Aisee Dharau Zimezidi (ujobless kazi sana)

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Aisee Dharau Zimezidi (ujobless kazi sana)

Yaani nimevumilia ila nimeona Leo niandike tu, yaani nipo home Sina kazi na kudharauliwa kumeongezeka

Yaani naambiwa nitenge chakula mezani na mdogo wangu wa kike yupo sebuleni anatazama TV na Hana kazi yoyote, na nimempita mbali tu kiumri.

Natumwa dukani nikanunue kweli vitu vidogo vidogo kama nyanya, vitunguu, mafuta nk na sio vitu vya jumla yaani vidogo vidogo na wadogo zangu wa kike wapo tu wametulia nyumbani,

Na anayonifanyia hayo ni Maza mdogo

Wadau mnanishauri vipi?
 
Ushauri uko wazi toka nenda katafute.

Wewe ni mtoto wa kiume, kugombania remote na dada zako ni upumbafu.

Amka asubuhi sepa, tafuta hata ka kibarua usichague kazi.

Ukipata buku 3, buku 2 weka akiba, buku nunua kafungu ka ndizi mbivu rudi nazo wape hapo kwenu. Wataanza kukuheshimu.

Lakini unaamka asubuh unakuna pumbuw unaanza kufungua hotpot lazima uonekane kipele
 
Sio kwa ubaya ila mtoto wa kiume jobless sasa unakaaje ndani tu? Yaani unashinda home kwanini usitumwe? Hebu toka nenda kijiweni huko utapata hata mishe nenda kawe hata saidia fundi kuwa hata winga beba hata mizigo bhana mwanaume umeumbwa kula kwa jasho jishughulishe usipojishughulisha utashughulishwa na ukiendelea sooon utapangiwa zamu ya kuosha vyombo shauri yako.
 
Mkuu wewe si upo Mambele USA wenzako tunatafuta connection ya kufika huko sasa imekuwaje uwe Jobless ?
Screenshot_20230810-135159~2.png
 
sio kwa ubaya ila mtoto wa kiume jobless sasa unakaaje ndani tu? yaani unashinda home kwanini usitumwe? hebu toka nenda kijiweni huko utapata hata mishe nenda kawe hata saidia fundi kuwa hata winga beba hata mizigo bhana mwanaume umeumbwa kula kwa jasho jishughulishe usipojishughulisha utashughulishwa na ukiendelea sooon utapangiwa zamu ya kuosha vyombo shauri yako
😀😀😀Poa poa Asante ,nimekuelewa ntafanya kama ulivyonielekeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom