Ahadi Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi Yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Petu Hapa, May 2, 2009.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko yoyote yanaanza na mtu binafsi ambaye ana msimamamo, nia, na uelewa jua ya mazingira yake. Mtu ambaye ameamua kwamba niwe peke yangu au na wenzangu nitatimiza nia yangu. Ni mtu ambaye halaumi wananchi kwamba hawawezi, ama mfumo unamizizi isiyongoleka bali anaimani safari huanza hatua kwa hatua, na pale utakapoianza wengine watakuja.

  Ninachopendekeza hapa ni tujiangalie sisi wenyewe na kujifanyia tathimini juu mabadiliko tunayoyaongelea kila siku. Tujitambue kama manunguniko yetu juu ya umaskini, ufisadi, uongozi, elimu, Zanzibar, iwapo yanajenga msimamo wowote ndani ya nafsi zetu. Kabla hatujamuangalia mtu mwingine, je sisi tunajitambua na tunamisimamo madhubuti juu ya mabadiliko tunayoyataka. Tumejipa majukumu?

  Kwa maneno mafupi kabisa yasiyopinda toa ahadi yako ni mabadiliko yapi unataka kuyaona katika uchaguzi wa 2010, na cha msingi zaidi wewe kama mwananchi wa tanzania utashiriki vipi katika kuleta mabadiliko hayo!
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  May 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hapa Petu,
  Mkuu wangu kila mtu anapenda sana kuchangia pale anapotakiwa kuweka mchango wake..Tatizo la nchi yetu ni sawa na timu ya Mpira...UongozI wa timu ukiwa mbaya,kipewnzi cha timu hiyo ana kila haki ya kulaumu..timu ikiwa mbovu mshabiki ana kila haki ya kulalamika hata kama yeye hajui kuucheza..Hatuwezi wote kuwa wanasiasa na sio lazima kila mmoja wetu afe na uwezo wa kucheza mchezo huu kuzungumzia mapungufu ya nchi yetu..
  Hunishangaza sana pale tunapotaka kila mmoja wetu awe mchezaji wakati tunafahamu kabisa wachezaji (serikali) ni kundi dogo sana la watu waliochaguliwa...Na siwezi kuingia uwanjani hata kama naweza kuucheza kwa sababu itakuwa nje ya taratibu za mchezo huu..
  Hivyo mimi nitabakia shabiki na timu yangu Tanzania naipenda sana kiasi kwamba nitaendelea kugombana na Uongozi au timu iliyotuwakilisha maadam kila ligi tunabugia magoli.. something is wrong iwe inatokana na Uongozi, Kocha na hata wachezajui wenyewe..
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkandara

  Kuleta mabadiliko sio lazima uwe kiongozi! Ama useme nitagombea nafasi fulani au nitaiongaza serikali! Ama nitakuwa mwanachama wa siasa! Sio lazima uwe kwenye siasa uweze kushiriki katika mabadiliko!

  Tukirudi kwenye mfano wako wa mpira, timu inawachezaji wake 11 na wale wa akiba - hawa ndio tunawaona watu muhimu sana. Lakini amini na kwambi iwapo mashabiki wasingekuwepo! Wachezaji wa mpira wangepata faida gani! Ni ndani ya ushabiki wetu, wachezaji wa mpira wanapata umaarufu, pesa ya kula, na huku makocha na waandishi wakipata ajira! Katika ushabiki! kunawale ambao wanakwenda uwanjani kuangalia mechi, kunawale wanaongalia kupitia luninga, wengine radioni, wengine wanasoma magazetini. Na lipo lilekundi wanaosimuliwa. Kunawashabiki wengine wanakuwa wahisani, wengine wanakuwa wapiga debe, wengine watafuta wananchama wapya!

  Ni katika mfumo kama huo ambapo, majukumu yetu hayawezi kuwa sawa! Wala hayapaswi kuwa sawa! Kila mmoja kwa nafsi yake atakuwa na jukumu lake ndani ya nafasi yake lakini sote tukiwa na nia ya kufanya timu zetu zishinde, sio kwa washindani wajadi, bali itupe burudani zaidi na ipambane hata nje ya taifa letu! Uzuri wa washabiki wa timu za mpira wao hawana ukungu katika nia ya timu yao! Wanachotaka ni timu ya ishinde tu! Walionapesa, wasionapesa, waliowanachama, wasiowananchama, mechi itakapochezwa watashiriki iwe kwa kulipwa, kuzamia, kupitia luninga, kusimuliwa ama magazetini. We jua moja tu watashiriki.

  Ndio maana swali langu! kama mtu binafsi utashiriki vipi? Kwanza fanya utambuzi wa nini unataka! ndio utajua utashiriki vipi! amu timu yako ni ipi! ni chama cha siasa ama nchi?
   
 4. OsamaBinLaden

  OsamaBinLaden JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  halaf kutumia jina la mungu kamwe??? Loh

  wewe ni mwana siasa umekuja kuleta kampeni haya tuambia chama chako tukipigie kura???
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sina chama ndugu yangu!

  Mimi naamini nchi hii mabadiliko hasa kwa 2010 yatakuja tu pale ambapo watu wataona nje ya vyama vyao. Nitakupa mfano, watu wengi kwa sasa ukiwaambia ccm na chadema chama gani ni bora! wengi wanaweza kujibu ccm ama wasitoe majibu, lakini ukiwauliza wala rushwa wakubwa ni kinanani watakutajia majina - Rostam, Lowassa - etc. Pia ukiwauliza viongozi machachari watakutaji, Slaa! Mwakyembe! etc. Cha msingi hapa ni kwamba ingawaji individual politics sio za msingi na inawezekana ni hatari, lakini kwa sasa ndio zenye nguvu tanzania. Salama yetu ni kupata candidate wenye nia ya kweli ya kupunguza ufisadi tanzania na hao ndio watakaoshinda. Kwahiyo chama chochote kitakachoweza kupata wabunge wengi ni kile kitakachoangalia agenda na kyero za wananchi!

  Kura yangu mimi itaenda kwa watu nitaoamini wataleta mabadiliko na sio chama peke yake!
   
 6. E

  Epitome Member

  #6
  May 3, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Petu hapa, mimi nafikiri kwamba binadamu kwa nature yetu tulivyo ni waroho,tunapenda kujilimbikizia mali na ufahari. Hivi ndivyo tulivoumbwa. Kwa hiyo tusije tukakaa tunaomba eti tuje tupate mtu mwenye uchungu na nchi na ambayo yuko tayari kufanya mapambano na mafisadi. Tutaomba sana. Hata wenzetu walioendelea huko Ulaya na Marekani na Asia tabia za watu mara nyingi hazitofautiani sana. Tatizo kubwa tulilonalo sisi Tanzania na nchi nyingi za dunia ya tatu ni mfumo wetu wa kisiasa na kiutawala ambao umeacha mianya ya watu kuendelea kuabuse madaraka waliyopewa. Na ndio maana kuna watu wanapiga kelele kila siku kwamba katiba ibadilishwe ili kuweka mambo ya kimfumo vizuri. Katika utaratibu wetu wa uongozi wa serikali tumewapa madaraka makubwa sana viongozi wa kufanya maamuzi wenyewe hata kama taasisi nyingine zitakuwa hazikubaliani naye. Hii ni tofauti sana na nchi za dunia ya kwanza ambapo hata Rais au Waziri huwezi kufanya maamuzi fulani makubwa bila ya kupata idhini na makubaliano na labda kamati fulani. Hii ndio tofauti kubwa sana ninayoiona kati ya nchi zetu na nchi zilizoendelea. Ni mfumo uliopo na sio kwamba Gordon Brown ni mtu mwenye maadili sana kuliko Kikwete, tofauti ni kwamba Gordon Brown yuko kwenye mfumo ambao hawezi kujiamilia tu kitu chochote.

  Suala la pili ni kwamba wenzetu baada ya kutoka mbali sana wameweka utamaduni wa kutokuvumilia makosa ambayo ni obvious na makubwa yanayokwamisha maendeleo ya nchi. Na hili ni mfumo waliojiwekea. Tumesikia baadhi ya nchi za Asia kiongozi ikidhibitishwa kwamba umhusikia katika ufisadi adhabu ni kunyongwa. Huu ni mfumo ambao wenzetu wamejiwekea, na ambao unamfanya mtu yeyote anayepewa madaraka kuona harati iliyo mbele yake pale atakopofanya ufisadi.

  Kwa kuhitimisha hoja yangu, nafikiri kama sis kama nchi hatutaweka mfumo bora wa kuendesha mambo yetu, tusije tukatarajia tunaweza kupata mtu akatuonea huruma.
   
 7. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Epitome,

  I believe in the power of the people! If only people remember they created the constitution they can change it. The problem is we have give the constitution it own life beyond our own creation.

  So, yes, we could speak of change and i see it coming as people have begun to question things, and let no one pretend we have answers! As no one hold the whole truth! Let people question as is the only way the government can stay in check. We can never pretend to know the right pass, but we know for sure silence will not take us anywhere! and not knowing people stands will never move forward!

  As people we are saying we are tired of corruption, and we are confused about it. Let stand in our confusion with set of questions. Let us form our positions and that how we can move forward. It is until the citizens where this country should go, we will move forward, and that decision can only be reach if individual decide what they want to do in the election of 2010

  Franklin D. Roosevelt, First Inaugural Address, 1933 just keep it simple on the power of the people.

  "If I read the temper of our people correctly, we now realize as we have never realized before our interdependence on each other; that we can not merely take but we must give as well; that if we are to go forward, we must move as a trained and loyal army willing to sacrifice for the good of a common discipline, because without such discipline no progress is made, no leadership becomes effective. We are, I know, ready and willing to submit our lives and property to such discipline, because it makes possible a leadership which aims at a larger good. This I propose to offer, pledging that the larger purposes will bind upon us all as a sacred obligation with a unity of duty hitherto evoked only in time of armed strife."
   
Loading...