Ahukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kumuua mke wake bila kukusudia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mhandisi, Novat Kaberwa baada ya kukiri kosa la kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake na kumsababishia umauti baada ya kurudi nyumbani saa 3 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, kisha baadaye akarudi nyumbani akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoachiwa.

Hukumu imetolewa na Msajili wa mahakama, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa alimuua mke wake bila kukusudia
 
Alimpiga kiasi gani?na kwakutumia nn? km ametumia makofi na ngumi machache tunaweza kusema hvyo lakin km ni silaha amekusudia.

hata na hvyo ilishndikana nini kumfukuza achukue hamsini zake?hao watoto aliwaacha njaa bdo watakuona baba katili na mwuaji,amemwua mama kikatili
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mhandisi, Novat Kaberwa baada ya kukiri kosa la kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake na kumsababishia umauti baada ya kurudi nyumbani saa 3 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, kisha baadaye akarudi nyumbani akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoachiwa.

Hukumu imetolewa na Msajili wa mahakama, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa alimuua mke wake bila kukusudia
Kosa lilifanyika lini? Unaweza kukuta kesha kaa mahabusu miaka mitano.
 
Ungekua na knowledge ya sheria usingeandika hiyo comment.

Kuua mtu peke yake hakumfanyi mtu kuwa na hatia, wanaangali kitendo ulichofanya na kiwango cha kusudio lako wakati unatekeleza huo uhalifu.
nina knowledge pengine kukushinda
 
Back
Top Bottom