Airtel...wameshindwaje?nini tatizo?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Wakati fulani dunia hii ilikuwa karibu nusu ya simu zote za mikononi
ni NOKIA...walilishika soko la dunia nzima
Hata Iphone zilipoanza ilikuwa inasemwa Iphone wanauza simu za mwaka mzima
ambazo NOKIA wanauza katika wiki moja...

Hata hivyo kampuni ya NOKIA ikaishia kufilisika na kuuzwa..maneno maarufu ya CEO wao yalikuwa haya 'We didn't do anything wrong,but somehow we lost'

Sasa juzi niliposikia Airtel wamefilisika na sasa wanafanya restructuring na kupunguza
wafanyakazi....swali la kwanza nililojiuliza ni..'wamekosea wapi'?

Airtel ni kampuni ya tatu now kwa ukubwa Tanzania kwa kampuni za simu kwa idadi ya wateja
ilikuwa ya Pili nyuma tu ya VODA...wakati fulani..

Huduma zao hasa internet zinaaminika kuliko hata wengine kama Tigo...

matangazo ya biashara wapo vizuri kila mara wanakuja na ubunifu mpya
mara 'hamia Airtel' mara 'hatupimi'...mradi...ukiwatazama huwezi sema
wanafanya 'makosa makubwa'....wakati kuna kampuni za simu zipo kama hazipo
mfano Sasatel,Smart,na zinginezo...ukisikia Airetel wamefilisika....unashangaa

na swali linabaki lile lile....'wamekosea wapi'?


Kuna watu ambao wanaweza saidia kujua nini hasa kimetokea kwa Airtel?
 
Uhuni wa kubadili badili majina na kutokuwa na msimamo, ona voda wanakomaa tu hata wateteleke vipi wamo tu,

Ss hawa airtel na tigo kidogo tu wanataka kukimbia,
 
The Boss.....nokia kikubwa walichoshindwa ni kwenda na mabadiliko...mimi nilibahatika kuongea na aliekua mfanyakazi wa NOKIA yaani alilalamika sana kuhusu uongozi....hasa wkt wa mapinduzi ya "mechanical phones" kwenda smart phones hapo ndipo walipokosea...wenzao walipokua wanabadili technology wao waliamini kile walichoona na ukizingatia walikua na jina kubwa walizania hawataweza shindwa hivyo walibakia na mechanical phones aka nokia za tochi...kulikua na proposal nyingi sn zililetwa kwa ajili ya kufanya watu wa move from nokia za tochi kwenda smart phones but wao walibakia static tu hawakuamini mawazo ya wengine at the end wenzao walikua mbali wkt uongozi unakuja funguka kua tunatakiwa kwenda nokia smart phones....kwa upande wa airtel hakuna tofauti sn...wanaamini wao ni best ...mawazo yao ni best (managements) na hio ndio inayowaangusha....ukiangalia vitengo vyao karibia vyote vimekua outsourced wale unaoaona pale kazi yao ni kusaini karatasi tu but in terms of technology it is outside their hands....waliamini wanapunguza matumizi kumbe wanaua kampuni wenyewe...huo ndio uelewa wangu mdogo THE BOSS
 
Mkuu The Boss kufanya restructuring siyo kufilisika. Ni kubadili namna ya uendeshaaji wa biashara ili usipate hasara kubwa na uweze kunufaisha wanahisa wako. Restructuring ni kujipanga upya tu.
 
Mkuu The Boss kufanya restructuring siyo kufilisika. Ni kubadili namna ya uendeshaaji wa biashara ili usipate hasara kubwa na uweze kunufaisha wanahisa wako. Restructuring ni kujipanga upya tu.

Wametangazwa kufilisika
hkuona magazeti?
 
Mkuu The Boss kufanya restructuring siyo kufilisika. Ni kubadili namna ya uendeshaaji wa biashara ili usipate hasara kubwa na uweze kunufaisha wanahisa wako. Restructuring ni kujipanga upya tu.
Ni kweli kufanya restructuring sio kufiliska ila nikutaka ku-copy na mdundo wa soko.

Hawa jamaa wameona scale haiendi kwa ufanisi hivyo hawana budi kuweka mambo sawa. January walitangaza kufanya haya ila naona hawakuwa serious kivile wenzao Voda January walishalifanya.
ac2352d86f846e8d991a788b440ebc3d.jpg
 
Back
Top Bottom