Aibu kwa vyombo vya habari Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu kwa vyombo vya habari Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zipuwawa, Oct 18, 2012.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Wengi watadhani ninachokiandika hapa ni cha kijinga ila vyombo vya habari vya Tanzania vina tia Aibu. Kazi ya vyombo vya habari ni kupasha habari jamii hasa pale habari zozote muhimu au mbaya zinapotokea. Lakini imekuwa tofauti kwa vyombo vya habari Tanzania yapo kama sasa kuna matukio mengi zanzibar na Tanzania Bara lakini vyombo vinapiga miziki tu bila hata kujua umuhimu wao wao wanasubiri saa 2 usiku ndio watoe habari hizo huku hata habari nyingine kufichwa kabisa huu ni ujinga na aibu.
  Angalau ITV hujitahidi kutoa habari za saa lakini nao wamekuwa wakirudia hata za jana ina maana gani? TBC ndio ujinga kabisa sioni hata haja ya kuwa na chombo hichi kwa Taifa , Star TV kama kawaida......Sasa nani kasema vyombo vya habari ni kuwapasha watu habari saa mbili tu usiku na marudio sanne au saa tano.

  Kwanini Wananchi hawapati habari za kweli na za uhakika zikiwa za moto? Huu ni ujinga na ugonjwa kwa vyombo vya habari.
  Nasema Bora uwe humu jamii Forum utapata kila siku kuliko kusikiliza hizi radio na TV za kibabaishaji.

  Wanajamii mimi nakerwa na hili kutokana na matukio mengi kama ya uchomaji wa makanisa na mengine kupata kutoka kwenye mitandao kuliko hivi vyombo vya habari. Nawasilisha hoja yangu wana jamii
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama wanapiga muziki tu masaa 24
  inaweza kuwa 'hakuna hatari hiyo unayohisi'
  au labda wanaokuja Jf wana 'sensationalize' hizo habari wakiwa na interest zao pia
   
 3. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nafikiri upungufu/tofauti tuliyonayo hapa kwetu na mfano - nchi za ulaya ni kwamba;- vyombo vyao vya habari vimegawanyika in terms of categories - some are more of 'informative' na vingine ni entertainment zaidi na ndio maana you cannot tune in 'BET' and expect to get news from it rather ukitaka news utaenda 'CNN' BBC etc.

  Sasa usiwalaumu vyombo vyetu vya habari, wapo responsible kutuhabarisha, ndio wana mapungufu lakini pia am sure wanajitahidi kadri wawezavyo na ndio maana - katika hivi vyombo vya habari tulivyonavo - kuna ambao wanajitahidi sana kutoa report hata kama ikija saa mbili usiku lakini atleast wamei-report in detail enough kuliko wale ambao hawata report kabisa!

  Tukitaka kuwalaumu kwa sababu hawatoi news in real time tukumbuke basi kwamba na wao wana programs nyingine ambazo ni lazima zirushwe hewani kwasababu zinachangia katika ku-finance operations zao, so instead they will gather information na kuzileta kwetu muda unapofika. My thoughts!!!
   
 4. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Umetoa maelezo mazuri sana! Lakini hata TBC kweli vipindi vyao wanahitaji kurushwa ili wapate chochote?
   
 5. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa hilo la TBC mimi siwezi kujua kwa kweli wala kuongelea, nimetoa mfano generally..... am sure they must have their reasons!!!:peep:
   
 6. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mambo mengine yanakuzwa mkuu wala usipate shida na habari za JF! Kila mtu anatumia jina feki na yupo huru kuandika atakavyo watu wanaandika tu kutafuta attentions za watu waonekane na wao wamepost!
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Lakini nyingi huwa tunaamka nazo kwenye habari.....mi huwa naona habari nyingi huanzia JF
   
Loading...