Mkamba Towo
Member
- Sep 10, 2024
- 6
- 6
Jana jumamosi saa 6 mchana Nilifanya muamala airtel money pesa ya kununua ticket ya kusafiria jana usiku kwenda kusheherekea Eid Mkoa fulani.
Airtel walikata hela ya nauli na ada yao ya huduma Tsh 900 kwa huduma hiyo. Hadi nafika kituoni kupanda basi jana saa 4 usiku muamala haujakamilika na hivyo sikuweza kupatiwa tiketi ikabidi niilipe hela nyingine kununua tiketi mpya.
Nikapiga simu huduma kwa wateja wakasema wana shida ya mtandao na muamala utakamilika ndani ya masaa 24. Hadi sasa masaa 36 yamepita holaa nimepiga simu 100 wanasema bado wana shida ya kiufundi na mbaya zaidi wamehamisha goli na kudai masaa 24 hayajafika kwani wao wanahesabu masaa ya muda wa kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 na kwa siku za kazi tu.
Hivyo Jumamosi na Jumapili haziehesabiki na hata kesho J3 na J4 ikiwa ni Eid bado sio siku za kazi hivyo masaa 24 yataanza kuhesabiwa J5 saa mbili asubuhi hivyo niendelee kusubiri.
Nimejuta kutumia huduma hiyo ya airtel.. Je wenzangu huko mlipo mna hali gani na huduma za airtel?