AIBU: Hospital ya rufaa ya Morogoro haina huduma ya X-RAY

Jaji

Senior Member
Sep 4, 2011
129
13
Baada ya miaka hamsini ya uhuru ni aibu sana kwa hospitali ya mkoa ya morogoro ambayo imepandishwa kuwa hospitali ya rufaa kukosa huduma ya X-RAY.

Kuna siku nikiwa kwenye daladala nilisikia mtu akilalamika kwa kitendo hicho ila sikuamini. Jana ndiyo niliamini baada ya mmoja wa kijana aliyejeruhiwa jana kushindwa kuhudumiwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.....
 
Asante kwa taarifa, ntaenda kupata huduma hiyo INDIA. Tutafika???????.......
Chukia unyonyaji, Chukia CCM.
 
Pesa ya kununua risasi za moto,mabomu ya machozi na maji ya kuwasha huwa hazikosekani lakini za kuhudumia wananchi hamna!
 
Hivi mnafahamu kwamba fedha za wahisani ndio zinazoendesha wizara ya Afya??

Wahisani wasipotoa fedha leo kwenye wizara ya afya, serikali haitaweza hata kulipa Mishahara.

Habari ndio hiyo.
 
Halafu kuna mabwege humu kama Kingxiv yanasema maandamano hayana tija.
 
Wewe unashangaa Morogoro, sisi hapa Songea hospital ya mkoa ambayo ni rufaa sasa, haina X ray tangu miezi sita iliyopita, haina Ultrasound, kwa sasa wanafanya bs stool na rbg tu, imgeuzwa kuwa dispensary kubwa. Na haya si hapa tu bali ni hospital nyingi nchini. Mfano huku Songea tatizo halionekani coz ya hospital ya Peramiho ambapo huduma nyingi kwa mahitaji ya kitanzania zinapatikana.
 
Madaktari wakiishupalia serikali ifanye marekebisho mnawalimboka na kuside na serikali yenye siasa za majitaka kuhusu afya. Unadhani ni kiongozi gani ataenda pale kutibiwa akaacha kwenda Apolo akalishwe pilipili??
 
Madaktari walipotuambia kuwa huduma za afya ni mbaya bila shaka tullidhani inawahusu wao tu. Uliloliona Morogoro ni sehemu tu. hali ni mbaya nchi nzima. Ni bora wasiojua kinachoendelea maana hushangilia kila lisemwalo na wezi wa rasilimali zetu kwa jina la viogozi wa nchi.
 
Hamna pesa jamani, kwa nini hamuelewiii????? Serikali yenu bado inaimarisha jeshi la polisi ili tuuthibiti upinzani! Mikutano ya kila siku ya magwanda mnadhani hela tutabakiza baada ya kununua risasi na mabomu ya machozi? Jamani tuhurumieni, hawa CHADEMA wanatukimbiza mno hadi tunashindwa kuwafikiria wananchi.
 
So Ruvuma, Tanga, Morogoro etc kote mwendo RBG, na B/S for Mps??!..dah?! sijui zile za wilaya, Health Center, Dispensary ndio zikoje?!!
 
So Ruvuma, Tanga, Morogoro etc kote mwendo RBG, na B/S for Mps??!..dah?! sijui zile za wilaya, Health Center, Dispensary ndio zikoje?!!

Mkuu usiende mbali huko wilayani kutaka kujua kukoje, Hospitali za mikoa ni aibu tupu. Hospitali ya Mkoa Kilimanjaro haina major wala minor theatre tangu tarehe 27/12/2010 baada ya wizara kufunga jiko lililokuwa likitumika Kama major theatre kwani ilikuwa na Hali mbaya na minor theatre mbovu kuliko maelezo. Ujenzi Wa new major theatre is another silly session discussion.
 
Wewe unashangaa Morogoro, sisi hapa Songea hospital ya mkoa ambayo ni rufaa sasa, haina X ray tangu miezi sita iliyopita, haina Ultrasound, kwa sasa wanafanya bs stool na rbg tu, imgeuzwa kuwa dispensary kubwa. Na haya si hapa tu bali ni hospital nyingi nchini. Mfano huku Songea tatizo halionekani coz ya hospital ya Peramiho ambapo huduma nyingi kwa mahitaji ya kitanzania zinapatikana.

harafu akina Malaria sugu wanasema mission hosp zisipewe ruzuku!
 
Watanzania mtajiju. Mliambiwa bora maisha kwa kila mtanzania, mkadhani ni maisha bora kwa kila mtanzania. Kiswahili kitamu bana.
 
Pesa ya kununua risasi za moto,mabomu ya machozi na maji ya kuwasha huwa hazikosekani lakini za kuhudumia wananchi hamna!

Kiongozi mmoja alisema kuwa "...tuko tayari kwa vita dhidi ta Malawi..." Hii ilikuwa na maana kuwa pesa za kugharamia vita tayari zipo !!!
Lakini ukienda hospitali za serikali, hamna x-ray machine, hamna ct-scan machine, n.k. Hii ndio nchi yetu Tanzania!!
 
Baada ya miaka hamsini ya uhuru ni aibu sana kwa hospitali ya mkoa ya morogoro ambayo imepandishwa kuwa hospitali ya rufaa kukosa huduma ya X-RAY.

Kuna siku nikiwa kwenye daladala nilisikia mtu akilalamika kwa kitendo hicho ila sikuamini. Jana ndiyo niliamini baada ya mmoja wa kijana aliyejeruhiwa jana kushindwa kuhudumiwa kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.....

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro huwa inatoa huduma za X-Ray, ila nadhani kwa muda huu mashine zitakuwa zinaitirafu na hazifanyi kazi.
 
Back
Top Bottom