Aina za wachumba

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
1. VIPWENTE- hawa ni aina ya wapenzi ambao yeye anaweza akakumisi hadi anahisi network zinakata lakini hakutafuti ng'ooo iwe kwa meseji au laivulaivu kwa sababu hataki kuonekana yeye ndo wa kwanza kukutafuta. Ukimpigia simu tu au kumtext aje hakatai.

2.VIMBUNDU- hawa ni aina ya mapenzi ambao hakuonyeshi hata kiduchu kama yuko deep kwako..lakin ole wako akuone unaongea na kidemu/ kiblazamen kingine kazi mbona unayo...hawa huwaga wanapenda ndani kwa ndani kama meli za kivita. Hawa asilimia kubwa wanatoka mikoa ya iringa na njombe. Akijua una-dem au bwana kama hatamroga atajiua yeye.

3.VISHOKOMZOBE- hawa ni aina ya wapenzi ambao tangu umeanza kuvunja ILE AMRI hajawahi kukupa hata kijizawadi hata cha asante tu kwa kuridhishana, hawa wanajua kupokea tu hawajafundishwa kutoa.

4.VINJUNJIO- hawa ni aina ya wapenzi ambao yeye huonyesha tabasamu pale anapokuwa na haja na wewe ila mkishamalizana haja ikiisha hana tyme tena na wewe, kwa asili hawa hawana uwezo wa kutulia na mchumba mmoja. Akiwa na wewe atakuwa na akiba hata tatu..!

5.ATONDILE- hawa ni aina ya wapenzi ambao wanakuwa na michepuko zaidi ya 6 ila ole asikie kuna mtu anakunyemelea wewe hiyo vita yake bora world war hawa nao wanapenda ndani kwa ndani.

6.VISHUMUNDU- hawa ni aina ya wapenzi ambao we uwe na michepuko, umpige, umfungie nje, umtukane, ukatae kumtambulisha hakuachi ng'ooo ndo kwanza anazidisha malavidavi...ukikutana na aina hii oa/ olewa fasta au mpka mungu ashuke akwambie huyo ndo nimekuletea.

7.MANDONYA- hawa ni aina ya wapenzi ambao yeye kukuvalisha pete sio kazi utakaa na lichuma lake hata 3 yrz na hawaoni shida kukupeleka shopping mlimani city lakini kukuoa mpaka Yesu arudi au utasikia kamuoa angel wa Bagamoyo.

8.VIBINUZI- hawa ni aina ya wapenzi ambao yeye ukiwa nae muda wote anachati ukiuliza anachati na nani kinawaka, simu zao ni usiguse utakuwa unatafuta vita.

9.VIBUMBUSWA-hawa ni aina ya wapenzi ambao haipiti siku bila kugombana yani hata mkienda kulala ukaweka pozi la kulala kiubavu ubavu utasikia me hata sipendi ukilala hivyo huwa naota ndoto mbaya ili mradi tu mgombane.

10.VITUSU AMAIZING-hawa ni aina ya wapenzi ambao mapenzi yao yamepitiliza ni zaidi ya mapenzi kiasi kwamba hata ukipumua tu utasikia pole baby
hujaumia kweli?
hahahahaaaa.....

Vipi mwenzangu Mapenzi yako ya aina gani hapo?
 
Shule si mmeshafungua huku JF mnaingiaje?
Acha bangi,unataka kila mtu aandike kukuridhisha ww?? Me nna umri sawa na baba yako. Jenga tabia ya kuheshimu watu wote bila kujali tofauti zao. Hili ni jukwaa huru,kila mtu anapost kile alichonacho na si lazima uchangie. Ukiona pumba we pita pembeni!
 
Mdogo mdogo
 
Shule si mmeshafungua huku JF mnaingiaje?
1452744453676.jpg
 
Mdogo mdogo
Poa mkuu,nilikuwa najaribu kumpa ukweli huyu dogo. Hapa jukwaani huwezi kuridhishwa na thread zote. Na member hawawezi kuandika mambo serious muda wote,km jukwaa lingekuwa hivyo sidhani km lingevutia wengi. Kinachovutia jukwaa ni kwa sababu kila kitu kinaandikwa. Na km kilichoandikwa kipo nje na utaratibu mods huwa wanaondoa. Tukubaliane kwamba tumeumbwa na tofauti za mitizamo,mawazo,maamuzi,sura nk. Lazima tuvumiliane.
 
Tunaishi na watu wa kaliba tofauti ila wengine wetu huwa ni watu wa kushangaza mno kwakuwa hapa zaidi ya kuelimishana lakini pia tunaburudishana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom