Aibu jimboni kwa Waziri Mkuu (Ruangwa); Wapiga kura wake waishi kwa kula mbilimbi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,788
Hekari zaidi ya 545 za mahindi na mpunga zilizoko katika kijiji cha Nanjulu tarafa ya mandawa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi zimesombwa na maji kufuatia mafuriko yaliyo sababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo kaya 231 zinaishi katika maisha ya shida na kula matunda ya porini aina ya mbilimbi kama chakula cha kuwafanya waendelee kuishi.

Nihali isiyo ya kawaida kwa wahanga hao baada ya mtafiti wa kituo cha utafiti wa mazao jamii ya mizizi cha naliendele kutoa sampu ya shina la Mhogo kwa mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima nakuamua kuwapa akina mama moja na jingine akina baba wagawane matarajio yake yalikatishwa ghafla na kile kilicho daiwa kuwa ni njaa na kuanza kunyang’anyana Mhogo huo ambapo wameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la tatu kwani maisha yao yamekuwa wakiishi kwa kula matunda ya porini.

Wahanga hao wakiwemo viongozi wa taasisi ya utafiti na maendeleo naliendele wametembelea maeneo yalipo kuwa mashamba hao nakukuta mazao yamesombwa na maji ambapo mratibu mazao jamii ya mizizi kitaifa Daktari Geoffrey Mkamilo amesema imewalazimu kupeleka mbegu hizo zinazozaa kwa muda mfupi ili wahanga hao wapate kujikwamua kimaisha baada ya miezi miwili ijayo kuanzia sasa.

Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi.Mariamu Mtima akipokea mbegu hizo ameshukuru kituo cha mbegu cha naliendele kwa kutoa mbegu hizo ambazo zitawafanya wahanga hao kurudi katika hali ya kupata chakula kwa muda mfupi sambamba na kuwataka vijana waache kucheza pulu na bao badale yake walime iliwaondokane na umasikini.
 
Sichangii kwa undani sana juu ya hili lakini nikukosoe tu mleta mada Mbilimbi huwa azijiotei porini bali upandwa na zina uchachu na ndio maana utengenezewa kitu kinachoitwa achali ambacho huwa kama appetizer wakati wa kula chakula kwa hiyo labda wanakula vitu vingine lakini sio mbilimbi na pia suala hilo sio aibu kwa PM kwani hilo ni janga na limetokana na mafuriko hivyo sidhani kama PM alikuwa na uwezo wa kulizuia hilo.
 
Watu wengine shida sana.
Yaani we mwenyewe unasema ni mafuriko, halafu we mwenyewe unasema ni aibu !!!
 
Mbilimbi kwa viwavi haviliki bhana

Waharakishiwe chakula cha msaada

January utawahamisha na hawa kwa kukaa sehemu hatarishi?
 
Hivi kitengo cha maafa kiko chini ya Wizara gani?, kwa nini hawajapeleka misaada?.
 
Watu wengine shida sana.
Yaani we mwenyewe unasema ni mafuriko, halafu we mwenyewe unasema ni aibu !!!
Kwa hiyo mafuriko hayana namna ya kukabiliana nayo,watu waachwe wale udongo kisa ni mafuriko.Kitengo cha maafa kiliundwa cha nini sasa si wangeacha tu ikitokea mafuriko watu wawe wanakula mbilimbi?
 
Sichangii kwa undani sana juu ya hili lakini nikukosoe tu mleta mada Mbilimbi huwa azijiotei porini bali upandwa na zina uchachu na ndio maana utengenezewa kitu kinachoitwa achali ambacho huwa kama appetizer wakati wa kula chakula kwa hiyo labda wanakula vitu vingine lakini sio mbilimbi na pia suala hilo sio aibu kwa PM kwani hilo ni janga na limetokana na mafuriko hivyo sidhani kama PM alikuwa na uwezo wa kulizuia hilo.

Hata mimi nilishangaa kuona mleta mada anashangaa watu kula mbilimbi, ningeshangaa kama ningesikia wanakula udongo
 
Back
Top Bottom