Nduhu tabu
Member
- Jul 21, 2017
- 90
- 99
AIYOLA
SEHEMU.........01
AUTHOR.......MWL.SADALAH
CONT.....0629306194
WHATSAPP........0768552126
Chini ya mti wa muembe, uliokuwa nje kidogo ya kijiji sofu,kata ya kwala,wilaya ya kisarawe, mkoa wa pwani mashariki mwa nchi ya Tanzania. Alionekana kijana mmoja aliyekuwa amekaa chini ya jiwe lililokuwa kando ya mti huo. Alionekana kuchoshwa na hali ya umasikini na alikuwa kwenye dimbi zito la mawazo. Alikuwa alikuwa amevaa suruali nzito ya jinsi iliyojazia uchafu na kuifanya ionekane nyeusi, shati jeusi lililo chanika, na chini alikua amevaa viatu vya wazi yaani sandals sijui aliziokota wapi. Usingeweza kumtofautisha binadamu huyu mwenye akili zake timamu na vichaa wanaoranda mitaani na kwenye madampo ya uchafu. Alionekana dhaifu sana nadhani shauri ya njaa na ni ndovyo ilivyo kuwa.shingo yake ilikuwa imepinda kidogo na kufanya kichwa chake kitulie vyema kenye magoti yake.
"Oya oya" ilikuwa ni sauti aliyoisikia vyema kutoka nyuma yake na kumfanya ashtuke kidogo kwa unyonge akageuza shingo yake na kumtazama mtu aliye mshtua.
"Vipi ndugu yangu nimekuona hapa muda mrefu na unekana kama hauko sawa"
Akauliza.
Jamaa akasita kidogo kisha akaguna na kumjibu.
"Daaaah!!!! We acha tu bana"
"Kulikoni"
"Maisha kaka"
Baada ya kauli hiyo yule jamaa akahisi kuna kitu kwa huyo jamaa akaainama na kumshhoka bega kisha akamwambia
"Naitwa jamali sijui mwenzangu unaitwa nani vile"
"Mi naitwa paschal matogwa" akajibu kwa kujitambulisha
"Sijawahi kukuona hapa Sofu wewe ni mwenyeji wa wapi bwana paschal"
"Samahani nikuombe kitu"
"Usijali we omba tu hata usiwe na wasiwasi"
"unaweza kuendelea na safari yako tu"
paschal akamwambia jamali, kisha akainama tena alionekana kukereka na maswali mengi aliyokuwa anaulizwa.
Ukimya mdogo ukapita na baadae વjamali akaonekana kama anafikilia kitu kisha કakaanzisha tena mazungumzo
"Usiseme hivyo રndugu yangu mi ni mtu mwema japo sina uwezo ila ninaweza kukusaidia "
"Unataka kunisaidia kweli" akauliza paschal.
"Kama jambo liko ndani ya uwezo wangu naweza kukusaidia kweli. Paschal akamwangalia jamali kwa kumdadisi kisha.
વ"labda kweli anaweza kunisaidia au ndo walewale tu" akawaza paschal "ila ngoja nijaribu tena" akaendelea kuwaza, akakumbuka mateso aliyoyapata kwa miongo miwili sasa, akamkumbuka mpenzi wake pros, picha ya wazazi wake wawili baba na mama take ikapita akilini mwake. Haraka haraka akayakumbuka maisha yake ya nyuma yakamjaza maumivu.
"Vipi wewe...." Sauti ya jamali ikamuamsha tena kutoka alipokuwa ameinama na safari hii uso wake ulikuwa umejaa machozi
"Na...o..mba uni..sa..saidii.ie cha..cha...kula na maji" Akaomba paschal kwa kwikwi na kwa sauti ya chini
Jamali akazidi kuzungukiwa na roho ya huruma. "Mi ni maskini na nina shida ila huyu jamaa anashida sana tena zaidi yangu lazima nimsaidie" akawaza jamali kisha akamshika mkono, akamuomba waongozane kwenda nyumbani kwa jamali. Taratibu akaanza kujikongoja huku akisaidiwa kutembea hakika alikuwa amejichokea sana. Haikuwa mbali sana waliweza kufika nyumbani kwa jamali.
***************
Mwezi desemba Mwaka 1979 mzee juma alirudi kutoka katika mapigano ya vita vya Tanzania na Uganda wengi hupenda kuita vita vya kagera. Alifika Moja kwa Moja kijijini kwao kasulu mkoa wa kigoma na akawakuta ndugu zake, waliomlaki kwa furaha hawakuanini kama Huyo ndugu yao amerudi akiwa mzima maana vita ni kama mnavyojua kufa au kupona. Alifanyiwa sherehe kubwa ya kumkaribisha nyumbani, watu wakala, wakanywa na wakacheza mziki. Watu wengi kutoka kila sehemu walihudhuria sherehe hiyo isipokuwa MTU mmoja, tena mtu wa karibu sana na familia hiyo. Siyo mwingine bali ni mke wa mzee Juma. Aliogopa na hakujua atamweleza nini mume wake. Wakati anaenda kupigana alimuacha mke wake na watoto watatu. Akiwa huko make wake alikosa uvumilivu na akajikuta anachepuka na kupata mimba hatimae mtoto wa nne ambae siyo wa mzee juma. Hakutegemea kama itakua hivyo na ndiyo sababu ilimfanya aende akajifiche katika kijiji cha Runzewe akiwa yeye na mtoto wake mmoja alikuwa anaitwa jamali mtoto huyu alikuwa na umri wa miezi mitatu tu. Huko akawa anajishughurisha na biashara ndogo ndogo ya kuuza ndizi mbivu.
Baada ya kukaa kijijini huku, taarifa ya mke wake kujifungua akawa ameshaambiwa na waongo si unajua tena vijijini. Taarifa hiyo ilimfanya ajenge chuki dhidi ya mke wake akawaza kuja kumfanyia kitu kibaya pindi atakapo mtia machoni. Alikaa kijijini hapo kwa miezi mitatu huku akifanya upererezi, na hatimae alijua sehemu alipo. Siku hiyo hiyi jioni alichukua kisu chake akakieka kiunoni na akaenda stend tayari kwa safari. Kama bahati Siku hiyo alipata basi la kwenda kahama lililokuwa limecherewa akapanda tayari kwa safari.
Alifika Runzewe saa mbili usiku, kwa kuwa alikuwa anaijua mke wake anajishughurisha na uuzaji wa ndizi. Alienda kwenye genge la jioni na alikusudia kuondoa uhai wa mtu leo leo. Kama bahati alimuona kwa mbali na roho ya kinyama pamoja na hasira ikamjaa. Akaamua apoteze muda kwenye kijiwe cha kahawa kilichokuwa jirani na gange hilo. Baada ya kama nusu saa alimuona mama Huyo aliyekuwa make wake akikusanya vitu, akambeba mwanae mgongoni ambae ni Jamali kisha akaanza kuelekea alikokuwa anaishi. Bila kuchelewa juma naye alisimama na kuanza kumfatilia. Alitembea umbali mdogo akaziacha taa na kuingia gizani. Hapa ndipo Mzee Juma naye aliongeza mwendo na akafanikiwa kumpata.
Story unaweza kuipata yote kwa tsh 2500 whsapp au Facebook in box kwa sh. 500 vipande vitatu.
Huu ni mwanzo tu je, ni nini hatma ya Mama huyu, hatma ya paschal na hatma ya Jamali.
Coment
Like
Share
Itaendelea.......