Aibiwa fedha zote kwenye akaunti kwa NBC MasterCard kupitia ATM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibiwa fedha zote kwenye akaunti kwa NBC MasterCard kupitia ATM

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mzalendo JR, Oct 5, 2012.

 1. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Wizi wa elektoniki unaonesha kushika kasi jijini baada ya watu wawili kuibiwa fedha zao kwa kutumia MasterCard.

  Mmoja wa waandishi waandamizi wa gazeti la HabariLEO, Bantulaki Bilango mwenye akaunti namba 017201056410 iliyofunguliwa katika tawi la NBC Moshi ameibiwa zote zilizokuwemo kwenye akaunti yake kupitia ATM ya tawi la Benki hiyo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza baada ya kutoa taarifa NBC Makao Makuu yaliyopo Mtaa wa Sokoine Drive mapema leo, Bilango alisema baada ya kutoa fedha katika akaunti yake kupitia ATM iliyopo tawi la benki hiyo la Viwandani barabara ya Nyerere jana, leo alikupokwenda ATM zilizopo katika tawi la Corperate, alikuta fedha hizo zimechukuliwa muda mfupi kabla yake.

  Taarifa ya benki aliyopewa ilionesha kuwa pesa hizo zilitolewa leo asubuhi katika ATM iliyopo Kinondoni.

  Scan sehemu ya statement uonyeshe jinsi gani mwizi huyo alivyoiba.

  "Jamani huu wizi ni wa aina yake. Mimi nimechuka Master Card yangu juzi tu leo hii kuna mtu amekomba pesa zangu zote kwenye ATM," alisema .

  Hata hivyo alipoomba waangalie kamera zao kwa kuwa kila anayeingia kwenye mashine za ATM humulikwa walidai kuwa hiyo ni hatua ya juu sana inayohusisha polisi, hivyo hawawezi kufanya hivyo kwa wakati ule.

  Hata hivyo, Bilango anasema alipata ushirikiano mzuri katika tawi la benki ya Viwandani katika barabara Nyerere alikochukulia fedha jana ambapo msimamizi wa Huduma kwa Wateja na Huduma za Biashara na Nje, Matilda Manumbu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa benki hiyi waliahidi kufuatilia kwa karibu ili kuweza kumpata mhusika.

  Kulingana na maelezo ya Bilango, kadi iliyokuwa ikitumika kuiba fedha ni ile ile ambayo alikuwa anayo mfukoni. Alisema la kushangaza, wakati yeye akiwa nayo, mtu mwingine alikuwa akiendelea kutoa fedha katika ATM.

  Mmoja wa wateja alisema wizi huo unaoweza kufanyika kwa kuwatumia wafanyakazi wa benki lakini wakati mwingine kuna carbon inaachwa kwenye mashine ya ATM ambapo mteja akiweka kadi, taarifa zake zinanaswa kwenye carbon hiyo na baada mwizi kutumia taarifa hizo kuiba fedha hizo katika ATM nyingine.

  Alishauri wateja kuacha kutumia njia hiyo na badala yake watumie dirisha kwa kuwa mashine hizo zinatumiwa vibaya.

  Wizi huo unaonekana kukithiri hasa katika tawi la Kinondoni ambapo mteja mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake alichukulia fedha zake katika tawi hilo la Viwandani, kisha kuibiwa fedha zake kupitia tawi la Kinondoni wiki iliyopita kwa kutumia kadi yake ya ATM .

  "Nami nimelizwa, lakini wamesema wanashughulikia, hivyo naamini fedha zangu zitarudishwa maana walichukua mshahara wangu wote.

  Tukio hilo lilimpata tena mkazi mwingine, Fabian Rugaimukamu mwenye akaunti namba 2012401429 katika benki ya NMB tawi la Bank House.


  Source: http://ziro99.blogspot.com/2012/10/mwandishi-akombwa-fedha-zote-atm-ya-nbc.html
   
 2. u

  usawa wa Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wizi huu sasa umeshamiri sana , mdogo wangukaibiwa hivo hivo CRDB ATM pesa nyingi sana, mwizi alikuwa anatoa kila siku ya mungu 1 M mpaka siku mdogo wangu alipokweenda kutoa pesa akakuta anaambiwa hawezi kutoa pesa kwani alishafikia limit ya siku kutoa pesa. Ndo kushituka iweje siku hioanataka pesa anaambiwa kashatoa, ndio haraka kukimbilia CRDB kuripoti na hapo wakamwambia asubiri siku 45 za uchunguzi....verry sad
   
 3. u

  usawa wa Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wizi huu sasa umeshamiri sana , mdogo wangukaibiwa hivo hivo CRDB ATM pesa nyingi sana, mwizi alikuwa anatoa kila siku ya mungu 1 M mpaka siku mdogo wangu alipokweenda kutoa pesa akakuta anaambiwa hawezi kutoa pesa kwani alishafikia limit ya siku kutoa pesa. Ndo kushituka iweje siku hioanataka pesa anaambiwa kashatoa, ndio haraka kukimbilia CRDB kuripoti na hapo wakamwambia asubiri siku 45 za uchunguzi....verry sad
   
 4. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Hii ni hatari sana. Hizo ndio hasara za teknolojia za kisasa. Inabidi watu wa benki wawe makini sana katika jambo hili, ili kuzuia wizi wa fedha za wateja hauendelei. Wateja tutaogopa kutumia kadi hizi ambazo zinaonekana kuwa tanzi sasa.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  NBC hawafai...shangazi yangu naye yamemkuta maswahibu hayo hayo. Sishangai yule boss kawekwa kando kupisha uchunguzi. Ethics za wafanyakazi wao pengine ziko very low na ndio hao wanaoiharibu sifa ya bank.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mimi nimeanza utaratibu wa kucheki salio langu kwa siku mara nne, hii inaweza kusaidia kidogo
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,853
  Trophy Points: 280
  Maxmam ya kutoa pesa nadhani haizidi milioni tatu so ukute kaibuwa hela ya kufungulia acc

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 8. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kamera itakusaidia sana ku truck mtu aliyetoa hizo hela! Mimi nadhani technolojia nzuri ingelikuwa ni ATM kudetect account holder kwa kutumia fingerprint kutolea hela, nadhani hiyo ingekuwa komesha kuliko Password number.
   
 9. s

  senioswald Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani haya ndo matatizo ya utandawazi, maana tunaletewa technology kabla ya kuandaliwa jinsi ya kuitumia, kutokana na hali hii ni bora kutochukua hizi master card maana jinsi unavyokuwa na uwezo wa ku access pesa yako zaidi ndo jinsi wizi unavyoongezeka maana unaweza kuibiwa pia kimtandao maana hadi ulaya wanaweza ku access pesa yako
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kama mtu hajaibiwa kadi mara nyingi anayeiba anakuwa ni miongoni mwa watu anaowafahamu. Njia nyuri ni kuacha account open na once kadi hiyo ikiingia kwenye ATM wanadelay searching na immediately wanafanya utaratibu wa kumuhoji anayetoa pesa.
  Iwapo mtu anayeiba anatumia kadi ambayo siyo ile aliyepewa mteja, basi hapo mteja hajaibiwa, iliyoibiwa ni bank. Mteja atatakiwa kulipwa na bank kiasi chake kilekile kilicho kwenye account. Eitherway, mteja anatakiwa kutokupoteza pesa kwa either kumtambua mwizi wake au kulipwa na bank.
  Kutumia fingerprint ni nzuri, lakini on the other side inalimit mteja. Mtu anaweza kuwa mgonjwa akamtuma mwanae akamchukulie pesa. Wakati mwingine mtu anaweza kusafiri akaiachia familia kadi ili mshahara ukiingia wanacheza nao. Ila ikiwa fungerprint hilo haliwezekani.
   
 11. s

  senioswald Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la wizi wa mtandaoni, unaweza kuhisi na kung'ang'ana na ATM mashine kumbe wizi uko electronically zaidi na sio kwamba kuna mtu kaenda kusimama kwenye machine, watu wa benk upade wa IT wanajua la kufanya na ndo wanaweza kutoa majibu sahihi
   
 12. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red! hayo mahojiano na majibu yake si ni secret information ambazo ni sawasawa na kama ilivyo password? Source ya matatizo ya password, inaanzaga hapo kwenye kumuachia mtu mwingine kadi (familia,rafiki,mke/mume,ndugu) hapo haliwezi kuwa tatizo la benki iwapo password yako itahujumiwa.benki haitahusika.
  Fingerprint ndio komesha kabisa, kama unapenda mtu mwingine awe na access na account yako unaposafiri au kuugua, ulipaswa ukamjazishe fomu flani na maelezo kwa permission na committment zako ndani ya benki.Na iwe uwezekano wa kuchukua hizo hela ndani (kwa teller) kwa kitambulisho na document maalum.Suala la ATM liwe lako binafsi.
   
 13. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,230
  Trophy Points: 280
  inaelekea nyumbani kwako na ATM mashine ni hatua 1.
   
 14. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa wateja wa CRDB jengeni utaratibu wa kucheki salio kila siku kupitia simu zenu za mikononi kwa kutumia CRDB Mobile banking
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ethics zingekuwa zinaniruhusu ningekwambia ni kwanini biological data hazitumiki
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kwenye bluu inaonekana hawa benki kama wanasita kuangalia rekodi za kamera kama vile wanafahamu vizuri kinachoendelea hapo (i.e wanafahamiana vizuri katika huu wizi). Hiyo kwenye nyekundu hapo ndo kwenye suluhu ya yote vinginevyo sasa inatia hofu kweli kweli.
   
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Vipi gharama za hii huduma mkuu zikoje?
   
 18. s

  souvenir Senior Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haswa hili jamani huo wizi mostly wafanyakazi wa ndani wanahusika sana na kesi nyingi sasa hivi ni crdb.halafu me nashangaa tangu wale Wabulgaria wakamatwe na kina nani sijui nilitegemea benk waelekeze wateja kucheki pale kwenye ile catrage wezi wanapodakia data lakini coz they know inside outside game hawawezi fanya hivyo
   
 19. s

  souvenir Senior Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tena biometric ndo mbaya zaidi coz once utakaposign in coclusively itaonyesha we mwenye account ndo umechukua.CRDB me nilitoa pesa zote Na NMB sa hivi ukichukua pesa on the sport unapokea msg kwenye simu kama sio wewe umechukua pesa uwajulishe.sa kama no ya simu ulibadilisha rhat is up to you
   
 20. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  hapo kwenye red inasaidia sana kwa haraka kujua kama kuna tatizo
  ! wasiwasi wangu pia ni kama bank itaweza kushughulikia hizo taarifa kwa haraka mara upatapo hiyo sms, iwapo utataka kuwajibu aliyetoa hela kwenye a/c yako sio wewe (ni mwizi).kama hawatakuwa faster kushughulikia itakuwa haina tofauti na mwanzoni.
   
Loading...