Aina mpya ya wizi/wezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aina mpya ya wizi/wezi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KAKA A TAIFA, Jun 13, 2011.

 1. KAKA A TAIFA

  KAKA A TAIFA JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jamani kuweni macho na wezi hawa,akina dada/mama=wanawake kadhaa hapa jijini wamekwapuliwa handbags/pochi wanazoninginiza mabegani na wezi hawa.yaani wao wanatembea na bajaji ,pikipiki, tax,magari madogo ya abiria ,wanaendesha mwendo wa taratibu usawa wa mama /dada mtembea kwa miguu akiwa na pochi/handbag lake begani au mkononi.wakishamfikia tu wanalikwapua /wanakupua kwa nguvu na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.kwa kuwa mlengwa anakuwa kama ameshitukizwa na pia kushtuka kwa tukio, bado anakuwa haamini kilichotokea na hivyo huduwaa.huku mkupuaji akimwacha kwa mbali na waliokaribu kuanza kuelewa kilichotokea.akina mama /dada chukueni tahadhari na jaribuni kuripoti matukio haya polisi.pia ukiweza chukua/andika namba za chombo husika katika tukio.je wanajamii hili mnalionaje?
   
 2. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli ni hatari sana. Fikiria kina dada humo huweka vitu vyao muhimu kama lipstick, vitambulisho nk. Kwa kufanyahivyo ni kuathiri maisha ya watu. Kwa kweli njaa ni darasa katika dunia
   
 3. M

  Mkare JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio kwa kina dada/mama tu. Pia wababa/wakaka. Wakaka wamekwapuliwa sana laptops kwa style hii.
   
 4. g

  gracious86 JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 433
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mmmh! Hilo nalo neno. Shukrani sana kwa kutuinform!
   
Loading...