Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,580
Wakuu,
Ni ukweli usiopingika kuwa Lolote litakalofungiwa Duniani pia litakuwa Limefungiwa Mbinguni, na Lolote litakalokataliwa Duniani litakuwa limekataliwa Mbinguni!
Ni hivi:
Leo kulikuwa na uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa Parokia ya Kijenge iliyopo kata ya Olorieni hapa Arusha, ambapo Meya(wa kichina) wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo alikuwa mwenyekiti hapo awali. Huwa kunakuwa na taratibu za kumpata mwenyekiti kila baada ya miaka mitatu. Sasa leo viongozi kutoka vigango vya parokia ya Kijenge waliamua kupiga kura ya mwenyekiti. Kulikuwa na majina mawili la Gaudence Lyimo na Nicas Lila. Wapiga kura walikuwa 58.
Kura zikapigwa, Meya wa Kichina Gaudence Lyimo ambaye wakati kura zinapigwa alitokomea alipata kura 0, Nicas Lila alipata Kura zote 58.
Pia kwa kuweka Kumbukumbu sawa, Jumapili ya tarehe 21 July kulikuwa na uchaguzi wa mwenyekiti wa kigango cha kijenge. Katika uchaguzi wa kigango huyu huyu Nicas Lila alimpiga chini Gaudence Lyimo aliyepata kura 1 Nicas Lila alishinda kwa kura 260.
Baada ya uchaguzi baadhi ya watu walikuwa wakizungumza kuwa Gaudence Lyimo mwaka wa 2010 mwezi kama huu wao walimchagua kuwa mwenyekiti wa kigango na parokia ya kijenge, sifa hiyo ikampa nguvu na umaarufu uliomfanya apate ushindi wa udiwani, matokeo yake anakwenda kukalia umeya ambao hakuupata kwa haki, na bado anaendelea kukalia kiti cha damu. Watu waliuawa Januari 5 2011 kwa ajili yake, madiwani wakafukuzwa kwa ajili yake, bomu la soweto likaua watu kwa ajili yake, sasa tumemkataa kanisani na kwenye jamii.
Kwa ujumla mengi yalisemwa .....
Huyu ndiyo Meya Gaudence Lyimo
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums