Ahsante Halima Mdee...

Ahsante Halima Mdee...

Status
Not open for further replies.
Kwa heshima napenda kumpa ahsante Mbunge wa Chadema Mheshimiwa Halima Mdee kwa haya:

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa CHADEMA kikiwa chini ya Mtendaji wake mkuu (KATIBU MKUU-TAIFA), Mhe. Wilbroad Peter Slaa. Hakika kila Mtanzania anaona kazi unayoifanya ya kuhakikisha chama chetu kina kuwa juu na Watanzania wote wanatuunga mkono. Mungu akupe uhai, naamini ipo siku tutaifikia Nchi ya Ahadi! - Halima Mdee Bungeni 11-07-2012 .

Soma zaidi: "tutaifikia Nchi ya Ahadi".

Mheshimiwa Zomba, elimu yako ya sekondari umesoma Tanzania?
Kama jibu ni ndio, basi katika somo la kiswahili kwa elimu ya sekondari kuna kitu kinaitwa "Tamathali za Semi" mfano Dhihaka, tafsida ,kejeli/shitizai, Sitiari, Tashibiha, Tashihisi, Mubaalagha, Tabaini, Takriri.
Tafadhali rejelea hayo mafundisho, hakika utamuelewa Bi. Mdee
 
Wewe unasema hayo, tazama huyu mwenzio anasemaje:

Na huyu:

Huyu mwenzenu anakiri kuwa hayo ni

Nawashangaa, maneno yangu mimi ni haya tu "Kwa heshima napenda kumpa ahsante Mbunge wa Chadema Mheshimiwa Halima Mdee kwa haya".

Ni kipi kilichowakwaza? Nimebandika maneno ya Halima Mdee nikaweka na mafundisho "very deep" ya Mwakasege, sijatia langu zaidi ya heshima na kumpa ahsante Mheshimiwa Halima Mdee. Unajuwa mnashangaza sana mnapokurupuka na kupinga ambacho hata sijui mnapinga nini? nawauliza, mnapinga maneno ya Halima Mdee? au ya Mwakasege au Ahsante yangu?

dogo acha unafiki jana si ulipost hii thread au umei-renew? Mbona hakuna issue au jaribu kuwa wazi unataka kusemaje?
 
Pamoja kuwa mimi ni mwislam lakini mwenzetu hapo umepotosha, ukifurahishwa na usemi kwenye kitabu cha dini waweza kuutumia. Ndo maana watu wengi hata si waislam inshallah nk. Hiyo akili chafu mnayoitumia CCM imepitwa na wakati, kila chama kinachokuja juu mnakizushia udini kama mlivyo izushia CUF na watanzania wapumbavu wakaamini kuwa ni cha dini. Waislam wenzangu, nawaomba msiwaamini wahuni kama kama hawa, hakuna chama chochote Tanzania kinawezashinda kwa kupitia udini. Pamoja kwamba Halima mdee ni mwislam mwenzetu lakini bado huyu jamaa anajitahidi kuunga hoja isiyo na maana. Watanzania tusonge mbele pamoja, udini tuushinde tubadirishe nchi yetu. Allahu akbar

pamoja mkuu!
 
Mheshimiwa Zomba, elimu yako ya sekondari umesoma Tanzania?
Kama jibu ni ndio, basi katika somo la kiswahili kwa elimu ya sekondari kuna kitu kinaitwa "Tamathali za Semi" mfano Dhihaka, tafsida ,kejeli/shitizai, Sitiari, Tashibiha, Tashihisi, Mubaalagha, Tabaini, Takriri.
Tafadhali rejelea hayo mafundisho, hakika utamuelewa Bi. Mdee

Nimemuelewa sana muktadha (naona katika nahau zako zote hilo umelisahau) wake Mheshimiwa Halima Mdee, hususan alipoelekeza ubeti huo wenye kina wa "tutaifikia Nchi ya Ahadi" kwa Dokta wa Kanoni Slaa. Na ndiyo maana nikamwambia "Ahsante Halima Mdee".

Nikamsoma Mwakasege katika mafundisho yake kuhusu maana ya kuifikia Nchi ya Ahadi, sina shaka na mafundisho hayo na sina shaka Halima Mdee anajuwa anachokiandika na hakukurupuka na bila ya shaka nikampa ahsante kwa hilo. "Mcheza kwao hutunzwa".

Jee, kuna mghafala hapo au ni ukhafaf wako tu?
 
dogo acha unafiki jana si ulipost hii thread au umei-renew? Mbona hakuna issue au jaribu kuwa wazi unataka kusemaje?

Niliyo-i-post jana ipo kwenye link, hujaona link kwenye post #1 au unakurupuka tu.
 
Nimemuelewa sana muktadha (naona katika nahau zako zote hilo umelisahau) wake Mheshimiwa Halima Mdee, hususan alipoelekeza ubeti huo wenye kina wa "tutaifikia Nchi ya Ahadi" kwa Dokta wa Kanoni Slaa. Na ndiyo maana nikamwambia "Ahsante Halima Mdee".

Nikamsoma Mwakasege katika mafundisho yake kuhusu maana ya kuifikia Nchi ya Ahadi, sina shaka na mafundisho hayo na sina shaka Halima Mdee anajuwa anachokiandika na hakukurupuka na bila ya shaka nikampa ahsante kwa hilo. "Mcheza kwao hutunzwa".

Jee, kuna mghafala hapo au ni ukhafaf wako tu?

Hahahaa...Mkuu Zomba ni vyema tu kumuelewa mheshimiwa Bi. Mdee kuwa alikua anamithilisha "kuifikia Nchi ya Ahadi" kwenye maziwa na asali kwa Wayahudi kama nuio lao kuondokana na dhiki na kadhia za jangwani.
Alichokosea labda uniambie wale walisafiri toka eneo moja la kijiografia kwenda eneo jingine. Lakini sisi Tanzania kama Nchi na Taifa(Watanzania), hatuna mahali pa kwenda kwani hapa ndio kwetu. Kama kuna ahadi yoyte iliyotolewa juu yetu kuifikia nchi fulani, basi nchi hiyo ndio hii. Ila ambacho tunapaswa kukifikia ni muda ambao tutakula na kusaza hizo asali na maziwa (maliasili za nchi yetu).
Heshima kwako mkuu...
 
Pamoja kuwa mimi ni mwislam lakini mwenzetu hapo umepotosha, ukifurahishwa na usemi kwenye kitabu cha dini waweza kuutumia. Ndo maana watu wengi hata si waislam inshallah nk. Hiyo akili chafu mnayoitumia CCM imepitwa na wakati, kila chama kinachokuja juu mnakizushia udini kama mlivyo izushia CUF na watanzania wapumbavu wakaamini kuwa ni cha dini. Waislam wenzangu, nawaomba msiwaamini wahuni kama kama hawa, hakuna chama chochote Tanzania kinawezashinda kwa kupitia udini. Pamoja kwamba Halima mdee ni mwislam mwenzetu lakini bado huyu jamaa anajitahidi kuunga hoja isiyo na maana. Watanzania tusonge mbele pamoja, udini tuushinde tubadirishe nchi yetu. Allahu akbar

Hapo juu kuna chochote kuhusu Uislaam au Ukristo> au unajishuku tu? kuna neno langu hapo zaidi ya kumpa Ahsante Mheshimiwa? soma vizuri post yangu namba moja uniambie hayo yote uliyoyaleta yanahusu nini?

Umesema wewe ni Muislaam, ngoja nikukumbushe kipande hiki katika Sura 2 aya ya 14.

Q. 2:14. Na wanapo kutana na walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao na mashet'ani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi. Hakika sisi tunawadhihaki tu.
 
Hahahaa...Mkuu Zomba ni vyema tu kumuelewa mheshimiwa Bi. Mdee kuwa alikua anamithilisha "kuifikia Nchi ya Ahadi" kwenye maziwa na asali kwa Wayahudi kama nuio lao kuondokana na dhiki na kadhia za jangwani.
Alichokosea labda uniambie wale walisafiri toka eneo moja la kijiografia kwenda eneo jingine. Lakini sisi Tanzania kama Nchi na Taifa(Watanzania), hatuna mahali pa kwenda kwani hapa ndio kwetu. Kama kuna ahadi yoyte iliyotolewa juu yetu kuifikia nchi fulani, basi nchi hiyo ndio hii. Ila ambacho tunapaswa kukifikia ni muda ambao tutakula na kusaza hizo asali na maziwa (maliasili za nchi yetu).
Heshima kwako mkuu...

Halima Mdee hakuelekeza beti hiyo kwa Dokta Slaa bila ya kuwa na ujumbe mzito, Halima Mdee ni zaidi ya umjuavyo. Naomba isome maana kamili hapa: "tutaifikia Nchi ya Ahadi".
 
Wewe unasema hayo, tazama huyu mwenzio anasemaje: Na huyu: Huyu mwenzenu anakiri kuwa hayo ni Nawashangaa, maneno yangu mimi ni haya tu "Kwa heshima napenda kumpa ahsante Mbunge wa Chadema Mheshimiwa Halima Mdee kwa haya". Ni kipi kilichowakwaza? Nimebandika maneno ya Halima Mdee nikaweka na mafundisho "very deep" ya Mwakasege, sijatia langu zaidi ya heshima na kumpa ahsante Mheshimiwa Halima Mdee. Unajuwa mnashangaza sana mnapokurupuka na kupinga ambacho hata sijui mnapinga nini? nawauliza, mnapinga maneno ya Halima Mdee? au ya Mwakasege au Ahsante yangu?
Wanachopinga ni mantiki ya wewe unayejiita GT kuweka upuuzi kama huu hapa...wenye akili timamau wanajua Halima alimaanisha nini na yeye mwenyewe anajua alichomaanisha....Hata Civics ya form II inafundisha lengo la chama cha siasa ni nini... Na Literature ya form III inafundisha pia matumizi ya lugha ya picha kwahiyo ukilaza na umbmbumbu wako tafuta jukwaa la vilaza ukasemee huko...Sipati picha huyo halima angekuwa mkristo ingekuwaje.......THINK LOUD.....
 
Kwa hilli zomba kufikiri kwako kuna tia mashaka.

Kazi yako ni kuwagawa watu kwa kutafsiri maneno bila kufikiri,,dhambi ya udini itaendelea kukutafuna na hauto acha kuleta mada ambazo hazina tija.

Na ugonjwa unao umwa hautibiki.
 
Wanachopinga ni mantiki ya wewe unayejiita GT kuweka upuuzi kama huu hapa...wenye akili timamau wanajua Halima alimaanisha nini na yeye mwenyewe anajua alichomaanisha....Hata Civics ya form II inafundisha lengo la chama cha siasa ni nini... Na Literature ya form III inafundisha pia matumizi ya lugha ya picha kwahiyo ukilaza na umbmbumbu wako tafuta jukwaa la vilaza ukasemee huko...Sipati picha huyo halima angekuwa mkristo ingekuwaje.......THINK LOUD.....

Hivi ni kipi usichokielewa kwenye post namba moja kuna lolote kati ya hayo uliyoandika? mimi nimemsifu kwa kumpa ahsante. nalo pia ni baya? shule sijui, ukristo sijui Halima angekuwa vipi, yote yanahusu nini hayo? au nimegusa pasipotakiwa?
 
Context ni hii hapa, ni wapi ilipokaa "kisharishari" tafadhali nifahamishe:

Haitatokea shabiki wa Simba na jezi yake nyekunde akakae jukwaa la kijani kushangilia Yondani akiwagalagaza Msimbazi..
 
Haitatokea shabiki wa Simba na jezi yake nyekunde akakae jukwaa la kijani kushangilia Yondani akiwagalagaza Msimbazi..

Wakiwa timu ya Taifa? kwi kwi kwi teh teh teh!
Halima-Mdee.jpg

Yanga

HALIMA+MDEE.jpg

Simba
 
Wakiwa timu ya Taifa? kwi kwi kwi teh teh teh!

Aisee hii kali wapi pameandikwa Timu ya Taifa..?! Afu timu ya Taifa wanavaaga jezi nyekundu na njano wamenza lini?
 
Aisee hii kali wapi pameandikwa Timu ya Taifa..?! Afu timu ya Taifa wanavaaga jezi nyekundu na njano wamenza lini?

Taifa la "Nchi ya Ahadi". Wewe haumo?
 
Martin Luther king,JR kwenye hotuba ya 'I SEE THE PROMISED LAND' april 3,1968 memphis,Tennessee alimaanisha huo uozo wako,kumbe ukubwa wa kichwa sio wingi wa makamasi..vichwa vingine vina makamasi sio ubongo ama kweli kila ubongo uko kwenye kichwa ila si kila kichwa kina ubongo!
 
big up halima hurreeeey chadema umeongea na tumekusikia kabisa tena kwa makini halima you are a hero hawa magamba waseme tuu lakini tutawafundisha tuu wakitugesi gesi kwenye ardhi yetu na hawa wawekezaji
 
Kwa heshima napenda kumpa ahsante Mbunge wa Chadema Mheshimiwa Halima Mdee kwa haya:

Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa CHADEMA kikiwa chini ya Mtendaji wake mkuu (KATIBU MKUU-TAIFA), Mhe. Wilbroad Peter Slaa. Hakika kila Mtanzania anaona kazi unayoifanya ya kuhakikisha chama chetu kina kuwa juu na Watanzania wote wanatuunga mkono. Mungu akupe uhai, naaminiipo siku tutaifikia Nchi ya Ahadi! - Halima Mdee Bungeni 11-07-2012 .

Soma zaidi: "tutaifikia Nchi ya Ahadi".

Hii imetulia big up jembe.IPO SIKU TUTAFIKA NCHI YA AHADI.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom