Si mtu mwenye kitambi, ila sina fikra potofu na unyanyasaji juu ya wale wenzetu wenye vitambi (kwa lugha za vijana "watu wenye mgeni"). Bali ni mchambuzi tu wa kina kwenye maswala ya kijamii.
Katika maisha yangu, sijawahi kusikia kuna mtu ambae ameamka saa 11 asubuhi, na kuweka nia ya kufanya juhudi kuongezeka kitambi, au kusema "nataka niongezeke kilo 100 safari hii" na kuonesha msisiitizo wa kuanza papo hapo kutekeleza hio nia.
Watu huanza kuwa wabaguzi pindi mtu anapopata kitambi au kunenepa, huanza kusema "ushakua bonge, wewe hivi, wewe vile". Ushauri, nani anajali? Ridhika na jinsi ulivyo tu. Tena kama vipi kiambie hicho kitambi "Naona umeanza kuchomoza mgeni, karibu sana, itabidi tu nikupende na nitakutunza kwa juhudi zoteee!"
Wengine hukimbilia kufanya "dayati", ila nimegundua dayati ni kwa ajili tu ya wale wanene waliouchoka unene wao. Kwani hakuna kitu kinacholeta mawazo potofu kama masaa ya kwanza ya kufanya dayati, siku ya pili hua afadhali ya jana.
Wengine hukimbilia kufanya mazoezi ya kukimbia masafa marefu, tatizo la mazoezi haya pale unapotambua kua mwili wako hauna shepu ya kukuunga mkono (yani kukusapoti) kuendelea kukimbia ujue ushafika umbali mrefu ambako kurudi tena ulipotoka hata kwa kutembea ni kasheshe, utaishia kupanda bajaji muda wa kurudi!
Kama hujachoka kitambi chako, mikono juu
NA HIZI NDIO AINA ZA VITAMBI
1) KITAMBI MCHUCHUMIO
Hiki kimekaa kama herufi "D". Eti kinatokana sana sana na kula michemsho na bia za ofa.
View attachment 866048
2) KITAMBI MTEPETO
Eti ni kitambi cha wastani hivi, kinakua kama tairi yenye pancha, ambacho mtu akivaa nguo panapana hakionekani. Hichi hakina madhara kwa mmiliki, kipo katika vile vitambi "least harmful" kabisa.
View attachment 1803461
3) KITAMBI MVURUGO
Hiki kitambi kimekaa kama herufi "0". Kinapatikana sana kwa kula kitimoto kushushia na bia.
View attachment 866050
4) KITAMBI MTUNGUO
Hichi wanacho sana wadada. Kina umbo kama yai vile. Kwa "dayati" hakitoki labda kwa maombi maalum ya kufunga.
View attachment 1803464
5) KITAMBI MBONYEO
Kitovu hakionekani. Eti kina sababishwa sana kwa kula "rushwa" ila akisimamishwa tu kazi, kinaisha chenyewe.
View attachment 1803448
Changia ya moyoni, kama huna cha kuchangia gonga "LIKE" kuwapa sapoti wenye ugeni!!!