Aina ya Wanawake wanaopendwa na wanaume Duniani!

Aina ya Wanawake wanaopendwa na wanaume Duniani!

kuchangumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
724
Reaction score
290
Wanawake wanaopendwa zaidi na wanaume na hata kuolewa mapema ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

Wanawake wanaochagua mtu kwenye mahusiano mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana.

Mwanamke anayeweza "kusema"Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine." Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu sana miaka hii.

Mwanamke ambaye ataridhika na wanaume ambao maisha yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke bora.
 
Asante mkuu.
Hapa tayari nimeshaanza kujiuliza, kwa macho au kwa mazungumzo uta tambua aje ainahiyo ya mwanamke?
 
Wanawake wanaopendwa zaidi na wanaume na hata kuolewa mapema ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
Wanawake wanaochagua mtu kwenye mahusiano mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo wanahitajika sana.mwanamke anayeweza "kusema"Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu sana miaka hii.
Mwanamke ambaye ataridhika na wanaume ambao maisha yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke bora.

Hakuna lolote....Wanawake mashankupe ndio wanaopendwa sasa we chunguza....Wale wenye msimamo utakuta wanaishilia tuu kuumizwa na kutendwa wanaonekana km walokole, washamba ......Ukisema enzi za baba zetu na mama zetu ndio walikuwa wanapenda wanawake wa hivyo ila sasa mmmmmhh... dhambi tupu ndio maana hawadumu
Chunguza dunia ya leo
 
hivi unasemaje niliye nae ananitosha wkati huyo mtu ni mzigo .... kiukweli am waiting for Mr right ambae ana hela ndio nitasema hivyo.....
 
Back
Top Bottom