Mabadiliko yoyote yanaanza na mtu binafsi ambaye ana msimamamo, nia, na uelewa jua ya mazingira yake. Mtu ambaye ameamua kwamba niwe peke yangu au na wenzangu nitatimiza nia yangu. Ni mtu ambaye halaumi wananchi kwamba hawawezi, ama mfumo unamizizi isiyongoleka bali anaimani safari huanza hatua kwa hatua, na pale utakapoianza wengine watakuja.
Ninachopendekeza hapa ni tujiangalie sisi wenyewe na kujifanyia tathimini juu mabadiliko tunayoyaongelea kila siku. Tujitambue kama manunguniko yetu juu ya umaskini, ufisadi, uongozi, elimu, Zanzibar, iwapo yanajenga msimamo wowote ndani ya nafsi zetu. Kabla hatujamuangalia mtu mwingine, je sisi tunajitambua na tunamisimamo madhubuti juu ya mabadiliko tunayoyataka. Tumejipa majukumu?
Kwa maneno mafupi kabisa yasiyopinda toa ahadi yako ni mabadiliko yapi unataka kuyaona katika uchaguzi wa 2010, na cha msingi zaidi wewe kama mwananchi wa tanzania utashiriki vipi katika kuleta mabadiliko hayo!