Salama wakuu ! Naombeni kujua wigo wa hii course ilitajwa hapo juu . kuhusu field zake maana kuna mdogo wangu anang'ang'ania. Mimi kama kaka yake sina ujuzi na hiyo course
Naeleza japo kiduchu yale ninayoyafahamu kuhusu hiyo kozi (ANEB).
Kimsingi ni kozi ya UCHUMI na BIASHARA iliyojikita katika kilimo na maliasili kuliko kuwa kozi ya KILIMO na MALIASILI iliyojikita katika uchumi na biashara.
Inatolewa na UDSM (College of Agricultural sciences and fisheries technology) na mwaka huu ndio itakua ni intake ya pili (ilianza mwaka jana). Ni kozi ya miaka mitatu na habari njema ni kwamba ni yenye kipaumbele cha mkopo.
Hapa unakua mchumi (kama mchumi mwingine) ila unakua umejikita zaidi kwenye kilimo na maliasili.
NIELEZE KWA MFANO;-
Huyu ni mtu anayeunganisha uzalishaji na fedha, mkulima wa nyanya analima nyanya zake, anapalilia, anaweka mbolea, dawa za kuulia wadudu n.k kwa gharama kubwa halafu mwisho wa siku soko hakuna (naamini umesikia watu wamelisha mifugo nyanya au kisado cha nyanya kinauzwa elfu moja). Sasa huyu ndio wa kulitatua hili tatizo kwa kumpa mkulima habari za masoko na biashara nzima ya kilimo.
Vivyo hivyo kwenye nyama, ngozi, maziwa, mayai, asali, nta, mchele na mengineyo mengi. Pia ana msaidia mkulima namna ya kuzalisha kiuchumi.
FIELD ZAKE:-
Serikalini, taasisi na mashirika yanayojihusisha na kilimo-biashara, taasisi za utafiti kwenye kilimo na maliasili, mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na kilimo na maliasili n.k
Kujiajiri;-
Anaweza kujiajiri kwa kufungua consultation firm yenye kujihusisha na utafutaji wa masoko (ya ndani na ya nje) ya mazao mbalimbali ya kilimo cha mazao, ufugaji mifugo, samaki, nyuki, na maliasili zinginezo.
Uandaaji wa miradi (tena hii ina hela mmmh) undaaji wa maandiko ya biashara (business plan) hasa katika sekta tajwa na mambo kadha wa kadha.
Nisikuchoshe:-
1. Siwezi kusema ni kozi nzuri au mbaya (maana itategemea yeye/nyie mnataka nini)
2. Sio kozi ya KUSOMEA KAZI (kama ambavyo daktari anavyokua anajua toka akiwa chuoni kwamba akishamaliza ataenda kufanya kazi kwenye hospitali ya Amana, Mirembe, Mafinga hospital au yoyote nyingineyo).
Kwa mengine ya ziada karibu. Niishie hapa wachangiaji wengine nao watie maneno.
Back to Maombi.