Aibu: Polisi yatuhumiwa kudukua simu ya Wakili Mwabukusi na kumuwekea maudhui Instagram ili impe kesi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,788
218,416
Screenshot_2023-08-16-15-15-13-1.jpg

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mbeya, Wakili wa Mwabukusi, Mwakilima, amesema kwamba Maudhui yanayosambaa mtandaoni na kudaiwa kwamba ni ya Boniface Mwabukusi yamewekwa na Polisi wenyewe baada ya kudukua akaunti yake ya Instagram baada ya kumnyang'anya simu yake ya mkononi.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, ndio maana hakukuwa na taarifa hizo awali, zimeletwa ghafla baada ya udukuzi huo kufanikiwa.

Lengo la jambo hili ni kuudanganya umma ili ijulikane kweli kwamba Mwabukusi na wenzake ni Wahaini.

Ni aibu sana kwa Jeshi letu la Polisi, kugundulika kufanya njama hii ya kijinga, na ni kuidhalilisha nchi nzima kwa manufaa ya DP WORLD na wapambe wake.

Nakala imfikie wakala wa DP WORLD Ritz
 
Polisi wajiweke mbali na haya mambo madogomadogo,hatakama wanapewa oda,wawe wanahoji.Hii inawachafua sana,halafu mwisho wa siku,viongozi haohao wanaotoa oda,wanakuja wanaanza kuwafokea mbele ya kadamnasi.Wajirekebishe, ikiwezekana hata kuijuzulu,ukiona unachoamriwa ni cha kijinga.
Mshahara inasemekana ni mdogo,kikokotoo kinawaimiza,halafu na watu wengine wawatumie kwa maslahi yao kweli?
PT,amkeni.
 
Back
Top Bottom