welding1682
JF-Expert Member
- Aug 20, 2019
- 2,229
- 4,838
Bora wako aise, wengine ukiona simu tu ujue kitachofata ni hela
Bro Kimbia, mwanamke wa namna hii kamwe huwezi kumridhisha.Habari, karibuni katika mada.
Kuna mdada niko naye katika mahusiano ya kimapenzi ila kwa sasa tuko sehemu tofauti katika harakati za kutafuta ridhiki. Kinachonikwaza ni kwamba ana tabia ambayo ni ngumu kuvumilika kwa kweli, kila siku ziendazo kwa Mungu ikifika usiku tu mfano ile saa 2 usiku imetimia, lazima akutext, call, whatsapp call video ili mradi vurugu na hakuachi mpaka ajiridhishe uko mwenyewe ndiyo atalala kwa amani.
Tofauti na hapo siku ukisema leo namute hizo sms, calls zitafika hata 400 na lawama juu.
Mwisho, kama unampenda sana dear wako kiasi cha kukaa mbali naye huwezi, mfate na siyo kusumbuana huu sasa ni utoto.
Watu wanachukulia poa sana hizi scenarios wanadhani ndio upendo kumbe ni utumwa. Kuishi unachungwa kiasi ambacho unaishi ili kutokukosea na kumuudhi na kibaya zaidi hawajui kua watu dizaini hii katika kila issue atatafuta sababu ya kuona unamcheat au humpendi.Nafikiri hujawahi kukutana na wa namna hiyo binafsi nilishindwa. Nilijiona nabanwa sana mpaka nashindwa kuwa huru hata muda mwengine ku enjoy na marafiki.
Unajua uzuri wa mambo ni kati kwa kati. Nilishindwa kuendelea naye.
Hujakutana na mwanamke mwenye Insecurities Issues mkuu. Hawaridhiki wale viumbe yeye muda wote anahisi unamcheat au humpendi.Kwa mahusiano kadhaa niliyopitia kwa hiyo kadhia mbona inavumilika tu.
Ila haivumilikia kama wewe huna hisia au humpendi kwa dhati huyo manzi.
Na inaboa zaidi kama humpendi coz kwako inakua usumbufu tu.
Kama unampenda wala sio kero, na watu wa hivo ukipokea mara moja tu ukamuelekez anakuelewa na anakuamini. Ila hizo delay zako zinamfanya azidi kukosa imani na wewe, na hao ni wepesi kuliwa kwa attention atayopewa na bazazi yeyote atakayeonesha kumjali.
Nakazia ✍️✍️Huyo demu kakupenda usiuzime moto wake wa upendo kwako.
Wengine tukiona meseji au simu ujue ni kizinga
Mwanamke akikupenda anataka ajihakikishie yuko peke yake na anataka kukulinda usije ukazama kwenye penzi la mwingine ndio maana unaona kama anakusumbua kwa meseji, simu au video call
Mwanamke akikupenda anataka uwe karibu naye, anahitaji sana kampani ya mpenzi wake
Kibiolojia wanawake wameumbwa wakiwa na asili ya kupenda kusikilizwa, mpe muda wako msikilize hisia zake cheka naye tanianeni, mpe ushauri, penda sana kumuuliza maswali ya kirafiki ambayo yatamfanya aeleze hisia zake. Kwa mfano Vipi mpenzi leo siku imeendaje? Umefurahia nini siku ya leo?
Halafu mbona mrembo ni mstaarabu sana anakuacha ufanye shughuli zako zote ila saa mbili usiku anahitaji kampani yako. Ukizingua utamkumbuka
mmoja nilimuacha alikus na hizo ishu ila pia sababu kuu ilikua hata mi sikumuelewaHujakutana na mwanamke mwenye Insecurities Issues mkuu. Hawaridhiki wale viumbe yeye muda wote anahisi unamcheat au humpendi.
Kibaya zaidi hua wanaamini kua humpendi na kosa lako lolote unalofanya (mf. kutopokea simu au a missed call) wao huamini ni point kwao kuthibitisha humpendi.
Wanataka kukucontrol kiasi ambacho maisha yako yote yawe kuhusu wao. Wana wivu na rafiki, co-workers mpaka ndugu zako wa Karibu. Yaani wanataka kila kitu katika maisha yako iwe kuhusu wao.
Kupigiwa simu au kutumiwa msg mpaka mida ya kazi au baada ya saa kadhaa na baada ya saa kadhaa unatumiwa msg. Ikifika jioni unapigiwa simu au kutumiwa msg. Usiku napo hivyo hivyo!Watu wanachukulia poa sana hizi scenarios wanadhani ndio upendo kumbe ni utumwa. Kuishi unachungwa kiasi ambacho unaishi ili kutokukosea na kumuudhi na kibaya zaidi hawajui kua watu dizaini hii katika kila issue atatafuta sababu ya kuona unamcheat au humpendi.
Ngoja huyo dada aondoke ndo mtoa mada atajua amepoteza nini karne hii ya 21.Mie nikipata mtu wa hivi nitafutahi sana kwa sababu mda wake wa thamani anapenda kuwa na Mimi. Na kingine anaacha mambo yake ya maana Ili azumgumze na Mimi.
Aisee mpe number zangu basi huyo dada. .
Ni kero richa ya kuwa inaweza kuwa ishara ya upendoKupigiwa simu au kutumiwa msg mpaka mida ya kazi au baada ya saa kadhaa na baada ya saa kadhaa unatumiwa msg. Ikifika jioni unapigiwa simu au kutumiwa msg. Usiku napo hivyo hivyo!
Alfajiri unapigiwa simu ya kuamshwa. Mara utatumiwa msg uende kazini salama. Utatumiwa tena msg umeshafika? Usisahau kula n.k Ikifika jioni utatumiwa msg mara pole na kazi. Usiku mtachat.
Weekend atataka uwe naye. Muda wote uwe naye. Hata mkitoka ikifika jioni atakutumia msg na usiku kuchat! Nikamwambia mama: Mimi ni mmoja lakini naishi kwenye jumla ya mtu mmoja mmoja (jamii). Nathamini penzi lako lakini kuna muda nahitajika kwenye masuala ya familia yangu! Kuna muda nahitaji wa kuwa peke yangu nitafakari masuala mengineyo. Lakini mapenzi si kifungo; muda mwengine nahitaji kuchil na washikaji kuzungumza, kupeana michongo, kubadilishana mawazo na muda mwengine ku enjoy tu urafiki wetu. Sasa wewe kona zote unakaba mama?!
Vuta picha ndiyo maisha ya 24/7. Sasa hayo ni mapenzi au kifungo? Ndiyo yale mambo ya Rama D nina kikao cha family wivu usiwe mpenzi. Hapana kwa kweli!
Ngoja tuone itakavyokuwaKwa mahusiano kadhaa niliyopitia kwa hiyo kadhia mbona inavumilika tu.
Ila haivumilikia kama wewe huna hisia au humpendi kwa dhati huyo manzi.
Na inaboa zaidi kama humpendi coz kwako inakua usumbufu tu.
Kama unampenda wala sio kero, na watu wa hivo ukipokea mara moja tu ukamuelekez anakuelewa na anakuamini. Ila hizo delay zako zinamfanya azidi kukosa imani na wewe, na hao ni wepesi kuliwa kwa attention atayopewa na bazazi yeyote atakayeonesha kumjali.
Ingawaje kila siku hakuna anachohisi kibaya na haachi.Pole sana... Hakuamini...
Tunakoendea itakuwa hivyoWa hivyo ukimuoa atakuchagulia hadi marafiki ili mradi akubane
Wewe ungefanya?Yeye mwenyewe umemjulisha?
Ila mkuu kwa upande wangu sioni kama ni shida. Kutokana na maelezo yako ni anakujulia hali mara moja kwa siku.Na muda anaofanya hivyo ni muda usio wa kazi ambapo umekuwa umetulia. Mwanamke wa hivi na kama hakusumbui sana kwenye hela, wapo wachache sana karne hii. Ukimuacha ndo utaona.Ni kero richa ya kuwa inaweza kuwa ishara ya upendo
Watu dizaini hii wanaupendo wa kweli hilo sikatai ila sasa sio waelewaNi kero richa ya kuwa inaweza kuwa ishara ya upendo