Aina za uhalifu mtandao - types of cybercrimes | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina za uhalifu mtandao - types of cybercrimes

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 4, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  YONA F MARO
  NAIROBI , Kenya – August 2010
  AINA ZA UHALIFU MTANDAO
  The ICT Pub

  Utumiaji wa Komputa zilizounganishwa kwenye mtandao unaendelea kukua kila siku sehemu nyingi duniani kasi hii ya maendeleo pia umeleta ukuaji wa kasi wa Uhalifu Mtandao katika maeneo mengi duniani .

  UHALIFU MTANDAO NI NINI
  Uhalifu mtandao ni uhalifu wowote unaofanyika kwa kuhusisha Kompyuta na Mtandao Pia watu kadhaa wamewahi au kujaribu kufanya uhalifu wa kawaida kwa njia ya mtandao mfano mtu anapoibiwa taarifa zake binafsi na kwenda kutumika sehemu nyingine na Udhalilishaji wa aina mbalimbali kwa njia ya mtandao .

  Kuna tofauti kidogo pale Komputa inapotumika kama sehemu ya Uhalifu ambayo haijaunganishwa na Mtandao lakini kitu kilichotengenezwa kinaweza kwenda kutumika kwenye mtandao au kisitumike kabisa .

  Mfano tumewahi kusikia Watu Wakisambaza Virus Zilizopo kwenye CD Na vifaa vingine vya Kuhifadhia vitu au wakitengeneza Vyeti Bandia , Risiti na aina nyingine ya Mali wanapotengeneza hivi vitu sio lazima Komputa iwe imeunganishwa na mtandao
  Uhalifu Kwa Mtandao unaweza kufanyika Sehemu yoyote na wakati wowote kama Kuna mtandao au Komputa wahalifu hutumia njia na hila mbalimbali kuhakikisha uhalifu wao unakamilika .

  UNACHOTAKIWA KUJUA
  Uhalifu wa Mtandao umezidi Usambazaji au Uuzaji wa Madawa ya Kulevya kwa Mapato ingawa Mtandao unaweza kutumika katika kufanikisha Biashara hii .
  Kila sekunde 3 Taarifa binafsi za mtu huibiwa duniani inaweza kuwa ni wewe au ndugu yako au jamaa yako mwingine uibaji wa Taarifa hii ni kuanzia Kwenye sehemu watu waposajili Taarifa zao binafsi kwenye Tovuti , Mitandao ya Simu na Majukwaa Mbalimbali .

  Bila usalama kama Antivirus , Firewall komputa yako inaweza kuingiwa na Virus au na Mhalifu wa Mtandao toka sehemu nyingine ya Dunia ndani ya Dakika 5 .

  TABIA ZA UHALIFU MTANDAO
  1 – Kuvamia komputa za wengine kwa njia ya Mtandao kwa nia ya Kusambaza Virusi au uhalifu mwingine kwa kundi au jumuiya ya watu Fulani .

  2 – Kutumia Komputa kama Silaha ya Kufanya au kuendeleza uhalifu uliozoeleka kama Kuuza Madawa ya Kulevya au Kuuza Bidhaa bandia .

  3 – Kutumia Komputa kama kifaa cha Kuhifadhia Taarifa Bandia mfano password , picha za watu , Nyaraka .

  Kwa siku za karibuni kumekuwa na Taarifa nyingi za uhalifu unaofanywa kwa njia ya Mtandao na Kompyuta kuna ambao wanafanya uhalifu huu bila ya wenyewe kujijua kama wanafanya uhalifu na wengine wanafanya kwa kujua kabisa wanachokifanya .

  Wahanga wakubwa kwenye Shuguli za kihalifu kwa Njia ya Mtandao wamekuwa vijana haswa ambao hawana kazi kwa kutumia kurahisisha kazi za wengine na watoto wadogo .

  Watoto wengi wamekuwa wakiwasiliana na watu wasiowajua kwa njia ya mtandao na kupewa Programu au kufundishwa kutumia baadhi ya vitu kwenye komputa zao ili waweze kutoa taarifa Fulani kwa wahalifu hao ndio maana huko nyuma niliwahi kuwaambia wazazi wafuatilie kujua watoto wao wanafanya nini kwenye mitandao na aina ya marafiki wanaowasiliana nao watoto wengi hawajui kama wanachofanya ni uhalifu .

  NJIA ZA UHALIFU MTANDAO
  Mara nyingi uhalifu mtandao unahusisha watu wengi au vikundi vya watu kadhaa sehemu mbalimbali duniani au sehemu moja ambao kwa siri hutumia njia Kadhaa kukamilisha uhalifu wako , mhalifu wa mtandao sio lazima awe kasomea au mjuzi sana kwenye kitu Fulani anachofanya lakini wengi hupenda kupeana maarifa kwa njia ya Mtandao .

  DROPPERS/CARDERS – Hawa ni watu ambao hupokea vitu vilivyonunuliwa na CreditCard Zilizoibiwa Kwa njia ya Mtandao katika sehemu ambazo hazifikiki kwa Urahisi .

  CASHIER – Hawa wanakazi ya Kutoa Hela kwenye Account za CreditCard zilizoibwa sehemu mbalimbali duniani .

  SPAMMERS – Ni zile Barua pepe tunazoziona kila mara za kutuomba Taarifa Fulani kuhusu sisi kwa matishio kwamba Email zetu zitafungwa barua hizi huenda kwa mamilioni ya watu .

  WEBDESIGNERS/TOVUTI – Hawa ni wale wanaotengeneza Tovuti kwa ajili ya Kuuza bidhaa Fulani kwa njia ya Mtandao zinazofanana na zingine lakini hizi zinakuwa za kihalifu na sio halisi unaweza kuweka taarifa zako zikaenda kutumika kwenye shuguli zingine hapo juu .

  EXPLOITERS – Hawa huitwa Script Kids kazi yao ni kutafuta Sehemu wanazoweza kuhifadhi tovuti au komputa za wengine ambazo hazina usalama kwa ajili ya kuanzishia uhalifu wao hapo haswa kwenye Database .

  AINA ZA UHALIFU MTANDAO
  Reshippings
  Inahusiana na Mhalifu sehemu moja ya dunia kupokea mzigo au bidhaa Fulani iliyonunuliwa kwa njia ya mtandao na kuituma kwenda sehemu nyingine mara nyingi creditcard za wizi ndio hununua bidhaa hizi lakini mhalifu anaweza kuwa anajua anachofanya au hajui anachofanya kama ni uhalifu wengi wao huwa wanakutana na wahalifu wenzao kama marafiki kwenye forums .

  Cyber Bullying
  Hii inahusiana zaidi na uonevu unaofanywa na baadhi ya Watu kwa jamii zingine za watu hii mara nyingi unahusisha picha au wale watu wanaojuana kwa njia moja au nyingine na mara nyingi unahusisha mitandao jamii kama Facebook , Nchi kadhaa ulaya kwa sasa zinasheria za kuadhibu watu wanaofanya uhalifu huu .

  Bahati Nasibu/Lotteries
  Mara nyingi ni pale wahalifu wanapotuma barua pepe au kuweka matangazo kwenye tovuti kadhaa kuwaambia watu kwamba wameshinda Bahati nasibu ya mamilioni ya shilingi lakini anatakiwa kutoa kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kukomboa fedha alizoshinda kwenye bahati nasibu hiyo .

  Piracy
  Huu ni aina kubwa kuliko wote wa uhalifu wa Mtandao unahusisha kushusha ( Download ) Nakala za muziki , video au Programu za komputa hata leseni za Programu bila kununua na bila udhini ya mtengenezaji au msambazaji .

  Hii haihusiani na pale unapojaribu kudownload program huria ambazo tovuti husika au watengenezaji wameamua kuziweka huru kwa ajili ya kutumika na watu wengi duniani kote lakini bila kuvunja makubaliano ambayo huandikwa kwenye sehemu ya program hiyo .

  Spam
  Utumaji wa Barua pepe haswa nyingi za matangazo au bidhaa Fulani bila ridhaa ya watu hao wanaotumiwa na mara nyingi bidhaa hizo au matangano hayo huwa yanaunganishwa na tovuti ambazo zina bidhaa bandia au tovuti za kampuni ambazo hazipo nchi nyingi hazina sheria za kupambana na SPAM lakini zina sheria za mtandao kwa ujumla .

  Kuna watu ambao kazi yao ni kuuza Emails ambazo hupatikana kwenye Mijadala ya wazi kwenye mitandao na aina nyingine za mawasiliano kama forwards .

  Phishing/Spoofing
  Ni pale Email ya mtu inapotumika kutuma Emails kwa watu wengine kwenye Mawasiliano yake bila ya yeye mwenyewe kuwa na taarifa mara nyingi ni katika kuomba msaada wa fedha labda amekwama sehemu Fulani nje ya nchi au eneo la mbali na alipo yeye haswa nchi za ulaya au afrika ya magharibi .

  Mauzo na Uwekezaji /Ponzi
  Hii inahusisha wale wahalifu wanaotoa Offer haswa kwa njia ya Mtandao ili watu waweze kujiunga na vikundi au offer za kuwekeza kwenye sehemu kadhaa kwa njia ya mtandao kwa makubaliano ya kupata percent Fulani ya fedha baadaye watu wengi huingizwa mjini baadaye na kupoteza hela zao walizozitoa wakati wa mwanzo .

  Uingiliaji Wa Mawasiliano
  Nchini Tanzania na nchi nyingi Duniani zina sheria za kusajili Laini za simu na vifaa vingine vya mawasiliano lakini usajili huu unamweka mtaje wa simu sehemu ya wazi ambazo taarifa zake zinaweza kutembelewa na wengine kama wafanyakazi wa kampuni hizo au zingine za matangazo bila taarifa za Mtumiaji wa vifaa au simu hizo .

  Wengi hufanya hivi kwa visingizio vya usalama wa Taifa wa Ndani wa Mataifa kadhaa duniani .

  Internet Extortion
  Hii inatokea pale wahalifu wanapo teka nyara njia za mawasiliano au mawasiliano ya kampuni au sehemu za kuhifadhi mali zao kwa njia ya mtandao na kuomba kiasi cha pesa ili waweze kuachia huru taarifa walizochukuwa au njia za mawasiliano hayo
  Usafirishaji/Uhamishaji wa Fedha Haramu .

  Watu kadhaa duniani wako kwenye mtandao wa kuhamisha fedha toka sehemu moja kwenda nyingine kwa njia ya mtandao fedha hizo zinaweza kuwa zimeibiwa haswa kwenye creditcard za watu , au wale watu wanaotembelea tovuti bandia na kuacha taarifa zao bila kujua au kutegeshewa program kwenye internet cafes , viwanja vya nende na sehemu nyingine nyingi .


  Uhalifu Mtandao umeleta hasara kubwa kwa mamilioni ya watu , serikali na mashirika kadhaa duniani haswa nchi za dunia ya kwanza ambapo watu wengi hutoa taarifa kwa vyombo vyao vya usalama hata hivyo mataifa kadhaa yamepiga hatua katika kuandaa sheria na taratibu zingine nzuri za kuweza kuadhibu wakosaji wote wanaohusishwa na aina hizi za uhalifu .

  Hili liwe funzo kubwa kwa nchi zinazoendelea haswa Tanzania inayotarajia kupiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya Teknologia huko mbeleni bila sheria nzuri zinazoweza kuongoza wananchi wake , bila kuimarisha vyombo vya usalama pamoja na watendaji wake Tatizo hili linaweza kuwa kubwa zaidi huko mbeleni na kuelemea Vyombo hivi.

  Kama inaonekana shida kuwa na sheria moja kuu basi kuwe na SHeria ndogo kwenye kila idara ya mawasiliano mfano Kampuni za Simu kuwa na Sheria Fulani kuhusu huduma Fulani wanazotoa kwa wateja wao kama ni mawasiliano ya Simu Internet nazo kampuni zinazotoa huduma za Internet Pekee nazo ziwe na sheria zao nzuri .

  Hizi ni sheria Za mawasilano ya SIMU na Mtandao , Sheria za Kuhifadhi Taarifa za wateja kama mawasiliano ya Simu na Internet .
  Kwa Taarifa zaidi tembelea
  CyberCrime & Doing Time
  Australian Institute of Criminology - Home
  Crime in the Digital Age by Peter Grabosky and Russell Smith, Sydney: Federation Press, 1998
  cybercrime.gov
  Welcome to CERT
  InfraGard - Public Private Partnership -Federal Bureau of Investigation (FBI)
  Webopedia: Online Computer Dictionary for Computer and Internet Terms and Definitions
  Cyber crime 'more profitable than drugs'
  https://www.javelinstrategy.com/news/831/92/Javelin-Study-Finds-Identity-Fraud-Reached-New-High-in-2009-but-Consumers-are-Fighting-Back/d,pressRoomDetail
  What Is Cybercrime?
   
Loading...