Airtel mkiendelea kunitumia huu ujumbe nitawapeleka mahakamani.

Airtel mkiendelea kunitumia huu ujumbe nitawapeleka mahakamani.

ALPHRED MAHUNJA

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
308
Reaction score
161
Kuna namba 15033 inanitumia ujumbe kuhusu habari za soka kwenye namba yangu ya simu ninayoitumia ya mtandao wa simu wa airtel.waliniambia kama sihitaji huduma hiyo niandike stopnow kisha nitume namba 15033 ili kujiondoa nikafanya hivyo lakini bado wanatuma mbaya zaidi imekuwa fujo kila dakika chache na bila shaka wanakata pesa maana hakuna cha bure dunia hii. Hivyo mpaka ikifika kesho wakiendelea nakwenda kwa pilato.
 
hata mm wamenitumia na hela wanakata huu ni wizi wanalazimisha kwa nguvu kukata hela zetu. eti wanakutumia habari za soka nani anaeshindwa kupata habari za soka dunia ya leo?huu ni wizi airtel msipojirekebisha tutawakimbia
 
Washenzi sana hawa airtel wanaudhi sana hara customer care yao haina msaada kuna wakati napigiwa simu nikipokea nasikia matangazo yao ya biashara nimewapigia several times kuwaambia sitaki ujinga wao wa ku-draw attention yangu hakuna marekebisho yoyote wanafanya,

Binafsi nimeanza kuwachukia kwakweli maana simu yangu wameigeuza ubao wao wa matangazo ya biashara, looks like wamekosa kabisa njia za kuwavutia wateja

Kama wanaingia humu please acheni usumbufu mimi nikihitaji kujua au kupata taarifa zenu nitatembelea website yenu au nitawapigia lakini siyo kuja kuniharibia concentration yangu ya kazi kwa upuuzi wenu, please stop!!!!
 
Sasa kesi yangu itakuwa ya mfano(precedent) kwa mashauri yote yajayo yatakayokuwa na hali kama hii.Nakwenda court ili iwe fundisho kwa mitandao yote iliyosalia.
 
Wananiambia nipige namba 090100777 ili nipate kunena na mtoa huduma lakini hakuna hiyo huduma katika hii namba. huu ni wizi wa dhahiri
 
Naunga mkono hoja,jina la kesi litakuwa nini mkuu..?wanasumbua vbaya,mara meseji mara simu. Kila dakika kila saa....
 
nshawatukana tayari sijaomba hiyo huduma wanatuma msg kila saa
 
Mimi voda wananiboa huduma yao ya sokoni, kila nikiistopisha hawataki kunitoa.
 
Wasamehe bure ni katika harakati za kiushindani na kutafuta wateja na Ku draw attention yao.
 
Yaani niko live nachek mechi alafu wananitumia sms eti wananipa matokeo ya mechi ninayoitazama.. hii kama sio bangi nini
 
Naunga mkono hoja,jina la kesi litakuwa nini mkuu..?wanasumbua vbaya,mara meseji mara simu. Kila dakika kila saa....


As if tumenunua simu zetu kwa ajili ya matangazo yao na siyo kwa matumizi yetu binafsi, hawajui kama wanatupa kazi ya kufuta meseji zao na muda mwingine kutumalizia charge huku wakijua hawachangii gharama yoyote kwenye matumizi yetu.

Matangazo yao waweke barabarani na kwenye vyombo vya habari na siyo kutufuata majumbani mwetu kutuletea usumbufu usio na tija
 
Eti "BURE! Wewe ni mteja wetu wa thamani na umechaguliwa kupokea habari za papo kwa papo kutoka Mwananchi. Kujiondoa piga *149*37#.
Upuuzi mtupu, eti jitoe, kwani niliomba kujiunga? TCRA saidieni wananchi tunaporwa mno!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom