Airtel kwenye baadhi ya maeneo inazingua

Mar 26, 2018
72
59
Mimi ni mtumiaji wa Airtel, nikiwa Dar inaperfom vizuri sana hasa maeneo ya Kimara ninapoishi.

Ila toka nimeanza project za kwenda mikoani nimegundua Airtel ni poor sana, nikiwa maeneo ya Moshi, Arusha, Manyara na Dodoma Airtel wanazingua sana.

Siku moja nimeingia Dodoma na hela Yangu iko Airtel Money, nilipata shida ya kukaa nje kwenye baridi hadi saa 6 Usiku, ndipo nikaweza kutoa ela ya kulipia guest na kula.

Ninavyoandika hapa nna wiki ya 3,toka nimefika Dodoma, Airtell wanachofanya kwenye data ni aibu, kwenye call ndo shida kabisa,drop calls ni nyingi mpaka keep yaani ukiwa unapiga kabla ya simu kutoka ishakata. Sasa Swali ni je Airtell wamechoka kufanya biashara?je ni chombo kinahusika na kuwachukulia hatua ili kiwawajibishe hawa jamaa.
 
Hii kadhia imeanza juzijuzi ni kwl mkuu hata Mimi line yangu imeanza kusumbua sana!..
 
tena usiombee uwe na airtel katika mikoa umeme unakatika kila mara.
nadhani wanategemea transfoma za tanesco hawa..
umeme ukikata tuu na simu huku hazitoki
 
tena usiombee uwe na airtel katika mikoa umeme unakatika kila mara.
nadhani wanategemea transfoma za tanesco hawa..
umeme ukikata tuu na simu huku hazitoki
Wameshaikodisha minara yao yote.
 
Wameshaikodisha minara yao yote.
Wanataka kukimbia nchi ?maana naona hawafanyi jitihada zozote kuimarisha miundo mbinu yao.

Unakuta sehemu kama Dodoma wakati wanaweka miundo mbinu idadi ya watu ilikuwa ni 900,000 sa hivi watu wako 3,000,000,miuno mbinu ile ile inawaudumia.
 
Aisee afadhali Airtel mara Kumi kuliko Tigo hawa ni majanga ya taifa...
Hiyo mitandao yote nimeachana nayo toka 2017 na sasa natumia Halotel
 
Jana nilikuwa safari, nikafika sehemu nikaona ngoja nitoe kidogo niwe na balance kwa pochi, nilichokipata ni noma, msg haiji, kwa wakala haijaenda, ningekuwa sina mia mfukoni ningeimba hallelujah! Nikaomba namba za wakala na namba yake personal nikaondoka, natembe kama 1hr msg inaingia, nampigia wakala anirudishie muamala wangu, yule dada akawa mwaminifu kanirudishia mzigo wangu.

Hii mitandao unaweza kufa njaa kama huna hata mia mfukoni.
 
Mimi kwqnza na washangaa sana mnatumia airtel iyo kitu kwa mikoani aifai
 
Huduma za simu sasa hivi zinazingua, wanatafuna vocha kama vile wanabwiya caste lite. Mikoani hali ni mbaya zaidi, unapiga simu unaambiwa haipatikani wakati simu ipo hewani, unatuma meseji haifiki kwa mhusika mpaka watu wanagombana akihisi hutaki kujibu meseji yake.

Unatuma meseji asubuhi inafika kwa mhusika saa nane usiku, ukituma meseji ukiwa ubungo mpaka ukifika nyumbani kwa mhusika kolandoto ndo na meseji zinaanza kuingia.

Hivi hakuna wanaosimamia ubora wa huduma za simu au wameenda kibulugwa wanakula nyama choma. Mitandao yote ya simu ni kero, mnatukera wateja.

Simu upige ukiwa nje ukiingia ndani mawasiliano ni shida inabidi uzunguke ndani mpaka upate network, simu zinakoroma utazani spika ni mbovu.It is too worse.

Nakukumbuka remmy, "Machozi ya samaki huenda na maji".
 
Mimi ni mtumiaji wa Airtel, nikiwa Dar inaperfom vizuri sana hasa maeneo ya Kimara ninapoishi.

Ila toka nimeanza project za kwenda mikoani nimegundua Airtel ni poor sana, nikiwa maeneo ya Moshi, Arusha, Manyara na Dodoma Airtel wanazingua sana.

Siku moja nimeingia Dodoma na hela Yangu iko Airtel Money, nilipata shida ya kukaa nje kwenye baridi hadi saa 6 Usiku, ndipo nikaweza kutoa ela ya kulipia guest na kula.

Ninavyoandika hapa nna wiki ya 3,toka nimefika Dodoma, Airtell wanachofanya kwenye data ni aibu, kwenye call ndo shida kabisa,drop calls ni nyingi mpaka keep yaani ukiwa unapiga kabla ya simu kutoka ishakata. Sasa Swali ni je Airtell wamechoka kufanya biashara?je ni chombo kinahusika na kuwachukulia hatua ili kiwawajibishe hawa jamaa.
Nipo Mbezi kwa Msuguli mbele yako tu lakini sipatagi internet yao.
 
TCRA hawawezi iingilia ishu yoyote kama waandamizi wanaona hawatopata gap la kupiga hela! Wako kibiashara zaidi!
Mimi natumia voda kwa siku napokea sms zaidi ya 4 za Pesa n Mpesa na Twendeni mjini na sheria ilishakataza matangazo ya ofa ambazo tayari zipo kwenye Menu yao!
Kwakweli Tanzania tuna ombwe la mamlaka na Taasisi imara
 
Back
Top Bottom