AICC, Arusha: Wakili Fatma A. Karume aangua kilio akiwahutubia Mawakili Wasomi

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Rais anayemaliza muda wake wa Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS), Wakili Msomi Fatma Karume ameangua kilio alipokuwa akifungua Mkutano wa Mawakili Wasomi unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha(AICC).

Wakili Msomi Karume alikuwa akitoa ripoti ya majukumu na utekelezaji wa majukumu hayo kwa kipindi chake cha Urais wa TLS. Ripoti hiyo imesheheni mafanikio yake yakiwemo kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ndani ya TLS na kusimamia utawala wa sheria kwenye nchi hii.

Wakili Msomi Fatma Karume alimaliza hotuba yake kwa kuangua kilio akiwaambia Mawakili Wasomi kuwa wamempa heshima kubwa na nafasi adimu na adhimu kuwaongoza kama Rais wao kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Katika kuonyesha kuwa amewagusa wahusika,Mawakili Wasomi walisimama kwa heshima huku wakimshangilia Wakili Msomi Fatma Karume. Kimsingi,Wakili Msomi Fatma Karume aliwaaga na kuwashukuru wanachama wote wa TLS.

Uchaguzi wa uongozi mpya wa TLS utafanyika kesho hapa Arusha.
 
Tupe taarifa alipoomba kura achaguliwe aliahidi nini na muda wake umeisha ametekeleza nini?

Mambo ya kulialia sidhani kama ni issue kubwa sana kwa great thinkers kujadili.

ACHA KULIA WEKA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKO MAMII.

Queen Esther
Aliahidi hasa kusimamia utawala wa sheria hapa nchini na imejidhihiri kuwa amefanya makubwa katika nyanja hiyo.
 
Tupe taarifa alipoomba kura achaguliwe aliahidi nini na muda wake umeisha ametekeleza nini?

Mambo ya kulialia sidhani kama ni issue kubwa sana kwa great thinkers kujadili.

ACHA KULIA WEKA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA AHADI ZAKO MAMII.

Queen Esther

Hao waliomchagua wame simama kwa heshima alio waaga wasingempa heshima hiyo kama hakukidhi matarajio yao.
 
66 Reactions
Reply
Back
Top Bottom