AIYOLA- Riwaya murua

AIYOLA.......3
AUTHOR.......MWL.SADALAH
CONT......0629306194
WHATSAPP.....0768552126
ILIPOISHIA..
Walishangaa kumkuta mzee mfupi akiwa ametapakaa damu na pembeni walimuona mtu akiwa amelala. Kama ujuavyo watu wenye hasira kali hawakutaka kuuliza hapohapo wakaanza.kumshambulia. moja kwa moja walijua huyo ndiye aliyesababisha mauaji kutokana na mazingira waliyomkuta.
SONGA NAYO...
Kutokana na wingi wa watu hao. Walitumia dakika chache sana kuuondo uhai wa Mzee Juma.
"Oya leteni kuni"
"Kwani hatuwezi kupata PETROL"
"Pale kw Mzee Jofley naona kama taili hebu vijana wawili walifuate"
Sauti hizo zilisikika bila mpangilio maalumu. Kazi ya kuua ilikuwa imeisha kilichokuwa kinafuata hapo ni kumchoma moto.
Baada ya dakika tatu wakawa wameleta taili la gari wakakusanya kuni kidogo na Mzee mmoja mvuta sigara akajipapasa kwenye koti lake akatoa kiberiti aina ya SPRINGBOK SAFETY MATCH na kuwasha moto.
Kilichokuja kuwashtua hapo ni gari lililokuwa limewasha taa likija kwa spidi ya ajabu sehemu walipo..
"Polisi.. Polisi..polisi"
Kelele hizo zilitotolewa na mwana mwano mmoja baada ya kugundua kuwa gari hilo lilikuwa ni la polisi. Wote wakaanza kukimbia na kutokomea sehemu mbalimbali na hata gari hilo lilipofunga breki na kusimama, hawakakata mtu hata mmoja sehemu hiyo ya tukio. Hawakuwa na jinsi ya kufanya, moto ulikuwa umeshika kasi ukitema cheche. Wakasubiri hadi ukazimika baada ya kichwa cha binadamu huyo kupasuka.
********
Kesho yake asubuhi askari hao waliwakamata vijana waliokuwa wanapita eneo hilo, wakashirikiana kuuhifadhi mwili wa Mzee Juma uliokuwa umeharibiwa vibaya na moto. Mwili wa Mama Jamali ulichukuliwa na Mzee Abdul Baba mwenye nyumba mahali anaishi. Kwa heshima na kufuata taratibu zote za kiislamu wakauzika mwili wa Mama huyo. Familia ya Mzee Abdul ikasimamia gharama zote za msiba. Ulikuwa ni msiba ulio hudhuriwa na watu wengi sana. Viongozi mbalimbali wa kisiasa na wale wa dini mbalimbali walikuwepo na hata pale walipopata muda wa kuzumza baada ya mazishi hawakusita kuongea.
"Ndugu mkuu wa wilaya, ndugu diwani wetu wa Uyovu, ndugu RPC, Mzee mwenye nyumba, mabibi na mabwana asalaam aleykum."
Ilikuwa ni shekhe wa msikiti wa Runzere Alhaj Manzil bin Shabaan. Alianza na salamu kwanza kisha akaendelea baada ya wote kuitikia.
"Binafsi nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za msiba huu jinsi ulivyotokea. Ni wazi inajidhihirisha kwamba wanaadamu tumekuwa na roho ya kinyama. Tunashindwa kufuata maarisho ya munyazimungu subuhana wataala......" (Akendelea kuongea.)
Aliongea maneno machache ila yalikuwa mazito sana na kila mtu yalimuingia. Alitoa mifano ya Aya za kwenye Quani na kutafsiri kwa kiswahili. Baadhi yao walilengwa na machozi. Alipomaliza akakaa na wengine wakaongea. Akapewa nafasi ya kuzungumza mkuu wa Wilaya mheshimiwa Melyaria Mgeta akaomba kama kuna msamalia mwema akabidiwe rasmi Mtoto Jamali na serikali itakuwa inatoa msaada wake ili kuhakikisha Mtoto huyo anapata mahitaji ya muhimu. Mama mmoja alijitokeza na hapohapo akakabidhiwa pesa taslimu shilingi laki moja na nusu na kuahidiwa kila mweze awe anafata shilingi elfu themanini kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya.
**********
Wengi walipenda kumuita Mama Jose kwa kutumia jina la mme wakea aliyekuwa anaitwa Joseph shimbi. Hawakubahatika kupata mtoto japo familia yao ilikuwa ya amani. Walikuwa na kashamba, nyumba mbili sa kawaida pamoja na duka la nguo. Baada ya kuishi kwa muda wa miaka minne ndani ya ndoa. Mme wake alipatwa na ugonjwa wa ajabu. Hata walipompeleka hospitali haikusaidia. Maiezi mitatu baadae alifariki na kumuacha mama huyo mjane. Aliishi na upweke kwa miaka mitatu huku akiendeleza mradi wa kuuza nguo alizokuwa anafuata Kampala. Akakabidhiwa mtoto mdogo amlee. Si mwingine bali ni Jamali. Alifurahia maisha ya kuishi na mtoto huyo akampenda na kumthamini kama mtoto wake wa kumzaa.
"Mamaaaa..."
"Unasemaje mwanangu"
"Jully mchokozi"
"Kakufanya nini tena huyu jully"
"Eti kaniambia nina kichwa kama embe"
"Nitamchapa.....!!!!, hebu nyamaza Baba"
Alikuwa ni Jamali mwenye miaka sita akisema kwa mama yake baada ya kuyaniwa na Jully mtoto wa jirani aliyekuwa mtundu kama nini.
*************
Siku zikazidi kwenda,miaka ikahesabiwa huku Jamali akiendelea na shule. Alijaliwa akili sana hata matokeo yake ya darasa la nne alikuwa wa kwanza ngazi ya wilaya na akawa mtu wa nne kimkoa. Matokeo haya yalimfurahisha sana mkuu wa wilaya na kuupalilia moyo wake wa kujitolea.
Darasa la tano alianza huku akiwa na akili aleile. Walimu shuleni walimpenda hata wanafunzi wenzake walimpa ushirikiano. Alisoma kwa bidii sana. Hakuwa mbinafsi, aliwasaidia wanafunzi wenzake waliokuwa wazito kitaaluma darasani. Hakika mambo yalikuwa mazuri sana.
"Jamaliii..... we Jamalii"
"Naaaaam Mommy"
"Amka Baba uende shule mbona leo umelala sana kulikoni"
"Mmmm..... Usingizi halafu mwili wote umechoka"
"Unaumwa....?"
"Hata siumwi"
Siku hiyo ilikuwa jumatano Jamali anaamshwa na mama yake ili aende shule. Siku hiyo Jamali alikuwa mzito sana haikuwa kawaida yake hata yeye mwenyewe alijishangaa. Aliamka na kwenda kwa mama yake. Alipofika akawekewa mkono shavuni iliapimwe joto ila ilkuwa kawaida. Akampa chai akanywa alipomaliza akaoga harakaharaka akavaa nguo zake za shule, akachukua begi lake la madaftari kasha akakimbia kwenda shule japo ilikuw anakaribia saa mbili na nusu.
STORY HII UNAWEZA KUIPATA YOTE WHATSAPP NA FACEBOOK INBOX KWA SHILINGI 2500 AU VIPANDE VITANO KWA SHILINGI 500
KWA STORY ZAIDI LIKE PAGE PENDWA YA MWL SADALAH
Facebook - Connexion ou inscription
mwlbarakasadalah/
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom