Aibiwa fedha zote kwenye akaunti kwa NBC MasterCard kupitia ATM

Modus- Operand:

Unapoagiza Kadi mpya, kabla ya kukupa kadi wale Jamaa wa IT/Card Manager wanaweza kuwa na computer scana ambayo akiscan/swipe card yako inaacha kumbukumbu kwenye computer hivyo anachukuwa plain card na kuscan tena, hiyo plain card inachukuwa kumbukumbu ya card yako waliyoscan mwanzoni. na bahati mbaya namba ya siri wanazifahamu. hivyo inakuwa rahisi kwao kuchota kwenye account yako. wewe ukichota na wao wanachota. Kwa wale wenye amount kubwa benki wasitumiye ATM labda kwa lazima sana.

Computer Scana/swipe za namna hiyo zipo nyingi sokoni kwa sasa.









Wizi wa elektoniki unaonesha kushika kasi jijini baada ya watu wawili kuibiwa fedha zao kwa kutumia MasterCard.

Mmoja wa waandishi waandamizi wa gazeti la HabariLEO, Bantulaki Bilango mwenye akaunti namba 017201056410 iliyofunguliwa katika tawi la NBC Moshi ameibiwa zote zilizokuwemo kwenye akaunti yake kupitia ATM ya tawi la Benki hiyo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutoa taarifa NBC Makao Makuu yaliyopo Mtaa wa Sokoine Drive mapema leo, Bilango alisema baada ya kutoa fedha katika akaunti yake kupitia ATM iliyopo tawi la benki hiyo la Viwandani barabara ya Nyerere jana, leo alikupokwenda ATM zilizopo katika tawi la Corperate, alikuta fedha hizo zimechukuliwa muda mfupi kabla yake.

Taarifa ya benki aliyopewa ilionesha kuwa pesa hizo zilitolewa leo asubuhi katika ATM iliyopo Kinondoni.

Scan sehemu ya statement uonyeshe jinsi gani mwizi huyo alivyoiba.

“Jamani huu wizi ni wa aina yake. Mimi nimechuka Master Card yangu juzi tu leo hii kuna mtu amekomba pesa zangu zote kwenye ATM,” alisema .

Hata hivyo alipoomba waangalie kamera zao kwa kuwa kila anayeingia kwenye mashine za ATM humulikwa walidai kuwa hiyo ni hatua ya juu sana inayohusisha polisi, hivyo hawawezi kufanya hivyo kwa wakati ule.

Hata hivyo, Bilango anasema alipata ushirikiano mzuri katika tawi la benki ya Viwandani katika barabara Nyerere alikochukulia fedha jana ambapo msimamizi wa Huduma kwa Wateja na Huduma za Biashara na Nje, Matilda Manumbu kwa kushirikiana na viongozi wengine wa benki hiyi waliahidi kufuatilia kwa karibu ili kuweza kumpata mhusika.

Kulingana na maelezo ya Bilango, kadi iliyokuwa ikitumika kuiba fedha ni ile ile ambayo alikuwa anayo mfukoni. Alisema la kushangaza, wakati yeye akiwa nayo, mtu mwingine alikuwa akiendelea kutoa fedha katika ATM.

Mmoja wa wateja alisema wizi huo unaoweza kufanyika kwa kuwatumia wafanyakazi wa benki lakini wakati mwingine kuna carbon inaachwa kwenye mashine ya ATM ambapo mteja akiweka kadi, taarifa zake zinanaswa kwenye carbon hiyo na baada mwizi kutumia taarifa hizo kuiba fedha hizo katika ATM nyingine.

Alishauri wateja kuacha kutumia njia hiyo na badala yake watumie dirisha kwa kuwa mashine hizo zinatumiwa vibaya.

Wizi huo unaonekana kukithiri hasa katika tawi la Kinondoni ambapo mteja mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake alichukulia fedha zake katika tawi hilo la Viwandani, kisha kuibiwa fedha zake kupitia tawi la Kinondoni wiki iliyopita kwa kutumia kadi yake ya ATM .

“Nami nimelizwa, lakini wamesema wanashughulikia, hivyo naamini fedha zangu zitarudishwa maana walichukua mshahara wangu wote.

Tukio hilo lilimpata tena mkazi mwingine, Fabian Rugaimukamu mwenye akaunti namba 2012401429 katika benki ya NMB tawi la Bank House.


Source: ziro99blog: MWANDISHI AKOMBWA FEDHA ZOTE ATM YA NBC...
 
Niliwahi kusikia kesi CRBD, mteja aliibiwa usiku wa manane, alijua hilo baada ya kukuta ujumbe subuhi, alipokwenda benki akajaza fomu na kuambiwa asubiri baada ya siku 45 ili uchunguzi ufanyike.
Business Manager akasema ni vigumu kuwatambua wezi kirahisi pale wezi wanapotumia ATM za benki tofauti, na hali ni tete kwa sasa.
 
Always CRDB is it coincedence?there is a game around amkeni Wabongo jamani tunapenda sana kuchukulia vitu easy
 
Nimepokea taarifa toka kwa rafiki zangu watano kuwa fedha katika akaunti zao za NBC zimekombwa usiku wa tarehe 05 October kuamkia jumamosi tarehe 06. Sasa nimeamini kweli NBC ni kichaka cha wezi, tumeshauriana kesho mguu kwa mguu hadi kwa lawyer tupate ushauri na baadaye twende NBC na baada ya hapo twende kwenye vyombo vya habari. Hapo ni lazima NBC wajue kama maharage ni mboga au ni chakula. Nina hasira nao hawa wezi wakubwa.
 
Sometimes vitu vidogo tu ambavyo tunaignore they can save us. Jenga utamaduni kutoa hela kwenye ATMs ambazo kuna benki yako hapo, most identity stealing huwa zinatokea on ATMs away from banks eg petrol station,malls etc
 
Ila na local banks zetu hazitaki kuwekeza kwenye security systems zao, wanatengeneza faida ila hawazibi mianya ya wizi hili ni tatizo ambalo kwa vijana wa mjini ni fursa kama kupanda kichanja cha farasi.
 
Mimi ili suala la wizi wa ATM nilishawahi kulisikia sana toka mda mrefu nikaanza kufuatilia kwa makini unavyofanyika,kitu kinachotokea hapa kuna kitu kinachoitwa card reader,hii ni external device ambayo ni very thin ambayo mwizi wa ATM anaichomeka kwenye sehemu ya ATM ya kuchomeka kadi ,hii Card reader ukifika pale hutaweza kuitambua kabisa kwa hiyo ukichomeka kadi yako Card Reader itarecord details zako zotee.Baada ya mda huyo mwizi wa ATM atarudi kwenye ATM ataichomoa hiyo Card reader ataondoka nayo,baadae hiyo card reader anaiconnect kwenye laptop ambayo inasoftware maalumu ya kuread hizo details na hiyo laptop iko connected na card printer,hivyo anaprint detail za watu idadi anayotaka hata kumi baadae anazichukua hizo cards na kwenda kuzitoa hizo fedha kilaini kadri anavyohitaji.
 
Nimepokea taarifa toka kwa rafiki zangu watano kuwa fedha katika akaunti zao za NBC zimekombwa usiku wa tarehe 05 October kuamkia jumamosi tarehe 06. Sasa nimeamini kweli NBC ni kichaka cha wezi, tumeshauriana kesho mguu kwa mguu hadi kwa lawyer tupate ushauri na baadaye twende NBC na baada ya hapo twende kwenye vyombo vya habari. Hapo ni lazima NBC wajue kama maharage ni mboga au ni chakula. Nina hasira nao hawa wezi wakubwa.

And MD Mafuru is back to office w.e.f today
 
CRDB wanajitahidi, ukijiunga na ile simBanking yao kwa kupiga *150*03# unaweza kuangalia balance yako muda wowote. Lakini nzuri zaidi ni pale unapotoa hela kwenye ATM yao, wakati hela zinatoka tu kwenye ATM sms inaingia kwenye sim yako kutoka CRDB "Ndugu mteja kadi yako inayoishia na namba xxxx imetumika kutoa kiasi cha shs xxxx tarehe xxxx saa xxxx katika ATM ya xxxx, kama huutambui muamala huu piga namba 0714197700" Mimi nimejiunga na huduma hii na mara zote nitoapo fedha lazima nipate ujumbe huu kabla sijatoka kwenye ATM.

My take;
Huyo bwana angekuwa anatumia CRDB card na amejiunga na simbanking angepata ujumbe huo hata kama ni usiku wa manane angepiga hiyo namba ya msaada na wahusika wangewasiliana na askari wanaolinda hizo ATM(mara nyingi ni wa makampuni binafsi) na mara moja wangemkamata huyo mwizi kabla hajavuka mlango wa kutoka katika ATM.
 
Atm za vichochoroni ni hatari bora uende sehemu ambaz ziko bussy hakuna mtu anaeweza kufanya ujanja huo za uchochoro unakuta askari mmoja kachoookaa anasinzia na kujambajamba akienda msalani mtu anaingia na kuweka vifaa kukopi taarifa za wateja ndugu jenga tabia ya kubadilisha password kwa mwezi mara 4 yaani kila wiki na passsword mpya!!
 
nilijua kwangu tuu!! mr wamemkombea hela zote nbc, anafatilia hadi leo hawampi hata majibu ya kueleweka karibu mwezi sasa
 
Nimepokea taarifa toka kwa rafiki zangu watano kuwa fedha katika akaunti zao za NBC zimekombwa usiku wa tarehe 05 October kuamkia jumamosi tarehe 06. Sasa nimeamini kweli NBC ni kichaka cha wezi, tumeshauriana kesho mguu kwa mguu hadi kwa lawyer tupate ushauri na baadaye twende NBC na baada ya hapo twende kwenye vyombo vya habari. Hapo ni lazima NBC wajue kama maharage ni mboga au ni chakula. Nina hasira nao hawa wezi wakubwa.

...Maa Mdogo,Ndugu zako wamefikia Wapi? Waombe waharakishe kwenda Vyombo vya Habari ili Kuwakoa Watanzania wenzao wenye Vijisenti vyao kwenye hiyo Benki wasije nao wakakombewa. Hii Itasaidia pia Uongozi wa Benki husika kuchukua hatua za Haraka na Madhubuti kushughulikia suala hilo...!
 
Back
Top Bottom