Agiza simu yoyote original /tablet unayoitaka kutoka Ebay/ U.S.A!

Agiza simu yoyote original /tablet unayoitaka kutoka Ebay/ U.S.A!

ni htc kwani samsung wanazo wengi nami nataka yangu tofauti kabisa je KAMPUNI YA LG hawana simu za aina hizo za smartphone au?
simu za smartphone nyingi waweza chomeka cable kwenye computer, be specific jina la simu gani kwa maana ya brand name (samsung/nokia/iphone/htc etc) pia na model namba yake.
 
Online shops huwa zina gift cards or discount coupons, how do they apply to your services?
kama site kwa muda huo itakuwa inatoa hizo vitu tutazitumia ili upate punguzo zaidi. sababu sio site zote wanatoa hizo vitu, na hata kama wakitoa huwa ni za msimu tu.
 
Mkuu ni HTC One hivo hivo, achana na hizo One X wala One V or S.
Ni new version ya HTC, wametoa hivi karibuni.
okay, brand new in box 750usd including shipping up to TZ,
$T2eC16RHJHcFFkB!wvffBRbGteLL3Q~~60_12.JPG
 
Duh! Yaani mtu una hela, wataka kuagiza kitu ebay au kwenye mitandao mingine, kwa nini upitie kwa mtu mwingine? Kama mtu ana account ya benki si ajiunge na huduma kama za paypal n.k ili kuweza kuagiza vitu online mwenyewe na si kupitia kwa mtu wa pili na kuanza kuchajiwa gharama za ziada? Kweli ujinga wa wengine ni ajira kwa wengine.

mkuu kwahiyo wanaokwenda kununua magari show-room na wanajua kuagiza lakini hawaagizi japan na wao ni wajinga? au wanaokwenda kula kwa mama ntilie au hotel na wanajua kusonga ugali nao ni wajinga?? hizi ni vitu vya kawaida sana kwa nchi zilizoendelea, kuna wengine hawataki complications wanataka tu baada ya siku kadhaa apewe simu mkononi . Plse no more qoutes.
 
safi nimeipenda hiyo ila bianfsi mmi ni muoga sana kuumizwa pamoja na kuwa ni kweli kwamba unafanya malipo ofisini na unapewa risiti lakini wabongo akissha kusanya usd za kutosha anaweza kusepa na hata mkimfungulia mashitaka ataatoa sababu na yupo radhi kesi iende mahakani na hat aikilipa ataloipa kwa installment.
 
Mkuu, hujazungumzia kabisa suala la kodi na TRA vp, una utaalamu wa kuwanyima MaCCM ulaji ama imekaaje hapo??Tusaidie kujibu hapo usijetuchakachua na hidden cost!!!!Now
 
Mnapokea order za electronics za magari,kama redio,obd2 scanners,alarms?
 
Online shops huwa zina gift cards or discount coupons, how do they apply to your services?
ha ha ha ha swali zuri sana mkuu nimecheka sana maana umefikiria kitu ambacho nilikuwa nimesahau hicho kitu, nahisi ni faida kwa mnunuaji tu
 
mleta mada atachanganyikiwa na maswali duh maana kila mtu na lake
 
Nahitaji sana nokia 3310 nipm

upo serious kweli unaitaka hii simu?! sababu gharama ya shipping tu inazidi gharama ya simu! 60usd including shipping hadi TZ. Hivyo sikushauri, ukizungu-zunguka kkoo unaweza ipata hii simu. Karibu
 
Mkuu, hujazungumzia kabisa suala la kodi na TRA vp, una utaalamu wa kuwanyima MaCCM ulaji ama imekaaje hapo??Tusaidie kujibu hapo usijetuchakachua na hidden cost!!!!Now

kwa avarage shipping time ninayo-i-approximate max 3 weeks /economy shipping huwa hawajali sana kuhusu vi-furushi vidogo, hivyo huwa no tax kwa economy shipping. EMS ndio huwa wananajali kila kitu lazima wakusindikize kulipa Maccm, lakini vivile uzoefu huwa unatumika, nafikiri umenielewa. usihofu, No hidden costs everything will be open. Karibu
 
Kampuni yetu inahusika na kuagiza na kuuza vitu vya electronics, computers, laptops, projectors etc. Kutokana ni ngumu kuagiza simu chaguo la kila mteja anayoitaka, tunachukua fursa hii kuwapa nafasi wateja wetu kutoa order ya simu/tablet anayoitaka, alimradi bajeti ya hiyo simu/tablets haizidi 500$.

Kwanini uagize simu/tablet toka usa?
una uhakika na u-orijino wa bidhaa unayoagiza, na pia unapata unafuu wa bei kwa bidhaa husika kulinganisha na ungenunua hapa tz, au na wakat mwingine unachokitaka hakipo kabisa tz.

Utaratibu unakuwaje basi?
weka jina la simu unayoitaka hapo chini, then nitakupa makadirio ya mchanganuo wa gharama wa hiyo simu ukijumlisha shipping mpaka unaipata mkononi. (makadirio ya simu unayoitaka yanaweza badilika wakati wowote)

Search hiyo simu au product kwenye online site yoyote ya Marekani, ebay/amazon/walmart then utupe link, hata wanazoship usa only tutakusaidia kulipia, na kupata hicho kitu in a max time of 3 weeks. (Express shipping by EMS ipo na haichukui not more than 10 days, ukiwa ready tutajadili faida na hasara zake)

sababu ni spesho order, mteja utalipa pesa yote ya simu/tablet in advance, kuepuka kuagiziwa simu inakuja halafu mteja analeta sababu nyingine. Malipo yote yatafanyika ofisni tu, na utapatiwa receipt kama ushahidi wa malipo ya gharama za kuagiza simu.

Kitachofuata ni wewe kusubiri wiki 3 tutakukabidhi simu yako. Zikipita siku 45 toka siku uliyopress order yako hujapata simu yako tutakurudishia pesa yote in full amount.

Simu/tablet ukishaletewa utatulipa 15% ya gharama ya simu/tablet jumlisha shipping kama ujira wetu wa kukuagizia simu, halafu ndipo simu utapatiwa mkononi mwako.

Ofis zetu zipo jengo la RUBADA, Ubungo Shekilango, ni nyuma ya jengo la Ubungo Plaza, baada ya Blue Pearl kuna barabara isiyo na lami inaingia ndani, mbele yako utaona ghorofa la rangi kijani/njano iliyopauka, ground floor ndipo ofisi zetu zilipo.

Changamoto na maswali yanaruhusiwa, but please kama thread haikuhusu save your jokes and non senses for other threads.

Note: Thread hii haifundishi kuagiza simu/product from online site au usa kwa namna yoyote, kama una swali kama hilo hapa sio mahala pake, sitajibu message yoyote wala usinisumbue kwa call ya namna hiyo. Asante

CLEVA TECHNOLOGIES, RUBADA building, Rubada Street, Ubungo Shekilango Box 4238 Dar Es Salaam Phone: 0714-345958 / 0752-858693

Serious clientele send pm or call 0714-345958 / 0752-858693

Kaka nipe kwanza bei ya iPad 3 na Sony Xperia Z kwa marekani kisha tutaongea baishara.
 
safi nimeipenda hiyo ila bianfsi mmi ni muoga sana kuumizwa pamoja na kuwa ni kweli kwamba unafanya malipo ofisini na unapewa risiti lakini wabongo akissha kusanya usd za kutosha anaweza kusepa na hata mkimfungulia mashitaka ataatoa sababu na yupo radhi kesi iende mahakani na hat aikilipa ataloipa kwa installment.
ni kweli lazima uwe makini, lakini nakuhakikishia hayo unavyosema kwetu hayawezi tokea, ukiwa serious unahitaji huduma yetu na ukitaka uthibitisho wowote ili uwe na uhakika wa usalama wa fedha zako, tutakupa. karibu
 
Kaka nipe kwanza bei ya iPad 3 na Sony Xperia Z kwa marekani kisha tutaongea baishara.

sony experia z 700usd by economy including shipping (max 3 weeks)up to tz, 720usd by EMS (max 10 days) including shipping up to tz. IPAD 3 funguka specifications unazotaka, screen inch ngapi 7" or 10", internal mem ngapi 16gb or 32gb or 64gb ?
 
Hongera kwanza kwa kurahisisha!
Swali langu ni hivi!!
Mnaagiza simu peke yake? Au na bidhaa nyingine! Mfano saa na jewels.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Hongera kwanza kwa kurahisisha!
Swali langu ni hivi!!
Mnaagiza simu peke yake? Au na bidhaa nyingine! Mfano saa na jewels.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

Thank you for the appreciation. tunaagiza simu na computers things sababu ndivyo tunavijua vizuri kwa maana ya specs ubora na n.k ili kujihakikishia tunakuwa na uhakika na tunachoagiza. mfano kama hizo jewels hatuzijui vizuri , hapo itakuwa ngumu.
 
Back
Top Bottom