Kwanini isiwe RFA, EA Radio au Magic FM pamoja na hiyo mawingu zote kwa pamoja zijiangalie?! Yaani wabongo hatuwezi kusifia kitu bila ya kukiponda kingine?! Efm wanafanya vizuri sawa, lakini kuilinganisha na Clouds ni sawa na kumuiga tembo kunya! Karibia redio zote za fm wameiga kila kitu kutoka Clouds. Tofauti ya Efm ni Bwakila, kuongeza muda wa kujadili michezo na kupiga singeli tu. Radio ambayo iko tofauti na nyingine ni RFA tu, nayo inafeli tu, sababu ya kisiasa. Efm onakuja vizuri, lakini haijafikia kiwango cha redio ya watu. Na kudhihirisha ubora wake ni kitendo cha kulinganishwa na kila kituo kinachoanzishwa Bongo. Clouds ilikuwepo hata kabla wengine hawajaja mjini na kipindi hicho Dj.majizo anahangaika na daladala beats yake pale magic. Na nimegundua watu wengi humu wana chuki na mawingu. Ila ni asili ya watanzania kumchukia mtu aliyefanikiwa. Mungu atunusuru na hii tabia.