Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Inaweza kuonekana kama si jambo kubwa sana, lakini likawa na maana kubwa sana. Tena linaweza lisionekane kumaanisha kitu lakini likawa na ujumbe mzito uliojificha.
Katikati ya rasimali watu zaidi ya mia mbili, na kuna wengine wamechukuliwa nje ya hao lakini bado wameshindwa kutimia 34 tu aliowakusudia Mh.RAIS! Hivi hilo ni jambo la kawaida kweli!? Labda angetumia wiki moja au mbili kuwatafuta huenda tungesema muda ulikuwa hautoshi. Lakini si hivyo, ametumia zaidi ya siku 32 kuwachuja toka miongoni mwa hao 200+ na nje ya hao lakini ameshindwa kuunda kikosi kazi chenye idadi aliyoikusudia achilia mbali sifa na umakini anaouhitaji kwani binadamu hatuwezi kuwa sawa!
Nionavyo mimi, ndani ya hao 200 na ushee wa CCM amewakosa wenye mawazo na maona ya kizalendo kwa nchi yao TANZANIA! Huenda, narudia tena huenda walio wengi wana uzalendo kwa wao binafsi, kwa chama, familia zao na kwa matapeli na mafisadi wakubwa wa nchi zaidi kuliko uzalendo walio nao kwa Taifa ndio maana RAIS anahangaika kuwamulika kwa tochi ndani na nje ya waliochaguliwa lakini bado hawatimii 34 aliowakusudia kuanza nao!
USHAURI WANGU: Mtakaporudi bungeni, jaribu kuwa wazalendo kwa nchi kuliko chama na watu. Jaribuni kuumizwa na shida za watanzania kuliko kung'ang'ania kupitisha mikataba itakayowanufaisha watu ambao wakiwa huko wana wacheka na kuwadharau! Jaribuni kuheshimu na kuthamini mawazo ya wanaokosoa serikali na kuelekeza nini cha kufanya kwani huo ndo wajibu wenu. HII NI AIBU KWA CHAMA TAWALA KUKOSEKANA KWA MAWAZIRI WENYE SIFA WA KUTOSHA!