katika kudhihirisha uswahiba na ufisadi wa mapacha watatu,chenge amewasilisha pingamizi la kisheria kutetea dowans ilipwe na serikali ya tanzania.source nipashe leo
Bongolala, wakati nasubiri kulisoma hilo Nipashe, ningependa kusisitiza mahitaji ya kisheria na mahitaji halisi ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ya kisheria ni laz`ima yatekelezwe no matter what, hata kama sio mahitaji halisi.
Tozo la Dowans lililotolewa na ICC ni hitaji la kisheria, kwa mujibu wa mkataba husika, uamuzi wa ICC ni uamuzi wa mwisho, haupingiwi na mahakama yoyote labda kufanyiwa mapitio na ICC yenyewe, hivyo kitendo cha kuusajili mahakama za nchini, ni kwa lengo la kuusajili uamuzi ule kwa utekelezaji tuu.
Siungi mkono tozo hiyo ya ICC kwasababu sio tozo halali, ila kisheria, maadamu wanasheria vichwa maji wetu waliukubali ule mkataba, na hivyo ndivyo mkataba unavyosema, then tozo hiyo imehalalishwa na mkataba mbovu ule, hivyo toso ile ni halali kisheria.
Nawaombeni wana jf na wananchi wote wa Tanzania, lazima tuukubali ukweli mchungu kwa kumeza kidonge kichungu cha tozo hii, tutatake tusitake, lazima tutalipa tuu, hatuna popote pa kutokea unless Tanzania kama nchi, tujitoe ICC na kuwafukuzia mbali hawa wanyonyaji wote wanaojiita wawekezaji wa kwendo makao n a mitaji yao, wakatumie fedha zao kutengeneza madini yao na sisi watuachie almasi zetu, Wasukuma tuzichezee bao, na dhahabu zetu tuziache humo humo ardhini, tubaki na umasikini wetu huku tumekalia malia zetu, kuliko kuwaruhusu wazipore kubadilishana na pipi huku wakituacha na umasini wetu palepale.