Aisee, kumbe mapenzi ya kweli yapo hadi leo?

Aisee, kumbe mapenzi ya kweli yapo hadi leo?

Poleni na majukumu wakuu! Niende 1kwa1 kwenye Mada husika Toka nikiwa mtoto nimekua mtu wa kuwaogopa Sana watoto wa kike hadi mwaka huu nimemaliza degree yangu Sina ujasiri na watoto wa kike nikitaka nifloo nae na maongezi ni hadi anisogelee hapo nitaongea japo kwa less confidence.

Lakini Hata hivyo, Hali hii imenisaidia kumpata girlfriend ambaye naamini Ana mapenzi ya kweli na mimi. KWANINI?

SABABU: Toka nimekua nae kama rafiki yangu wa kike (tumesoma darasa 1 chuo ki1),
Nimeshuhudia mengi Sana. 1 Kati ya hayo ni hili, nimejaribu Kua na mahusiano na mabint kadhaa wakati yeye yupo (japo sio kwa kumaananisha) aise amewapindua wote yani kila binti alikua anamface 1kwa1 ili amwambie amwache mme wangu miaka mi3 yote hadi tumemaliza chuo na ni , zaidi ya mabinti 4. angekua Hana mapenzi na mimi angenitua huu ndo ukweli.

Jingine licha ya kumfanyia yote hayo wiki ilopita amekataa barua ya posa kwao kwa ajili yangu image Nina kabint kengine then yeye anajua halaf kwao Kuna jamaa kajitokeza amuoe lakini amechomoa.. Hii ni kali kwa ninavyowajua hawa viumbe sidhani kama angekubali kuendelea tena Na mimi.

Nawakumbusha tena mapenzi ya kweli yapo haijalishi wote mmefanana level za elimu, uchumi au amekuzidi au umemzidi. Wanawake wanapenda Mbaya mbovu.

Nawasilisha karibuni kwa upembuzi wa kina zaidi. Asanteni
Common things are common but rare things happen.
 
Kuna usemi "Ukiona jogoo kwa mganga ujue manyoya yake yamemponza" Sasa we huyu demu unayemsifia juzijuzi tu watu wamrkula mithili Samaki kibua. Akiosha na Coca anakuja kwako. Hivi nyie wasomi wetu kweli? Mbona sie babu zenu hatuwa hivyo?
 
Chukua simu ya mpenzi wako ukae nayo japo lisaa limoja tu
Usipoona maruerue mle,ndi ujihakikishie mapenzi ya kweli bado yapo

Dunia hii ya leo labda upendane na Tarzan tundio mkweli
Manake TARZAN hajawahi ishi na binaadam tangu azaliwe
 
Samahan mkuu nimesoma linguistic hiyo ni Aina flani ya uandidhi tu.. Kwenye topic fulani ya Stylistics haimzuii mtu kuongea au kuandika Aina fulani ya uandidhi au uongeaji ilimradi tu nisiharibu Maana ama content.
Ndg msomi na muhitimu wa chuo kikuu Hiyo stylistics yako haiapply Kila mahali. Unafikiri Kila mtu angetumia language stylistic codes anazozijua angetosha hapa?
 
Mdogo wangu...!! Usijiaminishe na wala Usijihakikishie, ya chuoni ni yakichuoni tu, huku kitaa ni dunia ingine kabisa...!! Si ajabu baada ya muda flani utatuandikia tena ukiomba ushauri.

Kuna wahanga wengi aisee..!
 
Sio kwa dunia ya sasa

Nina wasiwasi na huyo mwanamke
 
Chukua simu ya mpenzi wako ukae nayo japo lisaa limoja tu
Usipoona maruerue mle,ndi ujihakikishie mapenzi ya kweli bado yapo

Dunia hii ya leo labda upendane na Tarzan tundio mkweli
Manake TARZAN hajawahi ishi na binaadam tangu azaliwe
Nimewahi kaa nayo Mara nyingi Sana sijaona lolote
 
Back
Top Bottom