka mbali tama na tafuteni kuridhika kwa maana mwenye tamaa daima amenyimwa, na mwenye kuridhika daima amependwa na kusifiwa na mngu


Asee hili andiko nimelipenda liko kwenye kitabu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…