Airtel mnazingua

Airtel mnazingua

Voda niliwakimbia sababu ya vifurush vyao ni kuiba. Huku airtel najiunga la siku 3 kwa 1000. Shida sasa ni kwenye network. Unakuta kitu una-seach muda mrefu sana.
Kampuni za simu wote wezi tu. Wana balance hivi:
1. Wanakupa GB nyingi kwa spidi ndogo sana, mwendo wa konokono (low latency). Au
2. Wanakupa GB chache sana kwa spidi kubwa (hizi hutadumu nazo kbs) mwendo wa farasi.
Walivyo wahuni, hawawezi kukupa vyo viwili kwa pamoja, yaani wakupe GB kibao na latency kubwa. HAKUNA
 
Kizuri gharama mkuu!
Vod sio gharama tu ni wezi pia. Unaweza ukatupia kifurushi let say cha wiki. Unaweza ukajikuta hata mara 2 hivi,labda uko safarini,hujapata hata muda wa kuchat. Lakini unafika unakoenda kesho yake ufungue ili uanze kukitafuna hicho kivuruz chako cha wiki. Usije ukashangaa unaambiwa ur everything is empty. Ukiwauliza jamani nimetumia saa ngapi wakati ilikuwa moja,mbili,tatu? Watakuambia hivyo hivyo mjomba umetumia kimeisha. Juzi tu kati hapo nimemsikia magembez alikuwa wizara ya maji zamani,anawalalamikia wamempiga hela hivyo hivyo
 
Kampuni za simu wote wezi tu. Wana balance hivi:
1. Wanakupa GB nyingi kwa spidi ndogo sana, mwendo wa konokono (low latency). Au
2. Wanakupa GB chache sana kwa spidi kubwa (hizi hutadumu nazo kbs) mwendo wa farasi.
Walivyo wahuni, hawawezi kukupa vyo viwili kwa pamoja, yaani wakupe GB kibao na latency kubwa. HAKUNA
Mamaeee zao...! Nitawaendea sumbawanga tu na wizi wao
 
Si ni bora Airtel Bando lao huwa linakaa kaa kidogo.. Unawajua Voda wewe?
Kutokana na speed yao ndogo ndomana unaona kama bundle lao (airtel) linakaa lakini ukweli ni kuwa kiwango cha mb/gb unazopata voda, tigo, halotel na airtel ni kilekile, tofauti inakuja kwenye speed.
 
It has been launched in Dar only...

Upcountry huko wataendelea kupata Edge na H+...

(Now i know where you live...hahaha)
Mbona airtel wanayo 4G
Kwangu mie hakuna mtandao bora kama airtel...speed yake ni nzuri sana kwa matumizi yangu
 
Upo mkoa/wilaya/kijiji gani?

Coverage za mobile providers hutofautiana mkoa hadi mkoa...

Kwa hapo Dar tu unapata labda Voda yupo vizuri Mwenge na akawa vibaya Temeke etc...hata mikoani ipo hivyo na huko ndio zaidi...

The good about Dar, mitandao ya simu inafanya packet transmission/IP transmission kwa uwepo wa consortium fiber...

Lakini huko kaswenswe ni mwendo wa microwave kwa sana with an outdated equipments, alitumia babu hata mjukuu, lots of framelosses, bad QoS etc
 
It has been launched in Dar only...

Upcountry huko wataendelea kupata Edge na H+...

(Now i know where you live...hahaha)

Hahahahahah lakini sijawahi kuficha ninakoishi
 
Airtel net iko slow sana. Kwa nini msihamie 4G. Hata hii 3G ni kama haina kitu kabisa,ni kama 1G tu hivi.

Muda mwingine unashindwa hata kufanya biashara kwa sababu ya hili dude.

Juzi kati hapo mteja amekuja dukani anahitaji spare ambayo haijui mfanano wake.

Mimi mbio mbio nii-Google,weee aibu,inaseach tu mamaeee...!mteja nimemtuliza mpaka akaniachia hilo tusi hapo juu. Wiki hii ndio kabisaa.

Na huu uzi nimeurudia kuuandika na kuu-send mara ya pili. Ya kwanza ime-seach karibia dakika 3,ile niikate nianze upya,si ukapita nayo.
Siku nilipoenda ku swap line yangu ya airtel kwenda 4G ndio ilikua mwisho wa matumizi maana network ilikata jumla si 3G wala 4G iliyofanya kazi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sio kweli
Au ni wewe mwenyewe? Kama wewe mwenyewe nikupe hongera yako. Lakini huyo ana sura ya upole sana. Huyo hawezi kushusha nondo hizi,si kwa upole huo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom