Ahsante Dangote na serikali, bei ya cement Morogoro 9,800

LAPTOP2016

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
728
2,140
Kwa hili napenda kuipongeza serikali na kampuni ya cement Dangote, bei ya cement imekua nafuu sana kwa wale wanaojenga wakati huu, najua kwa Dar itakua pungufu zaidi ila sisi wa mji kasoro bahari tunanunua kwa shilingi 9,800.
 
Mwezi wa pili nilikuwa sehemu moja Mbeya....inaitwa Kiwira madukani Tukuyu huko, cement nikanunua mfuko 16,500.... Wakati mwezi huo huo Ifakara Moro nikanunua 12,500...... Moro mjini nikakuta ni 11,000....

Saizi naona Moro kila muuza cement anaweka mabango barabarani akitangaza bei yake....huyu 10,400....10,500.....10,700........10,000......naona sasa inazidi kuja chini.....mahindi na unga nao unakuja bei chini....kuna mahali panaitwa Lukobe....kuna mtu kilo moja ya unga anauza 1,500.... Sukari anauza 2,000. Naona mambo yanaanza kulegea....japo mfukoni kuna utata
 
Hivi jamani cement ya Dangote kwa Kahama inapatikana kwa bei gani? Anaye jua tafadhali. Na kama nataka mifuko mingi mfano 700-800 bags wanaweza kuniletea? Eneo ni kama Km 150 Kutoka Kahama.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Kanda ya ziwa hali bado tete.

Kahama 16,000.

Usafiri wa uhakika wa reli ni muhimu sana kwenye kupunguza huu utofauti wa bei kati ya Kanda moja na nyingine.

Gharama za Usafirishaji WA bidhaa kwa malori ni soo.
 
Hivi jamani cement ya Dangote kwa Kahama inapatikana kwa bei gani? Anaye jua tafadhali. Na kama nataka mifuko mingi mfano 700-800 bags wanaweza kuniletea? Eneo ni kama Km 150 Kutoka Kahama.
Mkuu ni vizuri ufuatilie mawasiliano ila semi huwa linabeba tani 3o ambayo ni mifuko 600 mkuu
 
Kanda ya ziwa hali bado tete.

Kahama 16,000.

Usafiri wa uhakika wa reli ni muhimu sana kwenye kupunguza huu utofauti wa bei kati ya Kanda moja na nyingine.

Gharama za Usafirishaji WA bidhaa kwa malori ni soo.
Yeah gharama za usafiri ndizo ishu mkuu
Zinaleta tofauti ya hizi bei
 
Back
Top Bottom