hydroxo
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 3,247
- 6,769
Mapacha ni viumbe(watoto) wanaozaliwa kwa pamoja, mmoja baada ya mwingine na mama mmoja.
Kuna aina mbalimbali za mapacha, lakini zilizo za msingi ni mbili,ambazo ni;
1.Mapacha wanaofanana(monozygotic twins).
-Mapacha wanaofanana hupatikana kwa yai moja la mama(ovum) kurutubishwa na shahawa moja ya baba(one sperm cell) na kuunda zaigoti,lakini katika kipindi cha ukuaji wa zaigoti ujigawanya mara mbili na kutengeneza viinitete(embryo) viwili vinavyokua watoto wawili.
mapacha wanaofanana mara zote huwa wa jinsia sawa na hufanana genetically.
2.Mapacha wasiofanana(fraternal or dizygotic twins).
-Mapacha wasiofanana hupatikana kwa mayai mawili ya mama(two ova) kurutubishwa na shahawa mbili tofauti za baba,kunakopelekea kuundwa kwa zaigoti mbili tofauti.
Zaigoti hizi mbili ukua tofauti na kuwa viinitete viwili tofauti ambavyo hatimaye uwa watoto wawili tofauti.
Mapacha wasiofanana wanaweza wakawa wa jinsia sawa au tofauti, pia wanaweza fanana na mtu mwingine ndani za familia.