Air Hostesses, ni vema kutunza ngozi zenu

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
6,223
7,408
Mara kadhaa ukipanda Ndege za Shirika fulani (jina kapuni) unakuta Ma-Air Hostess ngozi zao ama zimekakamaa kama mamba au rangi zaidi ya moja kutokana na mkorogo.

Tujifunze angalau hata kwa wenzetu.

14939268117c73923cbb5ff7c4a9d4878054708124.jpg
 
Unapanda ndege au unawapanda wao? Acheni Ulevi, hasa ulevi wa madaraka na fedha. Mnabagua watu kwa rangi zao, vimo vyaona sura zao. Waafriaka ni viumbe waajabu sana.

Nimeona Mbunge kabisa aliyechaguliwa kabisa na kuingia Bungeni anajisifu kwa sura na kuwaponda watoto wa Kiafrika waliosoma na kupata kazi kwa weledi mkubwa.

Wajengeeni ujasiri Waafrika badala ya woga. Imefikia mahali hata teizi zinaangalia Sura ! Kweli ndiko tunakohitaji kwenda?

Hivi wachina wanauzuri gani ukilinganisha na Dada zetu hata wa kigogogogo?
Lakini wanajiamini .

Yule mbunge angekua ni wachama Kingine hoja ya Musukuma ingeungwa mkono mana kauli yake italeta ubaguzi na unyanyapaa.

Sio muda mrefu hata Walemavu watakosa ajira maofisini kutokana na mwonekano wao usio na mvuto.

Kwenye kila idara Kila mtu angependa kuhudumiwa na mdada au mkaka mwenye sura nzuri sana sana kama malaika na sio tu huko kwenye ndege yenu lakini tunachoangalia ni weledi na elimu ya mtu sio sura yake.

Sura waende huko kwenye Facebook na mashindano ya mamisi.
 
Mbona hao ulioupload wana ngozi mbaya? Vipi mfano wako umetisha.
 
Mkuu, 1000 digits; umeandika kama mgombea wa wadhifa fulani hivi. Huwezi nunua ndege kwa mabilioni halafu zihudumiwe na "cheap class of tending standards". Eti ubaguzi???

Yaani ndani kuna vinono vingi, mgeni umtengee viporo: hivi akirudi kwao ata kutangazaje? Wala siyo kwamba mnawatetea hao wahudumu wasiyokidhi vigezo bali ni mpango maalum wa kulihujumu shirika letu la ndege kisaikolojia, wenye akili wanajua.

Siwezi pata huduma mbovu kwako leo, ukatarajia nirudi tena kesho au nika ku-'recommend' kwa mwingine. Biashara inakufa hivyo. Tuachane na hoja za kufurahisha genge katika masuala mazito ya kibiashara na uchumi.
 
1000 digits,

Unaumwa kweli MUNGU kaumba wenye sura mabalimbali wazuri kwa wabaya angalia hata bar yenye watoto wazuri hupendwa.

Ati ubaguzi kuna sura nzuri zenye mvuto si kila mmoja ni Askari polisi sura za kipolisi haziwezi kuwa sura za wahudumu wa ndege, ATC inawabidi kutafuta wanawake wanao pendeza. Hata biblia inatenga kulikuwa na malikia Esta mfalme Ahusuero akampenda alikuwa mzuri kuwazidi wanawake wengine wa enzi hizo.

Mnawasikiliza wabunge wavuta bangi walioingia bungeni kuharibu na kupitisha miswaada ya maccm, hao hawajijui wanatetea matumbo yao. ATC itakufa kama huduma hazifai
 
1000 digits,
Kama tunafanya biashara hisia na kuridhishana tuwekee pembeni kila professional ina vigezo vyake... Ila kama tupo tupo tu kila mtu ni air hostess
 
Hahahaha Ila Ni kweli Sasa air hostess ana tofauti gani na beki tatu maana wote Wana tenga chai na maandazi

Au ana tofauti gani na kondakta au utingo

Au kwakuwa wao chombo chao kina paa angani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulishawaona wale Wa Emirates? Unamfanisha na huyo anayekutengea chai hapo Halmashauri ya Nanyamba?
 
Kwa mfanya biashara yeyote mwenye malengo na biashara yake lazima abuni mbinu za kuifanya biashara ipate watu wengi na kuikuza.

Hao wahudumu wa baa kuwa na mvuto mtasema pia wanabagua watu kumbe ndo mbinu alotumia mwenye biashara kuvuta wateja kwa kuweka warembo wanaovutia kweli kweli.

The same kwa ATCL ili kuvuta watu hao air hostess kuwa na mvuto ni mbinu ya muhimu mno
 
Back
Top Bottom