Aishi na Maiti ya Mama Yake Kwa Miaka 6 ili Kuchukua Mshiko Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aishi na Maiti ya Mama Yake Kwa Miaka 6 ili Kuchukua Mshiko Wake

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Sep 24, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>


  Penelope Sharon Jordan
  Thursday, September 24, 2009 3:24 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuihifadhi maiti ya mama yake chumbani kwake kwa kipindi cha miaka sita huku akijipatia isivyo halali pesa za kiinua mgongo chake.


  Penelope Sharon Jordan, 61, mkazi wa Florida, Marekani alihukumiwa jumatatu kwenda jela mwaka mmoja na siku moja kwa kuiweka maiti ya mama yake nyumbani kwake kwa miaka sita huku katika kipindi chote hicho akifanikiwa kuchukua kiinua mgongo cha mama yake zaidi ya $230,000.

  Awali Penelope alifikishwa mahakamani mwezi juni mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za wizi wa pesa za serikali.

  Polisi waliugundua mwili wa mama yake baada ya Penelope kuwaruhusu polisi waingie nyumbani kwake mnamo mwezi machi mwaka huu.

  Mwili wa mama yake ulikutwa ukiwa umeoza kitandani kwenye mojawapo ya vyumba vya kulala vya nyumba yake.

  Penelope aliwaambia polisi kuwa mama yake alifariki zaidi ya miaka sita iliyopita kutokana na magonjwa ya uzeeni.

  Wakati wa uchunguzi wa kesi hiyo iligundulika kuwa Penelope alimwambia dada yake kuwa mama yao alifariki kabla ya mwezi disemba mwaka 2001.

  Uchunguzi wa maiti ya mama yake haukuonyesha kama Penelope alihusika na kifo chake.

  Penelope awali alidai alikuwa hana pesa za kumzika mama yake lakini baadae alikiri mahakamani kuwa aliiweka maiti ya mama yake chumbani kwake ili aendelee kuchukua pesa zake za kiinua mgongo.

  Polisi walisema kuwa maiti ya mama yake ingeweza kuendelea kuoza kwenye nyumba hiyo kwa miaka kadhaa kwasababu kulikuwa hakuna ndugu wa karibu aliyekuwa akimtembelea Penelope mara kwa mara.

  Penelope alitakiwa na mahakama akitoka jela azirudishe serikalini pesa alizochukua kama kiinua mgongo cha mama yake kiasi cha $237,876.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  duniani kuna mengi ukistaajabu ya musa utaona filauni sijui kama nimepatia message
  Hiyo maiti ilikuwa haitoi harufu
  na miaka sita hiyo maiti ilikuwa imeshakauka kuna watu wana roho ngumu sana sijui ni mashetani???:eek:
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  binadamu tuko tofauti kwa kweli, mhh
   
Loading...