DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,143
Akizungumza leo Agosti 22,2025 kwa njia ya mtandao, Susan Lyimo Mwenyekiti Mteule wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), amesema, “Uchaguzi Mkuu wa 2025 kama utaendeshwa kwa Sheria na Kanuni zilizopo utakuwa umekosa mvuto wa Kitaifa na Kimataifa kutokana na madhira yanayofanywa kwa Vyama vya Upinzani hususan CHADEMA”
“BAZECHA tunawataka Watawala kusikiliza matakwa ya wengi kwa maana ya Watanzania na kuchukua hatua za haraka za kufanya mabadiliko ya Kikanuni na Kisheria ya Uchaguzi Mkuu ili taifa liingie kwenye Uchaguzi huru na wa Haki”