ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 3,554
- 3,750
Basi na kakiingereza kako ka ugoko hako ndio unadhani utaonekana 'msomi'! Duuuh.
Eti "personal inferiority 'belong' to you"!!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Msiuchukulie personal huu mjadala, ni maoni tu, yayoweza kuwasaidia kuongeza ufanisi kwenye kazi zenu kuheshimika zaidi na kuwasaidia wananchi.
Kuna matatizo mengi kesi za kubambikiziwa maskini, watu kukaa mahabusu muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa wengine hawana hatia kabisa, makosa madogo kama faini chini ya laki moja kutupwa jela miezi sita, ingewezekana kuwapa Community service.
Mrundikano wa watu magerezani, chakula, watu wenye mental problem kuendelea kuwa gerezani, wakimbizi mfano Waethiopia kuwekwa lupango kwa gharama kubwa sana ya kodi yako si bora wangepigwa faini,
Kesi za nyumba, Mashamba, viwanja, wakulima, wajane, yatima, makini wanavyodhulumiwa, gharama za kupambana na matajiri, Polisi, Usumbufu kwenye mahakama za mwanzo.
Haya mambo yangewapa credibility, relevance kubwa sana kama mngeyasimamia kwa nguvu zote kila siku, kupiga kelele kwa wananchi wengi. Sababu yanawagusa moja kwa moja.
Kwamba hata hapa JF mngeanzisha hata uzi kuwasaidia wananchi na basics abc za sheria, haki zao, kwenye criminal, property, cooperate laws etc.
Kwamba mnaweza kujitolea labda kuchukua kesi fulani moja kwa mwaka kwa wanyonge kuwasimamia bila pesa.
Ni ushauri tu kwa hii taasisi yenu. Msikwazike sana. Nothing personal.