Ahadi za mlaji Vs sera (Promises: Consumer Oriented Vs Policy Oriented ) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi za mlaji Vs sera (Promises: Consumer Oriented Vs Policy Oriented )

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by valour, Sep 18, 2010.

 1. v

  valour Senior Member

  #1
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jana katika kipindi cha 'This week in Perspective' kinachorushwa na TBC1, mwezeshaji wa kipindi alikuwa anawahoji Prof. Rweitama (UDSM), Maria Shaba (freelance journalist), Dr. Kitine (kada wa CCM) na Richard Mgamba wa gazeti la Guardian kuhusu kampeni za wagombea wa Urais. Walijadili mambo mengi lakini mjadala huo ulielekezwa zaidi kwa CCM na CHADEMA na sio vyama vingine. CUF ilijitokeza kidogo sana.

  Pamoja na mambo mengi mazuri waliyojadili mimi niliguswa sana na mjadala wa ahadi ambazo wagombea wamekuwa wakizitoa. Prof. Rweitama alisema ahadi za J.K nyingi kama sio zote zinamlenga mlaji, mfano atajenga uwanja wa kimataifa wa ndege (Kigoma na Bukoba), atanunua meli ziwa victoria, atanunua bajaji, atanunua kivuko ziwa nyasa nk. Ambayo kimsingi inaweza isimguse mwananchi wa kawaida moja kwa moja.

  Kwa upande wa Dr. Slaa yeye ahadi zake zimelenga katika sera kwamba atatoa elimu bure, atapunguza kodi kwa vifaa vya ujenzi hasa vijijini ili mwananchi wa kawaida aweze kumudu gharama za ujenzi, atapunguza mshahara wa urais kwa 20% na wabunge 15% etc. Kwa njia moja au nyingine mwananchi wa kawaida atafaidika moja kwa moja.

  Dr. Kitine huwa ni msemaji na mzungumzaji sana lakini kwenye mada hii alishindwa kuzungumza na mara nyingi alionekana dhahiri kukubaliana na wenzie kwasababu mambo mengi yalionekana kuwa na logic. kwahili ningependa kumpa credit.

  Ningemshauri JK nae aanze ku-focus kwenye sera kwasababu kwa njia hiyo mwananchi wa kawaidi ataguswa na hizo neema ambazo zinategemewa kutolewa.

  Ni bahati mbaya hiki kipindi kinazungumzwa kwa lugha ya kiingereza lakini ingesaidia sana kwa wananchi kuangalia mada kama hizi ili waweze kutoa maamuzi sahihi na makini ifikapo tarehe 31/10/2010
   
 2. e

  emalau JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Jana akiwa mto wa mbu ameahidi kulipa ng'ombe wa wamasai waliopotea!!!! ha ha ha ha ha ha ha ha! na akamsifia Lowasa kwamba ni mchapa kazi tehe teh tehe teh ha eti ndo rais mtarajiwa !
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kazi zipi hizo anazochapa sana? ina maana watanzania ni wageni? atumjuhi lowasa?
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  .....watanzania tunaongea vya kutosha na-argue tufanye actions!! hawa CCM wanatufanya vituko for granted kwamba watanzania wapole na watu wa amani so they (CCM) do what they do!!!!
   
Loading...