Ahukumiwa kwenda jela miaka 2 kwa kumuua mke wake bila kukusudia

ukimuachia hela ndugu yako ya chakula akienda kulewa watoto wakabaki na njaa unamuua si ndio??? basi safi sana
Kumbuka mtu anaweza kufa hata kwa kunaswa kibao kimoja tu. Huenda alikasirika sana akamzaba vibao kadhaa kwa lengo la kumuadhibu bahati mbaya binti akapoteza maisha jambo ambalo halikuwa kusudio lake. Ww hujawahi kumpiga mtu yeyote au hata kumsukuma tu? Umewahi kuimagine kitendo hicho tu kinaweza kupelekea mauti?
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mhandisi, Novat Kaberwa baada ya kukiri kosa la kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake na kumsababishia umauti baada ya kurudi nyumbani saa 3 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, kisha baadaye akarudi nyumbani akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoachiwa.

Hukumu imetolewa na Msajili wa mahakama, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa alimuua mke wake bila kukusudia
Ah muwache afe tu huyo mama.
Utaendaje kulewa na kuacha watoto njaa ??
 
Yani miss zomboko akishaleta mada huyooo humuoni tena jukwaani sijawahi kuona comment yake.

Ila asante sana kwa habari motomoto.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mhandisi, Novat Kaberwa baada ya kukiri kosa la kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.

Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake na kumsababishia umauti baada ya kurudi nyumbani saa 3 usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, kisha baadaye akarudi nyumbani akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoachiwa.

Hukumu imetolewa na Msajili wa mahakama, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa alimuua mke wake bila kukusudia
Naomba kuulza, mfano umemwacha mpenz af akajiua, akaacha ujumbe kiwa amejiua kisa umemwacha..hapa sheria inasemaj?
 
Mambo ya ndoa unaweza kufanya jambo hadi jamii ikakushangaa, inahitaj hekima sana kuishi na mtu mzima mwenzako
 
Unahisi nalingishia au

Manslaughter

Okay, manslaughter ndio kuua bila kukusudia.

Kwa hiyo manslaughter haina mens rea (nia ama kusudio ovu)?

Kwa maneno mengine, kama hakuna kusudio ovu (mens rea) kwa nini unafungwa?
 
Back
Top Bottom