Airtel Wagoma Kumlipa Mshindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Airtel Wagoma Kumlipa Mshindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Mar 13, 2012.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,102
  Likes Received: 341
  Trophy Points: 180
  Shame shame shame on you airtell
  niliwahi kuandika hapa thread ya watanzania mnaibiwa na mitandao msikimbilie hizi takataka
  zinaitwa ati shindano ...shindano la....uhuni mtupu..kuna mtu aliipgiwa simu akaambiwa na tigo
  atapewa kiasi kadhaa atangazwe mshindi tangu kesho ssina hamu na haya mashindano yao

  soma tanzania daima pg 4
  mteja kilema aiburuza mahakamani airtell
  mteja wa kampuni ya simu za mkononi airtell bernad tobiasi ameiburuza kampuni ya airtell kwa kudai fidia ya million 60 kwa kumtangza mshindi wa promosheni ya kwanjuka sms.....lakini ikashindwa kumpatia million 50..

  Tobiasi ambae ni mlemavu wa miguu na mikono anatetewa na kituo cha haki za binadamu wakili fulgence massawe kwenye kesi ya madai namba 12/2012 ambayo tayari imeshapangiwa hakimu

  kwa mujibu w akesi hiyo tobiasi ambae ni mteja wa airtell mwenye namba 0686 163 144 tobiasi alianza kushiriki mashindano hayo tangu mei 2011 na mshindi alitakiwa kupewa million 50
  wakili massawe amesema mteja wake alitangazwa kuwa mshindi mwaka jana kw akupigiwa na mfanyakazi mwenye namba 0784 100 778

  wakili massawe anasema mteja wake alipanda gari kuja dar toka kijijini na alipofika kwenye ofisi za airtell aliambiwa yeye sio mshindi kabisa ..alipoanza kulalamika na kuanza kupiga simu kwa ndugu wa karibu alishangaa kuitwa na mmoja wa wafanyakazi na kuulizwa namba yake ..baada ya dk kadhaa akaja akamwambia yeye alijishindia million moja na sio million 50....akasema alipopigiwa aliambiwa million 50 na sio million 1..hata hivyo akasema wampatie million 1 akisubiri kueleweka kwa hiyo mil 49 iliobakia ambapo mpaka sasa hata miatano yaani sh 500 ajapewa na airtell

  katika kituko kisichovumilika wakili masawe anasema kabla ya kufungua kesi hii niliwasiliana na airtell ambapo walikiri kumpigia simu mteja huyo kama mshindi na kuwauliza kwa nini wanakataa kumlipa hela zake...kampuni ya airtell ilidai ilishangaa walipompigia waliongea na thobias lakini walipopga baadae akapokea mwanamke ambae ni mkewe....hata hivyo wakili massawe amaesema amewapelekea vithibitisho kuonyesha tobias nimlemavu wa masikio lakini akuna juhudi zilizofanywa kumlipa haki zake..

  Aidha alidai kwa kuwa kampuni hiyo ndio ilimpigia kama mshindi basi atawajibika kuhakikisha analipwa haki zake zote na hela yake million 50 pamoja na usumbufu wa million 10 jumla million 60..wakili massawe anaiomba mahakama iamuru mteja wake alipwe kiasi hicho na kutoa adhabu kali kama fundisho kwa makampuni yanayotumia bahati nasibu kudanganya watu kujipatia fedha zisizo halali kkwa kuwahadaa watu na kuwapiga picha huku awapewei pesa zao.....

  Kwa niaba ya wana jf mh wakili f massawe tuko nyuma yako na naamini upumbavu huu autorudiwa tena na mitandao ya simu na watanzania muache ujinga wa kupenda vya dezo na makampuni nayo yako kibishara zaidi wanacheza dili mnaona watu wanakabidhiwa million kadhaa mnahisi kwako ni rahisi

  mungu awapiganie kwenye kesi hii na ntaifuatlia mpaka mwisho wa hitimisho
   
 2. Deejay nasmile

  Deejay nasmile JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,916
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Dah! Lakini basi lao zuri
   
 3. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,721
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Aitel for internet servie tu. After all no free lunch in globalized world.
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,743
  Trophy Points: 280
  siku za mwizi 39 ya 40 lazma akamatwe wamezid kuchezesha mamichezo.feki na hatuoni zawadi zenyewe,
   
 5. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ok, wakili Massawe, tunashukuru sana kuwatetea wanyonge, lakini ngoja kwanza.

  Airtel wanasema walimwambia kashinda milioni moja, nyinyi mnasema jamaa alisikia milioni hamsini. Halafu unasema umethibitisha kwamba mteja ni mgonjwa wa masikio! Sasa how does that help your case?
   
 6. Root

  Root JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,165
  Likes Received: 12,877
  Trophy Points: 280
  alikuwa anachezaje wakati ni mlemavu wa mikono
   
 7. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145

  Wakili Massawe inabidi ujipange kwa mteja wako kuweza kushinda hii kesi.
   
 8. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kazi rahisi, ataomba mahakama itoe amri ya kuleta yale mazungumzo kwa simu, nadhani huwa yanakuwa kwenye record kwa muda kama yapo ni ushahidi tosha.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Je yule mshindi aliyeshinda vogue(Range Rover) la Airtel kutoka KIA ni mchongo hule?
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ilivyoandikwa habari hii inaoneka kama kuna kitu kinakosekana hivi! Mteja anasema aliambiwa/alisikia sh 50m halafu wanasema ni mlemavu wa kusikia!...sasa hili la ulemavu wa kusikia sioni ni vipi linaweza kumsaidia mlalamikaji katika kesi hii.

  Naamini mashindano haya yanakuwa na record hivyo kujua ni namba ipi ilishinda na ilishinda kiasi gani pengine sio kazi ngumu sana.
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hizi zawadi ni changa la macho
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Alaah! hivi kumbe kwenye haya makampuni ya simu kuna bahati nasibu? Mimi nina line ya Airtel kwa ajili ya modem yangu na si vinginevyo na hata zile bonus za muda wa maongezi ninazopewaga sijawahi kuzitumia hata siku moja, mimi shida yangu ni Internet tu basi. hizo promo nyingine nyinyi endeleeni nazo tu kwa muda wenu, mimi sihitaji usanii on my way.
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wapumbaf sana hawa pale Airport maeneo yote ya Cargo tunapa EDGE mpaka nimeamua kuhamia Sasatel, ukipiga simu, hatua kumi kuna bango kubwa kama mlima Hamia Airtel! Uzuir kwa mkakasi ndani kipande cha mti!
   
 14. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hivi na ile JACKPOT BINGO ya Mengi iliishia wapi?
   
 15. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  nimecheck na jamaa yangu wa Airtel zawadi za Kwanjuka zilikua kama ifuatavyo,

  Daily winner of TZS 1,000,000/=
  Weekly Winner of TZS 5,000,000/=
  Final Grand Prizes will be TZS 20,000,000/=

  sasa hiyo 50mil,kwenye list aliyonitumia siioni.Pengine nafikiri kuna tatizo somewhere,so far hizi promotion nadhani hazina longolongo,kwani walikua wakitoa list ya washindi na pia muwakilishi wa bodi ya bahati nasibu ya taifa yupo, na pia nafikiri huwa anapata copy ya washindi husika.pia tunaweza kucheck huko.Vinginevyo pia makampuni shindani yanaweza tia mkono kuandika hiyo habari.

  Nakumbuka Vodacom waliwahi kupata kashfa mwaka fulani walikua na promotion mbili mwaka huo.Kulikua na promotion ya Voda millionaire ,halafu ikafuata ya Motorola kama sikosei.sasa wakati wa promotion ya motorola Afisa anaeandaa Data base hakuwepo ili bidi aandae mwingine.Kituko kilitokea huyu Afisa akachezesha bahati nasibu kwa kutumia database ya vodaMillionaire,badala ya Motorola .wateja walipopigiwa simu kuuliza kama walishiriki hiyo promotion wakagoma.Ndipo Afisa muhusika aliporudi na kugundua jamaa alitumia wrong data base.
  Bodi ya michezo ilishauri ibaki hivyo mpaka siku za kudeclare mshindi zinapokwisha kisheria ndio irudiwe upya.basi waliporudia wakawa wamerekebisha kosa hilo.
  sasa la huyu bwana tunahitaji taarifa sahihi, ili tuweze check na wahusika tujiridhishe kama haya madai ni ya kweli,kuliko mtoa mada alivyogeneralise,Lakini nafikiri kuna tatizo la huyu mshindi,kutokuelewa alichoshinda.
  Ni kwa mtizamo na uelewa wangu tu.
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Acha dhihaka..hujafa hujaumbika
   
 17. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  kuna mtu nilimshangaa alipigishwa mipicha na Western Union kuwa kashinda 5m kumbe wamemshikisha 1.5m...wacha liwe zogo na mkewe....ndugu na jamaa pia wapambe baada ya kusoma magazeti na kuona kive ktk TV
   
Loading...