Airtel Money sasa inanipa mashaka

Hi,
Sio mara moja, ni zaidi ya mara mbili ndani ya mwezi mmoja airtel imekua ikiniweka roho juu. Nishawahi kulipia bundle la king'amuzi cha Azam kwa airtel money, ilichukua 5 days kuunganishwa na Azam. Kwa madai wao Azam hawawezi kuniunganisha mpaka wapate malipo kutoka Airtel Money. Kwa siku tano sikuweza kuangalia taarifa za habari, mpira movies n.k

Leo tena natuma pesa kwenda Vodacom (M pesa) ni shida. Aliyetumiwa hajapata, nishapiga simu kibao huduma kwa wateja, eti wananiambia pesa imerudishwa kwenye account yako wakati huku napata zero tu.

Ninachoumia zaidi kuna wahudumu wengine hawanipi matumaini ya kupata huduma kwa wakati. Sasa sielewi huu mtandao sasa ndo umeshindwa kabisa katika huduma za pesa au ni nini?

Nyie wakuu nanyi mwakutana na kero hizi......?
Huu mchezo upo hata tigopesa nililipia king'amuzi cha continental
Mkuu, pole sana! Nafikiri labda huna bahati nao. Mimi huwa wananielewa sana mpaka wananitafuta wenyewe!
Asante mkuu
 
Wife alinunua umeme kupitia airtel money alipata shida sana ya kuongea na wahudumu siku 4 siku ya tano ndipo ilitumwa meseji ya unit za umeme.
 
Bro yaani Airtel wapo vizuri labda mtandao. Usihame mtandao maana vodacom usijaribu maana ni jipu
 
Hi,
Sio mara moja, ni zaidi ya mara mbili ndani ya mwezi mmoja airtel imekua ikiniweka roho juu. Nishawahi kulipia bundle la king'amuzi cha Azam kwa airtel money, ilichukua 5 days kuunganishwa na Azam. Kwa madai wao Azam hawawezi kuniunganisha mpaka wapate malipo kutoka Airtel Money. Kwa siku tano sikuweza kuangalia taarifa za habari, mpira movies n.k

Leo tena natuma pesa kwenda Vodacom (M pesa) ni shida. Aliyetumiwa hajapata, nishapiga simu kibao huduma kwa wateja, eti wananiambia pesa imerudishwa kwenye account yako wakati huku napata zero tu.

Ninachoumia zaidi kuna wahudumu wengine hawanipi matumaini ya kupata huduma kwa wakati. Sasa sielewi huu mtandao sasa ndo umeshindwa kabisa katika huduma za pesa au ni nini?

Nyie wakuu nanyi mwakutana na kero hizi......?
Halotel mda si mrefu wataipindua Airtel
 
Back
Top Bottom