kwakuwa ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa matukio haya hayakufanywa kwa bahati mbaya bali ni mkakati unaoratibiwa, na bado objectives hazijafikiwa!..ninaamini kikao hiki hakitakuwa na tija kwa waandishi wala wanajamii. wataishia kunya chai na kupewa ahadi hewa huku serikali ikijipa umaarufu wa utii bila shurtijamani mnachangia uzi huu kama vile mnatoka usingizini,waacheni waya zungumze nadhani tunacho takiwa kujadili ni matokeo baada ya mazungumzo hayo
wewe unaishi dunia ipi? siku hizi chama kinachopanga na kuteka watu aliwemo kibanda kinajulikana. soma kunathread inajadilia hapa tangu juzi au nenda kwenye u tube utaikuta.Wadau,
naombeni muniwie radhi ila leo sina budi kuwadisi waandishi wa habari wa Tanzania. Nimesoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa eti Waandishi Wanakutana na Dola Kujadili Usalama
Unakwenda kujadili usalama wako na mtu huyohuyo anayeuhatarisha? Dola hiyo hiyo iwapigao mabomu, iwatekao na kuwamwagia tindikali, iwapigao risasi na kusema iliwadhania ni majambazi, dola hiyohiyo iwacharangayo mapanga, iwatoboayo macho! Dola hiyohiyo?
Tangu lini panya wakakaa kikao cha usalama na paka? Au vipi swala na simba wakakaa kikao kwa ajili ya kujadili usalama? Hilo lawezekana?
Waandishi wa Tanzania hawajaungana! Alimwagiwa tindikali Kubenea na mwenzake Ndimara Tegambwage kucharangwa mapanga, waandishi walikaa kimya na sikuona la maana walilofanya kulaani kuteswa kwao! Likafungiwa gazeti la Mwanahalisi, sijaona la maana walilofanya kuilaani serikali! Akauawa Mwangosi kwa bomu, sijaona la maana walilolifanya kuilaani serikali! Alipigwa Risasi Mhariri wa Business Times, hakuna la maana walilolifanya! Sasa eti Kibanda, Mwenyekiti wao, ametobolewa jicho na kung'olewa meno eti wanakaa na dola kujadili amani!!! Amani ipi?
Hawa ndio wasaliti wa Absalomu Kibanda! Ndio wasaliti wa Kubenea; Hawa ndio wasaliti wa Mwangosi; Hawa ndio wasaliti wa taaluma nzima ya uandishi wa habari.... Badala ya kuchukua hatua madhubuti, wanabaki tu kuandikaandika vimakala vya kuilaani serikali!! Makala! Pachimbeni pachimbike! Hivyo ndivyo amani yenu itakavyopatikana na wala si kukaa meza moja na dola ambayo ndo yawatendea vitendo viovu!! Nasema pachimbeni; pachimbeni pachimbike!!
Walishaambiwa wana uwezo kiduchu wa kufikiri na kuhoji, na sasa wanauthibitishia umma walivyo sasa kuna ubaya gani?nahisi hawajitambui...!!
Nakubaliana kabisa na maneno yako, na ndiyo maana katika tukio lililomkuta Kibanda, vyombo vya habari vilivyolilaani tukio hilo vinahesabika. Nitavitaja miongoni mwake, gazeti la Mtanzania, ambalo ni mwajiri wake, magazeti mengine ni kama vile, Nipashe, Mwananchi na Tanzania daima.Ndugu yangu, wana nguvu ya kufanya hivyo ila tatizo hawajaungana. Ndio maana watatundwa mmojammoja mpaka waishe. Mwishoni watabakia waandishi wa gazeti la Mzalendo, watangazaji wa Radio Uhuru, na wale vibaraka wengine kama akina Ephraim Kibonde.
Nakubaliana kabisa na maneno yako, na ndiyo maana katika tukio lililomkuta Kibanda, vyombo vya habari vilivyolilaani tukio hilo vinahesabika. Nitavitaja miongoni mwake, gazeti la Mtanzania, ambalo ni mwajiri wake, magazeti mengine ni kama vile, Nipashe, Mwananchi na Tanzania daima.
Yapo magazeti ambayo hata ukiangalia vichwa vyake vya habari na uzito walioipa coverage ya hiyo habari, unaweza kujiuliza, hivi na hawa nao wamo kwenye tasnia ya habari?! Nitayataja baadhi ya magazeti hayo kuwa ni, Uhuru, Daily news, Habari leo, Jambo leo na Majira.
Ukija kwa upande wa vituo vya radio, huwa mara nyingi najiuliza kwa mfano Clouds radio, ambayo yenyewe inajiita the people's station, wakati katika tafsiri halisi hiyo radio ilipaswa iitwe the magamba's station!! Kwa kuwa propagandainayopigwa sasa hivi radio hiyo inaizidi hata radio yenyewe ya CCM ya Uhuru!!
Kinachofanyika na watawala hivi sasa ni ile mbinu ya devide and rule, kwa kuwa wanajua miongoni ya waandishi wa habari lazima watakuwepo watu wa design ya Yuda Iskariote, ambao watapewa vipande vichache tu vya pesa, ambavyo vitawafanya hata kama watashuhdia mwandishi mwenzao ametobolewa jicho, wao mradi mkono umeingia kinywani hawatojali!!
Kwa hiyo tunalazimika kumwomba Mungu kwa bidii sana ili aturehemu na kadhia hii kubwa sana inayolikabili Taifa letu kwa hivi sasa.
Mkuu Lubua,
Unamaanisha waandishi wakiwemo Pasco na Rioba? ..........
wewe unaishi dunia ipi? siku hizi chama kinachopanga na kuteka watu aliwemo kibanda kinajulikana. soma kunathread inajadilia hapa tangu juzi au nenda kwenye u tube utaikuta.
jamani mnachangia uzi huu kama vile mnatoka usingizini,waacheni waya zungumze nadhani tunacho takiwa kujadili ni matokeo baada ya mazungumzo hayo
hebu basi nidokeze kidogo kuwa ni nani anayefuata baada ya huyu, nitaficha siri. ila nawasikitikia kuwa muda si mrefu mtakuja jua madhara ya haya myafanyayo, mungu yu pamoja na wafanyao mema,.
Rama Ighondu amekamatwa?
.
Walimdhihaki Kubenea wakambeza wala hawakumpa ushirikiano alipo simami na kuufia ukweli wa alichokiamini,leo wamejionea!!basi tusemeje?
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
hakuna waandishi wa habari makini hapa bongo,wanalalia kwa kibanda kwa sababu ndo mwenyekiti wao,yule aliyegongwa na gari moshi akifichua biashara za magendo mpakani mbona hata story moja hatukuziona?,wanafiki wakubwa hao,wasipoungana na kukemea kila kinachompata mwandishi yoyote bila kujali sura,watakwisha