Agribusiness in Tanzania

JOFFREY BARATHEON

Senior Member
Jun 26, 2014
107
195
Hapa siongelei kilimo cha eka mbili tatu hapa nazungumzia kilimo cha kufa mtu kama wanavyofanya USA, Australia na nchi zinginezo

Swali Kwa nini wafanya biashara wakubwa kama akina Mohammed Enterprises na Bakhressa hawakujikita vilivyo kwenye kilimo hichi ?

Mo Enterprises naona wao ni wanunuzi tuu wa nafaka toka kwa hao hao wakulima wadogo wadogo lakini sijaona vigogo wa Agribusiness Tanzania

Tatizo ni nini ukizingatia serikali ya Tanzania tena wakati wa Pinda ilikuja na kilimo kwanza na mengineyo?

Je serikali inashirikisha vipi chuo cha kilimo cha Sokoine ? Kwa nini serikali kupitia TIC, chuo cha sokoine na TCCIA na Big Results now hawajatoa au hawajaweka data online ili mtu ujue fursa ziko wapi na kilimo kipi kinawezekana wapi?

Naamini kuwa kama tutapata mitaji (hapa nazungumzia mtaji wa up to $30 million) na pia kuingia JV na mashirika makubwa ya agri business duniani within 5 yrs Tanzania itatoa Africa's 1st Agri billionaire kwa sababu soko tayari lipo ndani hata kabla hatuja export nje...

Naomba tubadilishane mawazo kwenye hili jambo
 
Inawezekana "risk" za kilimo ni nyingi sana kiasi kwamba Mohamed anaona ni bora kununua mazao tu.
 
Tatizo tunataka wengine wafanye siyo sisi tufanye. Kwa nini unaongelea wafanyabiashara wakubwa waliofanikiwa tayari,huoti ndoto ya wewe kufanya ili uwafikie na kuwapita? Kwa taarifa yako Mo analima. Ninayafahamu mashamba yake ya mkonge na chai.Bakhresa ameanza kulima baadhi ya mazao na anaongeza thamani katika viwanda vyake mwenyewe. Tuanze mimi na wewe kuyatenda tunayoyawaza.
 
risks associated na katani ni ndogo sana, mwambie alime ufuta kama atakubali....ila ndio kati ya wanunuzi wakubwa wa ufuta.
katani inalimwa na wahindi na waarabu kwa nia ya kuhodhi ardhi mashamba ni maelfu ya maekari na mengi hayapo mbali sana na miji.
 
hao wametajirikia biashara hivyo ni kitu wanakijua vizuri. kusema waanze kulima wakati tayari ni matajiri ni kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya.
 
Kilimo Afrika kama huna mtaji wa maana utaishia lia
Wekeza vizuri zaidi weke hela ya maana utajua mwisho wa siku
 
Mazingira na sera siyo rafiki utafirisika.
Pia kuna siasa zimeingilia nimesha ona makampuni makubwa ya kilimo yanavyo hangaika na mazao yao kwa kufungwa mipaka hawarusiwi kupeleka nje ya nchi hata Kama umepata soko zuri ,
 
kilimo kinawezekana.

Ila ushauri mzuri ni kuanza kidogo kidogo. Ukiwa na malengo written ya kumiliki viwango hivyo
 
Back
Top Bottom