Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Rais anayemaliza muda wake wa Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS), Wakili Msomi Fatma Karume ameangua kilio alipokuwa akifungua Mkutano wa Mawakili Wasomi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha(AICC).
Wakili Msomi Karume alikuwa akitoa ripoti ya majukumu na utekelezaji wa majukumu hayo kwa kipindi chake cha Urais wa TLS. Ripoti hiyo imesheheni mafanikio yake yakiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ndani ya TLS na kusimamia utawala wa sheria kwenye nchi hii.
Wakili Msomi Fatma Karume alimaliza hotuba yake kwa kuangua kilio akiwaambia Mawakili Wasomi kuwa wamempa heshima kubwa na nafasi adimu na adhimu kuwaongoza kama Rais wao kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Katika kuonyesha kuwa amewagusa wahusika,Mawakili Wasomi walisimama kwa heshima huku wakimshangilia Wakili Msomi Fatma Karume. Kimsingi,Wakili Msomi Fatma Karume aliwaaga na kuwashukuru wanachama wote wa TLS.
Uchaguzi wa uongozi mpya wa TLS utafanyika kesho hapa Arusha.