nalikumbuka sana mkuu.
na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..
Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, Jaspert..(R.I.P)..
Nikiwa Arusha enzi hizo...nilipanda sana Msae maana wenyewe tulikuwa tunaita "chai Arusha, ugali Dar".....
Bila kusahau CHATCO huku unaangalia picha ya ANACONDA karibu kila bus lilikua lina hii movieShabaha, Ngorika, Amazon, Buffalo....
Hii Mwanza sasa na mikoa jirani ya Tabora na Shinyanga, Tanganyika yupo ila kwa style nyingine ila kuna gari inapiga Musoma - Mwanza kwa jina la Sandhu, na njia ya Mwanza - Dar enzi hizo kulikuwa na Mashiku Investment huku Dodoma to Dar kukiwa na Champion na Yarabi Salama kabla ya kupata ajali mbaya na kusababisha mfumo huu wa sasa wa mabasi kusafiri mchananani anakumbuka kipindi hicho salehe bus, midimu bus mwezi mpya, trans afrika, Tanganyika bus, na mengine mengi yalishakwisha.
Poleni mkuu...ila hivi ile ajali yao iliyomaliza zaidi ya watu 20 nadhani ilitokea mwaka 1999....
Maana nakumbuka baada ya ile ajali basi mimi ndio nikawa napanda sana haya mabasi nikiwa na imani hayawezi tena kupata ajali...
Mie nilikuwa mdau wa Dar express though nikikosa napanda Air Msae, pia kulikuwa kuna bus moja jamii ya haya Taqwq, Taafiq lenyewe lilikuwa linaitwa TAWHEED kama sikosei moja lilikuwa limeandikwa nyuma KOFFI ANNAN na lingine limeandikwa KITI MOTO yalikuwa yanatembea mpaka basi
Nakumbuka kabisa hili tukio ni la 1995 mwezi disemba!!
nalikumbuka sana mkuu.
na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..
Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, Jaspert..(R.I.P)..
:angry::angry::angry::angry:.......MMILIKI WAKE ALIPISHANA NA SERIKALI KUHUSU MALIPO YAKE YA KUSAFIRISHA "WAPIGA KURA" KWENDA ZANZIBAR KUPITIA BAGAMOYO MWAKA ULEEE WA 1995....MIMI NILIMSIKIA MWENYEWE AKISEMA....SASA HIVI ANA MA YUTONG YANAENDA MTWARA
Hili ni basi lililokuwa maarufu sana miaka ya 90, na lilikuwa likifanya safari zake kati ya Arusha na Dar es Salaam.
Sio kweli Msae kwa sasa inaitwa Metro Coach...office zao ni pale karibu na Shoprite kamata. Kilimanjaro ni kitu tofauti mazee. Acha upotoshaji